Ujumbe kwa mke na mume

Ujumbe kwa mke na mume

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
15,270
Reaction score
29,938
Nipo kazini mara nasikia simu yangu ya mkononi ujumbe ukiingia, nachukua kuangalia ni nani na nini..nakutana na ujumbe huu na maagizo :-

Kuwa "wape wanandoa wote unaowafahamu ujumbe huu.
Mungu na awatie nguvu!! Ameeeen....!!" Na kwa vile najua wengi ninaowafahamu wanapita hapa nikaona itakuwa njia nzuri kuweka hapa...na ujumbe wenyewe ni kama ifutavyo:-
"Ukiona mko vizuri kwenye ndoa, Usimsifu mumeo/mkeo, Endelea kumtukuza Mungu na kuweka maombi ya akiba.
Usitoke bila KUMWOMBEA mkeo/mumeo.
Jifunze pia kumwelewa mwenzako na kutokuuona udhaifu wake kama sababu ya wewe kumfanyia mabaya. Zungumza naye, mtie moyo, mshauri katika usiyoyapenda, mweleze uliyonayo.
Ondoa maswali nafsini mwako. Pata majibu sahihi kutoka kwake.
KUMBUKA NI NYAKATI ZA MWISHO.

Taasisi ya shetani isiyotaka ichanue ni NDOA. Ikiharibika familia nayo inaharibika.

TAFAKARI"..
 
Duuuhh kazi yake.

Tatizo letu Waafrika tunapigana na "ADUI" tusiemjua.

Ni kweli Mungu yupo lakini sisi waafrika tumemgeuza Mungu "hirizi" na shetani "kichaka" cha uovu.

Jambo lolote huanza ndani ya nafsi na maanisha "DHAMIRI". Ili kuondokana na matatizo kwenye ndoa tunahitaji kudhamiria. Nilipata uzoefu kidogo Japan. Japan dini hazina ushawishi na DINI kubwa ya wajapani ni kazi, lakini dhamira zao zimewatuma kuishi maisha yasiyo ya kinafiki.

Shetani ni wewe na Mungu ni wewe. DHAMIRI ikutume ufanye yaliyo MEMA katika Ndoa yako.
 
Back
Top Bottom