Ujue utapeli wa 419

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
669
Utapeli wa 419 ni utapeli ambao pia unajulikana kama Lipa Ada Kabla (Advance Fee Scam). Ni utapeli ambao hufanywa kwa kiasi kikubwa nchini Nigeria, na namba 419 ni ‘code’ ya Nigeria ya kitengo cha utapeli

Utapeli huu hufanywa kwa kumuahidi mtu kiasi kikubwa cha fedha aidha kwa kumwambia ameshinda michezo wa bahati nasibu, au kuna mtu anataka kuhamia nchini kwake

Kabla ya mtu kupewa kiasi kikubwa cha fedha alichoahidiwa hutakiwa kulipa hela kidogo, ambayo ni ada ya tozo ya kukamilisha mambo watakayotaja hao matapeli. Ikitokea ukatuma hela hiyo unakuwa umeshatapeliwa hela yako

Ripoti ya Bureau of International Narcotics and Law Enforcement Affairs imesema ziko njia nyingi zaidi za kumfanya mtu atume hela hizo. Na matepeli hao huwapata watu kwa kuwatumia barua pepe, Fax, Facebook nk

Signed
Oedipus
 
Back
Top Bottom