Ujumbe kwa wanachuo

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,338
MWAMBIE MDOGO WAKO

Mkumbushe ndugu au rafiki yako kuwa maisha ya CHUO ni sawa na BONGO MOVIE watu wengi huigiza. Hata yule alie tokea Mbeya vijijini atasema kwao Jijini Mwanza...

1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma uhasibu akawa dobi,Anaweza kusomea Sheria akawa boda boda.

2. Mwambie Kufaulu taaluma sio kufaulu maisha.wapo watu wenye elimu kumzidi yeye ila hawana ajira,Hata wenye ajira bado maisha magumu

3. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji,Ila akumbuke anatokea kijijini tena kule ndanindani... Hivyo asijikweze ili aonekane.

4. Mwambie Marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester, akumbuke chuo ndiko mlokole na Sheikh wote hujifunza Kulewa na kuvaa nguo za ajabu.

5 .Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni, hivyo aepuke wapenda starehe watamaliza pesa zake .

6. Mwambie Boom huwa linakuja ila Laki tano ya chuoni sio Laki tano ya nyumbani, hela ya chuoni huisha haraka tena bila mpangilio hivyo awe makini na matumizi yake.

7. Mwambie kama ni wa kike,marafiki zaidi ya 3 hatoweza kudumu nao. Watagombana tu.

8. Mwambie chuoni hakuna NDOA ila kuna uzinzi, Hivyo aachane kubeba majukum ya ndoa ikiwa kaenda kusoma, kwani Mapenzi CHUONI ni sawa na vitoroli vya Super Market ukimaliza kutumia unakiacha hapo hapo.

9. Mwambie awe na msimamo na asikurupuke kuanzisha mahusiano chuoni ikiwa nyumban ana mtu anae mpenda kwa dhati, Chuon kuna watu wapo kuharibu Malengo ya wengine awe makini.

10. Mwambie wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanajua kila kitu na wako juu ya sheria hivyo kama ni wa kike ajifunze kusali.

11. Mwambie Chuoni kuna Makanisa na Misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 10,000 lakini waumini ni wachache, Akumbuke kusali.

12. Mwambie kama ni wa kike kuwa aridhike na hali ya nyumbani, asifikirie kutafuta SPONSOR ili kupunguza ugumu wa maisha kwani Atajiingiza katika matatizo makubwa

13. Mwambie Simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima... Hivyo asipende kutumia vibaya pesa kuna siku atazikumbuka akimaliza masomo.

14. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau...

15. Mwambie Aepuke marafiki wanao mfundisha kutafuta wanawake au wanaume.

15. Mwambie asiwadharau watu ambao hawajapata nafasi ya kufika chuo, Siku akimaliza chuo wapo atawakuta wana biashara kubwa.

16. Mwambie chuoni kuna watumishi wanao jiendeleza na wanaendelea kupokea mshahara yao, wengi ni waume na wake za watu.. Hawa ndio hutumia pesa kulaghai mabinti na vijana.

17.Mwambie baada ya kumaliza masomo haimaanishi amefanikiwa maisha, Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia,

18. Mwambie Anapo waona kaka na dada zake wamemaliza chuo ila wapo tu mtaani asifikiri ni wazembe ila usawa na mfumo unabana sana.

19. Mwambie Maisha ni mafupi sana adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazurii, Lastly Asimdharau mtu yeyote, mkumbushe kuzingatia kuna maisha baada ya chuo...

Asisahau mtaani kugumu, kuna Mabinti wenye DEGREE zao wana amua kuolewa na vibabu, nao vijana kutembea na wazee sababu ya kukosa mlo...

Atambua kuwa leo hii dereva boda boda au bajaji ana uhakika wa kuilisha familia yake kila siku kuliko muhitimu wa chuo kikuu.

Hivyo asiwe na dharau kuwa hawezi kuolewa na mtu mwenye elimu ya chini pia akumbuke sio kila dereva au konda hajasoma, kuna watu wana vyeti vyao na ufaulu mzuri.

Kama haelewi basi tumuache, Tumsubiri akimaliza kusoma.

IKIKUFAA IFANYIE KAZI

MUNGU AWAONGOZE KATIKA NJIA ILOYOSAHIHI NA AWAPE UJUZI UTAKAOWASAIDIA HATA KAMA WATAKOSA AJIRA.

Cc: Fahamu Leo

Na Emmanuel Kasomi
 
Tatizo vijana wakifika chuo huwa wanajipa matumaini makubwa na kudhani maisha wameshayapatia.

Kijana anawadharau aliowaacha mtaani kwa kufikilia kuwa wamepoteza "future" katika maisha bila kutambua kuwa akiludi mtaani baada ya kuhitimu masomo ya chuo atawakuta watu walewale aliowaacha mtaani.
 
