Valentina
R I P
- Oct 12, 2013
- 24,688
- 28,850
**MUME NA MKE JITAMBUENI ILI MUISHI KWA FURAHA**
[HASHTAG]#MUME[/HASHTAG]
Mke wako si nguo, kwamba ikichakaa utanunua nyingine, Mke wako ni kitu chema toka kwa Mungu, huwezi kuweka mbadala wake, iwe fedha au awe mwanamke mwingine. Ni Mungu tu ndiye akupaye mke, hapatikani sokoni, wala dukani. Hapatikani hotelini wala bar, si shereheni wala msibani, hapatikani njiani wala kijiweni. Mke mwema mtu hupewa na Bwana.
Moyo wa mke wako wako na viungo vyake vingine si vipuri (spare) vya gari kwamba ukivunjika au kuharibika utaung'oa na kuweka mwingine. Huwezi kuununua kwa fedha, wala thamani ya dhahabu ya dunia nzima hailingani na thamani ya moyo wake. Kwa hiyo haununuliwi kwa fedha na hauna mbadala, ni vyema ukautunza na ukamtunza mkeo kwa gharama ya nafsi yako; ukijitoa nafsi yako kwake, unatoa na vyote ulivyonavyo wewe, na cha kwanza ni muda wako wote, upendo, upole wako, unyenyekevu wako, uvumilivu wako, yaani, maisha yako yote.
[HASHTAG]#MKE[/HASHTAG]
Mume wako si mashine ya ATM kwamba account yako inapoishiwa huoni thamani ya kwenda kwake. Mume wako ni mume wako, thamani yake si kile alichonacho nje, ni kile alichonacho ndani, na hicho huwa hakiondoki kwa sababu hana kitu mikononi cha kukupa.
Kama mke, wewe ni mlinzi wa thamani aliyonayo mumeo ndani yake, ukiteleza ameteleza, ukianguka ameanguka.
Mume wako ni maalumu kwa mahitaji ya moyo wako na si mahitaji ya mwili wako kwanza. Kabla hajaweza kutimiza mahitaji ya mwili wako (kama vile nguo, Viatu, gari nzuri, nyumba nzuri, salon nk.) angalia ni kiasi gani anaweza kutimiza mahitaji ya moyo wako ambayo ni upendo, kujali, kukuthamini; Kama ana upendo na anakujali na kukuthamini, atajitoa kwa ajili yako kwa moyo wake wote ili kuushibisha moyo wako na upendo wake kwako, kwa nguvu zake zote ili kukutendea mema, kwa akili zake zote ili asije kushindwa kuishi na wewe, na kwa vitu vyakev vyote alivyonavyo ili autunze mwili wako.
#MUME_NA_MKE
Thaminianeni na kuheshimiana si kwa sababu ya vile vinavyoonekana machoni penu na machoni pa wengine, bali kwa vile visivyoonekana, vya ndani. Maana vinavyoonekana si vya kudumu, ni vya muda tu, bali visivyoonekana ni vya milele.
Mke ni kitu kisichoonekana, ni umbo la ndani si umbo la nje. Umbo la nje si la kudumu, linaweza kutoweka wakati wowote; umbo la nje ni pamoja na umbile la mwili wake, viungo vyake, sura yake, mwonekano wake. Hivi vinamfanya yeye awe mwanamke, wala havimfanyi yeye awe mke. Na kwa sababu hiyo, si kwamba vikibadilika na mke anabadilika, vikiondoka basi eti na thamani ya mke inakuwa imeondoka. HAPANA. Mke adumu, yeye ni umbo la ndani si la nje.
Mume naye ni vivyo hivyo, ni kitu kisichoonekana, ni umbo la ndani na si umbo la nje. Vile alivyonavyo nje kama uzuri, umbile, mali na pesa havimfanyi kuwa mume, wala vile asivyonavyo kwa nje havimfanyi asiwe mume. Moyo wake na tabia yake kwa mkewe ndio humfanya yeye kuwa mume.
Mke mthamini na umtii mume wako, Na mume, mpende na kumjali mke wako si kwa sababu ya alivyonavyo nje, bali kwa sababu ya vile yeye mwenyewe alivyo kwako.
Hii nimekopy na kupest tu....