Ujio wa Wema Sepetu CHADEMA: Is She an Asset or a Liability? Mmeishaumwa na Nyoka, Hamjifunzi tu?!

kiukweli mpaka sasa chadema chini ya mbowe inazidi kudidimia sasa hivi kuna mambo mengi ambayo yeye akiwa mwenyekiti angeweza kuyasimamia na kuyapigania lakini badala yake anahangaika na watu kama wema.Kwakifupi wema ni mtaji wa magazeti ya udaku hasa ya shigongo ila kwenye siasa hamna kitu kabisa
 
Huwezi jua labda uwepo wake magamabni ndio ulipelekea awe na tabia zisizofurahisha, sasa upande aliokuja huwa wanasema ni kwa waliojitambua, bila shaka hapa anaweza kuwa mtu mpya! Maisha ni process.
 
Wanabodi,
Declaration of interest:
1.Mimi Paskali sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, sijawahi kuwa.
2.Mimi ni binadamu na mtu kutokea Kanda ya Ziwa, ambao wengi wetu tuna madhaifu na type fulani ya watu, hivyo naomba kukiri kuwa Wema ninampenda na kumkubali sana hata wife wangu anajua, hivyo maoni yangu kwenye bandiko hilo sio chuki binafsi na wala sio wivu kwa vile namzimikia Wema, na jinsi anavyotokelezea na Mbowe, wanapendezea, hivyo isije tafsiriwa namuonea wivu!.

Hili ni bandiko la swali kuhusu
Ujio wa Mrembo, Mnange na Mlimbwende Wema Sepetu Chadema: Is She An Asset or A Liability?. Haya mambo ya Chadema kuparamia warembo na walimbwende, na watu wenye majina makubwa, waliisha umwa na nyoka huko nyuma, hawajifunzi tuu? . Kiukweli I was surprised kumuona Wema seated next to Mwenyekiti Mbowe! or It just happened tuu hakuna aliye panga?!View attachment 474539 .
Screen-Shot-2017-02-25-at-5.11.40-PM.png

Mwigizaji Wema Sepetu, Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ni miongoni mwa waliojitokeza kuhudhuria mechi ya Simba vs Yanga kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam leo February 25 2017.

Screen-Shot-2017-02-25-at-5.09.02-PM.png

Mwigizaji Wema Sepetu na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe baada ya kushuka kwenye gari wakiwa wanaingia uwanjani.

Kwa Maoni Yangu...

Sasa kama Chadema ndio chama tegemewa na usajili wenyewe ndio kama huu wa Warembo, Wanyange, Walimbwende kama Wema, unategemea nini kwa 2020?!.

Kiukweli 2020 ni CCM tena na sio inashinda kwa sababu inapendwa sana, bali CCM inashinda kwa sababu Tanzania bado hatuna a credible opposition ya kuwa trusted na Ikulu yetu, unless watu wachoke mpaka basi na kuamua liwalo na liwe, hata kama ni kufanya majaribio ya kuijaribishia tuu Ikulu, bora tujaribishe tuu hivyo hivyo! .

Paskali.
Je mtu kuwa Asset anatakiwa asiwe "mrembo?, Mnyange?, Mlimbwende?" Sifa za mtu kuwa Asset kwenye Chama ni nini? Je walio Asset mbona hatuwaoni mkijitokeza kusaidia Taifa lisonge kutoka hatua moja hadi nyingine? CCM waliona nini kwa Wema hata wakamtumia kupiga kampeni na kuambatana na mtu mkubwa kiasi hicho Makamu wa Rais? Kama hakuwa Asset kwa nini walimtumia? Na kama maswali haya ni kweli yasiyo na wivu je ulihoji hivi CCM walipomtumia Wema kuwapigia kampeni? CCM walimtumia Wema wakapewa kuiongoza nchi, leo inakuwaje asiwe Asset anapohamia Chedema? Kama mtoa post ulishindwa kuhoji Uasset wa Wema kipindi akifanya kampeni na Makamu wa Rais leo umeipateje hofu ya Uasset wa mtu aliyekutengenezea Rais? .
 
Mayalla maana yake ni NJAA

Na wewe njaa zako zitakuwa zimehama kutoka tumboni kwend kwenye UBONGO! No wonder you're arguing like brainless myopic kid
 
Mtu mwerevu ubadili liability to asset. SAsa wewe nguvu yangu kama ni liability atabadilishwa Dawa kwenye sasa zakubadilisha watu Zippo.
 