Wiki iliyopita picha nyingi zimepigwa na wahitimu katika vyuo tofauti. Ili swala la picha unalizungumzia vipi maana naona umelisahau ?
 
Hili bandiko umelikopi kutoka bandiko lingine nmesahau jina la ule uzi..ni vizuri ukifanya hivi ukatoa na credits kwa muhusika mwenye bandiko lake.
Mkuu ungesoma vizuri usinge lalamuka ndo maana nikaandika
Cc: Fahamu leo
 
MWAMBIE MDOGO WAKO

Mkumbushe ndugu au rafiki yako kuwa maisha ya CHUO ni sawa na BONGO MOVIE watu wengi huigiza. Hata yule alie tokea Mbeya vijijini atasema kwao Jijini Mwanza...

1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma uhasibu akawa dobi,Anaweza kusomea Sheria akawa boda boda.

2. Mwambie Kufaulu taaluma sio kufaulu maisha.wapo watu wenye elimu kumzidi yeye ila hawana ajira,Hata wenye ajira bado maisha magumu

3. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji,Ila akumbuke anatokea kijijini tena kule ndanindani... Hivyo asijikweze ili aonekane.

4. Mwambie Marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester, akumbuke chuo ndiko mlokole na Sheikh wote hujifunza Kulewa na kuvaa nguo za ajabu.

5 .Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni, hivyo aepuke wapenda starehe watamaliza pesa zake .

6. Mwambie Boom huwa linakuja ila Laki tano ya chuoni sio Laki tano ya nyumbani, hela ya chuoni huisha haraka tena bila mpangilio hivyo awe makini na matumizi yake.

7. Mwambie kama ni wa kike,marafiki zaidi ya 3 hatoweza kudumu nao. Watagombana tu.

8. Mwambie chuoni hakuna NDOA ila kuna uzinzi, Hivyo aachane kubeba majukum ya ndoa ikiwa kaenda kusoma, kwani Mapenzi CHUONI ni sawa na vitoroli vya Super Market ukimaliza kutumia unakiacha hapo hapo.

9. Mwambie awe na msimamo na asikurupuke kuanzisha mahusiano chuoni ikiwa nyumban ana mtu anae mpenda kwa dhati, Chuon kuna watu wapo kuharibu Malengo ya wengine awe makini.

10. Mwambie wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanajua kila kitu na wako juu ya sheria hivyo kama ni wa kike ajifunze kusali.

11. Mwambie Chuoni kuna Makanisa na Misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 10,000 lakini waumini ni wachache, Akumbuke kusali.

12. Mwambie kama ni wa kike kuwa aridhike na hali ya nyumbani, asifikirie kutafuta SPONSOR ili kupunguza ugumu wa maisha kwani Atajiingiza katika matatizo makubwa

13. Mwambie Simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima... Hivyo asipende kutumia vibaya pesa kuna siku atazikumbuka akimaliza masomo.

14. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau...

15. Mwambie Aepuke marafiki wanao mfundisha kutafuta wanawake au wanaume.

15. Mwambie asiwadharau watu ambao hawajapata nafasi ya kufika chuo, Siku akimaliza chuo wapo atawakuta wana biashara kubwa.

16. Mwambie chuoni kuna watumishi wanao jiendeleza na wanaendelea kupokea mshahara yao, wengi ni waume na wake za watu.. Hawa ndio hutumia pesa kulaghai mabinti na vijana.

17.Mwambie baada ya kumaliza masomo haimaanishi amefanikiwa maisha, Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia,

18. Mwambie Anapo waona kaka na dada zake wamemaliza chuo ila wapo tu mtaani asifikiri ni wazembe ila usawa na mfumo unabana sana.

19. Mwambie Maisha ni mafupi sana adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazurii, Lastly Asimdharau mtu yeyote, mkumbushe kuzingatia kuna maisha baada ya chuo...

Asisahau mtaani kugumu, kuna Mabinti wenye DEGREE zao wana amua kuolewa na vibabu, nao vijana kutembea na wazee sababu ya kukosa mlo...

Atambua kuwa leo hii dereva boda boda au bajaji ana uhakika wa kuilisha familia yake kila siku kuliko muhitimu wa chuo kikuu.

Hivyo asiwe na dharau kuwa hawezi kuolewa na mtu mwenye elimu ya chini pia akumbuke sio kila dereva au konda hajasoma, kuna watu wana vyeti vyao na ufaulu mzuri.

Kama haelewi basi tumuache, Tumsubiri akimaliza kusoma.

IKIKUFAA IFANYIE KAZI

MUNGU AWAONGOZE KATIKA NJIA ILOYOSAHIHI NA AWAPE UJUZI UTAKAOWASAIDIA HATA KAMA WATAKOSA AJIRA.

Cc: Fahamu Leo

Na Emmanuel Kasomi
Umetisha Sanaa,,,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom