Ujumbe kwa kina Dada Joyce Kiriya umetisha

3squere

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
925
181
Kutoka kwenye page yake Facebook " Joyce Kiria
Hakianan huu ujumbe nauleta kwako kwa nia njema kabisa kwa ajili ya kumaliza 2013.

we Mwanamke mwenzangu ambae mpaka sasa bado unategemea mwanaume akuendeshee maisha kwa kila kitu, hakika unaitaji Ukombozi..

Siyo dhambi kama ukipata mwanaume anaekugaramia kwa vitu mbalimbali kwa hiari yake na mapenzi yake..siyo kwa kudai kama vile umemwajiri au ulimkopesha!!

Tatizo letu wengine tunawalazimisha wapenzi wetu watufanyie vitu kwa nguvu na asipofanya hivyo Utanunaje sasa!!

Mbaya zaidi Mara nyingi mnaomba vitu ambavyo wapenzi wenu hawana uwezo navyo! Na wewe mwenyewe mwanamke umeshindwa kujiuliza kwamba mbona wewe huna hivyo vitu unavyolazimisha ununuliwe? Yeye akaibe??

Unakuta mtu katongozwa tu! Anaanza oooh kodi imeisha, oooh nadaiwa ada, nataka galax note3, oooh nataka kiwanja, oooh nataka nyumba, oooh nataka gari, vocha, bili ya maji, umeme, nauli ya kwenda kusalimia ndugu na jamaa, oooh simu ya mama, !! Kiruuuuuuuu ndo maana wanaume wenye akili zao wanatoka baru...

Jamani wanaume siyo Migodi! Nao wanatafuta pesa kwa tabu sana.siku hizi maisha ni magumu sana, Ujumbe wangu wa kuanza 2014 Tushirikiane kuleta maendeleo yetu pamoja badala ya kugeuzana ATM...

Huu ujumbe kama umekugusa hakikisha unaingia 2014 ukiwa na mtazamo mpya tofauti na huo wa Kitumwa na epuka kabisa kuwa Mzigo kwa mwenzako....kuwa msaada kwake ili maisha yawe mepesi...

Hata wanaume siku hizi wapo Magolikipa...acheni siyo fresh

Mbutaaaaaa...

NOTE: USISAHAU OPERESHENI TOKOMEZA MICHANGO YA HARUSI NA SHEREHE 2014..Tuchangie maendeleo...
 
Posti kama hii enzi zileeee ungeambuliaje mitusi mpaka uone rangi zote...chezea babavichaaa wewe.....lakini sasa umeolewa na mchadomo a.k.a kigogo..........kwa raha zako mamaa.......
 
Joyce Kiria sikujuwi ila nakupenda kwa haya uliyo andika kama ni kweli. kwa uhakika tunahitaji wanawake kama wewe, yaani wenye kuona mbali na siyo wa kukaa tu saloon na kupiga domo na kudanganyana kama hawana akili.
 
Last edited by a moderator:
Ujumbe safi sana maana siku hizi vituko vya mizinga mpaka inakera. Na ukiamgalia hata mwezi hamjamaliza na yawezekana anajua kipato na majukumu yanayokukabili
 
Hapo mwisho pananihusu saaaana.... Yaan ukipiga hesabu ya michango ya harusi kwa mwaka mzima unaweza kuzimia!!!

Ngoja nifanye mkakati wa KUTOKOMEZA AISEE...

Yaani Mimi hiyo page ya michango ya harusi that chapter I closed it a while ago.
 
Kutoka kwenye page yake Facebook " Joyce Kiria
Hakianan huu ujumbe nauleta kwako kwa nia njema kabisa kwa ajili ya kumaliza 2013.

we Mwanamke mwenzangu ambae mpaka sasa bado unategemea mwanaume akuendeshee maisha kwa kila kitu, hakika unaitaji Ukombozi..

Siyo dhambi kama ukipata mwanaume anaekugaramia kwa vitu mbalimbali kwa hiari yake na mapenzi yake..siyo kwa kudai kama vile umemwajiri au ulimkopesha!!

Tatizo letu wengine tunawalazimisha wapenzi wetu watufanyie vitu kwa nguvu na asipofanya hivyo Utanunaje sasa!!

Mbaya zaidi Mara nyingi mnaomba vitu ambavyo wapenzi wenu hawana uwezo navyo! Na wewe mwenyewe mwanamke umeshindwa kujiuliza kwamba mbona wewe huna hivyo vitu unavyolazimisha ununuliwe? Yeye akaibe??

Unakuta mtu katongozwa tu! Anaanza oooh kodi imeisha, oooh nadaiwa ada, nataka galax note3, oooh nataka kiwanja, oooh nataka nyumba, oooh nataka gari, vocha, bili ya maji, umeme, nauli ya kwenda kusalimia ndugu na jamaa, oooh simu ya mama, !! Kiruuuuuuuu ndo maana wanaume wenye akili zao wanatoka baru...

Jamani wanaume siyo Migodi! Nao wanatafuta pesa kwa tabu sana.siku hizi maisha ni magumu sana, Ujumbe wangu wa kuanza 2014 Tushirikiane kuleta maendeleo yetu pamoja badala ya kugeuzana ATM...

Huu ujumbe kama umekugusa hakikisha unaingia 2014 ukiwa na mtazamo mpya tofauti na huo wa Kitumwa na epuka kabisa kuwa Mzigo kwa mwenzako....kuwa msaada kwake ili maisha yawe mepesi...

Hata wanaume siku hizi wapo Magolikipa...acheni siyo fresh

Mbutaaaaaa...

NOTE: USISAHAU OPERESHENI TOKOMEZA MICHANGO YA HARUSI NA SHEREHE 2014..Tuchangie maendeleo...

Nimependa Operesheni Tokomeza Michango ya Harusi na Sherehe, jamani Tanzania haya ni majanga makubwa. kwanini tutiane umasikini bana???
 
laiti kama ingeruhusiwa mwanamke mmoja aolewe na wanaume zaidi ya mmoja ningemuweka ndani huyu bidada,kaniimpres sana
 
Back
Top Bottom