Natumbua jipu la mwisho 2015, je upo kwenye penzi zito na mume/mke wa mtu?

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
NATUMBUA JIPU LA MWISHO 2015

JE UPO KWENYE PENZI ZITO KWA MUME/MKE WA MTU?

Sina shaka utakuwa umeshawahi kusikia kuhusu mtu aliyefumaniwa na mke/mume wa mtu. Inawezekana umeshashuhudia ugomvi kati ya wanandoa wanaotuhumiana kuhusu kutoka nje ya ndoa zao.

Kimsingi si tabia nzuri katika jamii, lakini ipo na watu waliopo ndani ya jamii hiyo hiyo. Kwa sababu tabia hii imeshamiri sana, hasa sehemu za mijini ndiyo sababu nikaamua kuzungumza na wenye tabia hizo.

1. UNASALITIWA
Kwanza kabisa unatakiwa kufanya kitu kimoja, kama upo kwenye penzi na mtu ambaye yupo kwenye ndoa yake, ni wazi kwamba hata wewe unasalitiwa. Kama aliweza kutoka nje ya ndoa, anashindwa vipi kutafuta mwingine/wengine?Mtu ambaye ameweza kugeuka kiapo alichokula katika ndoa, kwa kutembea na wewe, unadhani wewe una thamani gani kubwa hadi ashindwe kuwa na mwingine nje yako na mume/mkewe? Hili ni jambo unapaswa kulijua ili kuona kama upo tayari kuwa katika uhusiano wenye mtungo wa wenzi wengi.

2. JIANDAE KWA MAUMIVU
Waswahili wanasema: “Mke wa mtu sumu.” Siku hizi wameongeza kwamba hata mume wa mtu pia ni sumu. Tukiachana na maneno ya kiswahili, kisaikolojia, unapomtendea mwenzako jambo lisilo jema, basi nawe unatakiwa kujiandaa kuumizwa.
Kwa sababu umeamua kutoka na mwanaume au mwanamke ambaye unajua wazi ana ndoa yake, basi ujue wazi kuwa hata wewe kwenye ndoa yako, mume au mkeo naye atakusaliti.Tukiachana na suala la kisaikolojia, kiimani pia imekatazwa. Vitabu vitakatifu vimeagiza si tu watu wasitembee na watu waliopo kwenye ndoa zao, bali hata kuwatamani tu ni kosa sawa na mengine.Yote kwa yote, ukae ukitambua kuwa, maumivu ambayo unayasababisha leo hii kwenye ndoa ya mwenzako, yapo njiani kukufikia hata wewe hapo baadaye.Si lazima mkeo/mumeo awe na tabia kama yako, lakini lipizi lolote linaweza kufanyika ili kufanya ndoa yako iwe chungu kama ulivyofanya kwa mwenzako.

3. UNAJIWEKA KWENYE HATARI
Suala la usaliti lina maumivu makubwa sana, ukiachana na suala la maumivu, linaathiri mambo mengine kifamilia. Inawezekana wewe kwa kutoka na mke/mume wa mwenzako, akashindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo kama mwanandoa na hivyo kuwa tatizo kwa mwenzako.Hili lipo sana na wengi mnafahamu, kuwa kuna watu ambao huamua kuweka mitego ya fumanizi ili kukuchafulia. Hatari iliyopo hapo ni picha zako kusambazwa kwenye mitandao au mitaani. Ni aibu kiasi gani?Nakumbuka kuna wakati dada mmoja, mkazi wa Magomeni, Dar akiwa ndiyo kwanza ametoka kufunga ndoa yake, akaanza mchezo wa kumsaliti mume wake. Jamaa alivyogundua, akaweka mitego. Mwishowe akamfumania, akampiga picha za utupu na kuzisambaza mitaani kisha akaachana naye!
Wengine huwa wakatili zaidi, unaweza kukodiwa wahuni wakakuumiza au hata kukuua kabisa. Kwa nini uishi kwenye hatari kubwa kiasi hicho? Kwa nini usitafute wako wa peke yako na ukaishi kwa amani?

4. HAKUNA PENZI LA KWELI
Unachotakiwa kubaki nacho ni kwamba, mwanandoa ambaye anaacha nyumba yake na kukufuata, inamaana kwamba amekuja kwako kujistarehesha na si kwamba anakupenda.
Hata kama anakupenda, jiulize ilikuwaje akaingia kwenye ndoa na mwenzi wake halafu anakuwa na wewe? Ndoa ni muunganiko mkubwa ambao lazima wahusika wawe wamependana kwelikweli ndipo wakubaliane kuifunga.Kama ameweza kuisaliti ndoa yake, anawezaje kukupenda wewe kwa penzi la dhati? Ni mwanaume/mwanamke gani mwenye thamani kama aliye naye kwenye ndoa? Kama upo katika kundi hili ujue unajistarehesha tu, hakuna upendo wa kweli kati yenu.Kwanza utapendwaje na mtu ambaye tayari alishapenda na kuingia kwenye kiapo cha ndoa?

5. ZINGATIA
Kutoka kimapenzi na mtu ambaye ana mwenzake waliye katika muunganiko wa ndoa ni dhambi kubwa. Hutakuwa na uhuru naye na kwa kiasi kikubwa hata nafsi yako itakuwa inakusuta kuwa wewe ni mwizi!Una sababu gani ya kuishi maisha ya presha? Maisha ya kujilinda na kuchagua viwanja vya kwenda? Maisha yako yana thamani kubwa sana. Wapo wengi ambao hawapo ndani ya uhusiano na unaweza kutengeneza nao penzi zito na la kipekee!Kusoma maandishi haya ni kitu kimoja na kuyafanyia kazi ni kitu kingine. Uamuzi upo mikononi mwako.

2016 inakuja vijana BADILIKENI.
 
Last edited by a moderator:
Acheni ujinga jamani.......mwenzenu anawapa maneno ya hekina nyie mnamchukulia poa.......sio fresh.........

Ndugu mwandishi nashukuru sana kwa maneno yako ya kujenga......MUNGU akubariki sana best yangu
 
Tunaishi mara moja tu.
Hayo maneno yote ni namna tu ya wenye ndoa kulinda ndoa zao. Ila kiukweli anaetembea na mke/mume wa mtu wala hana maumivu makali sawa na mke/mume halali.
Lindeni ndoa zenu ila sio muhangaike na hao wa nje. Ndoa zenu HAZIWAHUSU.
Humu kila mwanandoa akiamua afunguke awe mkweli kabisa hawakosekani wenye MAPENZI MAZITO KWA MCHEPUKO KULIKO MWENZI WA NDOA.
Kikubwa ni furaha yako ilipo.
Tatizo lipk kwa mwenye ndoa anaekiuka kiapo na kuchepuka. Mtu wa nje ameingiaje?
Kila mtu afanye yake.
Wa ndoa alinde ndoa, mchepuko alinde penzi.

Nyongeza:
Wakati mwingine penzi la nje ndio linalodumisha ndoa.
 
Shikamoo dada
 
Siyo kila mtu aliyeoa ameoa kwasababu tu anampenda mwenzi wake,wengine ni tamaduni zao zimewapelekea kuwa pamoja na kwavile wanakuwa wamezoeana basi inabidi tu waishi ila kiukweli heart issues ni ngumu sana kuzidefine
 
Tunaishi mara moja tu.
Hayo maneno yote ni namna tu ya wenye ndoa kulinda ndoa zao. Ila kiukweli anaetembea na mke/mume wa mtu wala hana maumivu makali sawa na mke/mume halali.
Lindeni ndoa zenu ila sio muhangaike na hao wa nje. Ndoa zenu HAZIWAHUSU.
Humu kila mwanandoa akiamua afunguke awe mkweli kabisa hawakosekani wenye MAPENZI MAZITO KWA MCHEPUKO KULIKO MWENZI WA NDOA.
Kikubwa ni furaha yako ilipo.
Tatizo lipk kwa mwenye ndoa anaekiuka kiapo na kuchepuka. Mtu wa nje ameingiaje?
Kila mtu afanye yake.
Wa ndoa alinde ndoa, mchepuko alinde penzi.

Nyongeza:
Wakati mwingine penzi la nje ndio linalodumisha ndoa.
Hilo kweli wazo lako.
 
Wako akiwa kwako akitoka nje siwako!... kama wewe mkewe/mmewe mbona mie kanitaka?! ha ha haaaa misemo ya kitaani
 
Back
Top Bottom