Wanabodi,
Declaration of interest:
1.Mimi Paskali sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, sijawahi kuwa.
2.Mimi ni binadamu na mtu kutokea Kanda ya Ziwa, ambao wengi wetu tuna madhaifu na type fulani ya watu, hivyo naomba kukiri kuwa Wema ninampenda na kumkubali sana hata wife wangu anajua, hivyo maoni yangu kwenye bandiko hilo sio chuki binafsi na wala sio wivu kwa vile namzimikia Wema, na jinsi anavyotokelezea na Mbowe, wanapendezea, hivyo isije tafsiriwa namuonea wivu!.

Bandugu kuchua like kubwa hapo juu :):):):):):):):):)
 
Nasikia ana followers "wengi sana" huko Instagram. In that view, conclude if she is an asset or not.
Mkuu comment yako ime summarize hiyo endless article aliyokuja nayo Pascal.

Unajua hawa ccm wanamchukulia poa Wema sepetu wanaona kama hana impact yoyote ya kisiasa hapa nchini kwa huu ujio wake wa kuja chama kikuu pinzani.

Wanafikiri labda Wema ni kama Jacqueelin Wolper au Masogange au Shamsa Ford celebrities ambao ni less relevant kwenye macho ya wanajamii.

Hawajui kwamba kwenye swala la umaarufu na kupendeka kwa watu wengi Wema ni mtu mwingine kabisa ukilinganisha na hao wenzake.

Wema sepetu anaweza kuwa ni mtu wa ovyo na kwa mtu yoyote smart hawezi kuwa na time ya kumfollow. Ila kwa idadi ya wafuasi alionao ambao wengi ni akina dada tena wapiga kura, tayari hiyo moja moja inaonyesha yeye ni asset.

Na watakuja kujionea huyu dada ushawishi wake una nguvu miaka mitatu ijayo kwanzia sasa. Kwani kuna mwana ccm alitegemeaga Lowassa atawaenyesha vile?

Viongozi wa upinzani wana jua sana kucheza na mind control.
 
Hili ni bandiko la swali kuhusu
Ujio wa Mrembo, Mnange na Mlimbwende Wema Sepetu Chadema: Is She An Asset or A Liability?. Haya mambo ya Chadema kuparamia warembo na walimbwende, na watu wenye majina makubwa, waliisha umwa na nyoka huko nyuma, hawajifunzi tuu? . Kiukweli I was surprised kumuona Wema seated next to Mwenyekiti Mbowe! or It just happened tuu hakuna aliye panga?!

Nadhani ukiangalia kulia kwa Wema utapata jibu! Kama unavyoshangaa yawezekana Chairman naye kajikuta centre ya hayo na kama Binadamu imeshakuwa basi hainaga jinsi na ukizingatia kazi kubwa ya Demokrasia ni uhuru wa mtu mmoja mmoja.
Usi hofu yaliyopita siyo ndwele:):)
 
jibu rahisi.

mwalimu wangu wa siasa darasa la tano aliwahi nifundisha kuwa

1. mtaji wa chama cha siasa ni wanachama..... sina uhakika kama wema ni mwanachama wa Chadema au la

2. kwamba ili chama kiweze kuongoza dola ni lazima kipate uungwaji mkono na wananchi....sina uhakika kama kujiunga kwa wema kule Chadema ni kuibomoa Chadema

3. pia sina uhakika kwanini ilibidi Steve Nyerere kulalamika kwenye press na wewe Paskal imebidi kuja kulalamika hapa JF!

sisi tuendelee na kazi zetu
 
Wanabodi,
Declaration of interest:
1.Mimi Paskali sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, sijawahi kuwa.

Paskali.
mkuu Paskali. am not being petty lakini nime-smell ka-contradiction fulani kwenye bandiko lako. is it something deep in your subconscious that pops out involuntarily to reveal where exactly your heart is? kwamba japo unataka kuiaminisha dunia kuwa hauko Chadema lakini in actual fact wewe ni Chadema kindakindaki ila hutaki kuji-reveal mkuu?

kwenye title ya thread umetumia sentenso "Ujio wa Wema Sepetu Chadema....". lakini ah - wait a minute - umekuja kuandika "Mimi Paskali sio mwanachama wa chama chochote cha siasa....".

ujio ni noun ya verb "kuja" - yaani kitu kingine au mtu mwingine kuelekea kule uliko wewe mtumiaji wa neno "ujio" wakati huo.

mkuu, tufafanulie ili tukwangue huu ukakasi......
 
Great thinker, M-babe
 
Back
Top Bottom