Ujue ugonjwa wa Mba na tiba yake

Unaweza kwenda Moshi KCMC? Wana kitengo cha ngozi effective and efficient you will never regret.

Kwa Dsm nilishawahi kuelekezwa kwa specialist mmoja pale Samora jina limenitoka mzee fulani hivi lakini alichonipa hakikunisaidia kwa sababu mimi nina skin condition ambayo huwa inajirudia baada ya kipindi fulani.

Kwa hiyo nikajirudia zangu kcmc baada ya huduma za huyu wa Dsm kutonisaidia, niliona isiwe tabu.
 
pia namimi naomba nijuzwe dr. bingwa wa fungus. msaada jamani kama kuna mwenye no za simu
 
Nenda muhimbili,muulizie Dr Mboneko au clinic yake. Ukishindwa nenda new OPD ilizia specialist wa ngozi watakudirect
 
Asanteni sana wadau. Ngoja nianzie hapahapa mliponielekeza. Nitarudi kuwapa matokeo. Kwa kweli nimekua nikisumbuliwa sana na ngozi. Naanzia hapahapa Dsm, ikishindikana ntaelekea KCMC.
 
Wana JF naombeni msaada jinsi ya kumpata doctor bingwa wa magonjwa ya ngozi, au hospital nzuri yenye uzoefu na tatizo la ngozi, ninaisha hapa Dar es salaam.

Kwa mawasiliano: sms 0715266772 au e-mail erasto@comsec.co.tz

Asante sana
 
Nenda Muhimbili kule new OPD(specialist wa magonjwa mengi wanapatikana kule),nenda kaweke apointment ya kuonana na huyo specialist wa tatizo lako.
 
Wana JF naombeni msaada jinsi ya kumpata doctor bingwa wa magonjwa ya ngozi, au hospital nzuri yenye uzoefu na tatizo la ngozi, ninaisha hapa Dar es salaam.

Kwa mawasiliano: sms 0715266772 au e-mail erasto@comsec.co.tz

Asante sana
Tatizo lenyewe likoje?, ni chunusi, ukurutu, madoa au ni nini? fafanua zaidi, unaweza ukawa una chunusi tu unataka uende mhimbili
 
Kwanza uko wapi, Dar au mikoani? Kama uko kanda ya kaskazini nenda KCMC, kama uko kanda ya pwani / mashariki nenda Muhimbili au nenda pale Amana hospital kuna specialist wa ngozi anafika pale weekly; kama uko kanda ya ziwa nenda Bugando. Kumbuka kuna gharama utatozwa au utatakiwa kulipia, jitayarishe. Wakati ukisubiri kumuona mtaalamu, zingatia usafi, badili nguo za juu mara mbili kutwa na za ndani kutwa mara tatu, soksi mara moja kutwa, fua nguo zako kwa jik, na wewe oga mara nne kwa siku kwa medicated soap!!! Zingatia, ni ushauri wa bure huo!!
 
Naulizia dawa ya ugonjwa wa ngozi. Kuna mtu ana alama alama nyeusi na nyeupe mgongoni hadi mabegani kama viduala fulani hivi. Ametumia dawa nyingi ila hakuna nafuu. Ametumia ile dawa ya mafuta, pia zile za fangas bila mafanikio. Please mwenye msaada zaidi.

Asanteni
 
hizo alama zikoje, ni kama ngozi iliyoungua,

if yes na kama yupo dar mwambie aende muhimbili, clinic ya ngozi atapata tiba,
 
Aende hospital akawaone wataalamu wa magonjwa ya ngozi. Atapata dawa zipo huko zitamponya.
 
naombeni msaada,kuna mdogo wangu amekuwa na tatizo la kutokewa vipele mwili mzima,vinavyo washa,nilimpeleka hospital moja wakampima mkojo,na vdrl hawakuona ki2(non reactive),wakamuandikia dawa za kumeza na za kupaka,lakini hamna unafuu wowote!nikampeleka pengine napo wakampima hawakuona tatizo,wakasema itakuwa ni aleji,wakampa dawa inaitwa predsoline vidonge vya kumeza kweli akawa amepona!lakini alipoacha 2 vikaanza tena! Sasa cha ajabu hata mke wake naye ameanza kuwashwa!na wiki jana walikwenda wote hospital wakapimwa mkojo,na damu hamna tatizo!sasa itakuwa nini? Je aleji huwa inaambukizwa!?naomba mwenye kumjua dematolojist mzuri anisaidie.
 
jaribu hindu mandar kama upo hapa dar kuna speacialist wa ngozi na ni dokta mzuri sana na kama upo moshi au arusha jaribu kcmc kuna dokta anaitwa dk for nae ni specialist wa ngozi, ngoja wngine nao wakupe maujanja
 
Hamna daktari Mzuri wa ngozi Tanzania kama unabisha waulize Wizara ya Afya wakati wanamuhangaikia Mwakyembe na walipokosa kabisa ikabidi wampeleke India.:rockon::rockon::rockon::rockon:
 
Hamna daktari Mzuri wa ngozi Tanzania kama unabisha waulize Wizara ya Afya wakati wanamuhangaikia Mwakyembe na walipokosa kabisa ikabidi wampeleke India.:rockon::rockon::rockon::rockon:

hujui tabia ya viongozi wetu?hata kama wanaumwa mafua wanataka kwenda kutibiwa nje
by the way issue ya mwakyembe ilikua so complicated, madokta wa ngozi wapo wazuri hata muhimbili,hindumandar,tmj na tumaini
 
jaribu hindu mandar kama upo hapa dar kuna speacialist wa ngozi na ni dokta mzuri sana na kama upo moshi au arusha jaribu kcmc kuna dokta anaitwa dk for nae ni specialist wa ngozi, ngoja wngine nao. wakupe maujanja
wapo dar mkuu,kesho nitawambia waende.thanx,ningekugongea like,ila na2mia simu
 
Back
Top Bottom