Ujio wa Wema Sepetu CHADEMA: Is She an Asset or a Liability? Mmeishaumwa na Nyoka, Hamjifunzi tu?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,450
Wanabodi,
Declaration of interest:
1.Mimi Paskali sio mwanachama wa Chadema ila ni kada wa chama cha siasa.
2.Mimi ni binadamu na mtu kutokea Kanda ya Ziwa, ambao wengi wetu tuna madhaifu na type fulani ya watu, hivyo naomba kukiri kuwa Wema ninampenda na kumkubali sana hata wife wangu hilo alinajua, hivyo maoni yangu kwenye bandiko hilo sio chuki binafsi na wala sio wivu kwa vile namzimikia Wema, au naona wivu wa jinsi anavyotokelezea na Mbowe, na jinsi wanapendezea kwa ukaribu huo, hivyo isije tafsiriwa namuonea wivu!.

Hili ni bandiko la swali kuhusu
Ujio wa Mrembo, Mnange na Mlimbwende Wema Sepetu Chadema: Is She An Asset or A Liability?. Haya mambo ya Chadema kuparamia warembo na walimbwende, na watu wenye majina makubwa, waliisha umwa na nyoka huko nyuma, lakini hawakomi na wala hawajifunzi tuu? . Kiukweli I was surprised kumuona Wema seated next to Mwenyekiti Mbowe! or It just happened tuu hakuna aliye panga?!
hqdefault.jpg
.
Screen-Shot-2017-02-25-at-5.11.40-PM.png

Mwigizaji Wema Sepetu, Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ni miongoni mwa waliojitokeza kuhudhuria mechi ya Simba vs Yanga kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam leo February 25 2017.

Screen-Shot-2017-02-25-at-5.09.02-PM.png

Mwigizaji Wema Sepetu na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe baada ya kushuka kwenye gari wakiwa wanaingia uwanjani.

Kwa Maoni Yangu...

Nimeona baadhi ya viongozi, wanachama na washabiki wa Chadema, wakifurahia ujio wa mlimbwende Wema Sepetu kujiunga Chadema as if Chadema wamelamba dume, kiukweli Chadema wamelamba garasa, an empty shell kwa sababu mrembo huyu hanaga msimamo hata mara moja, kuanzia kwenye choice of friends na love life yake, has never been stable and settled, hivyo kujiunga kwake Chadema ni hasira tuu za kutuhumiwa bila CCM kuonyesha kumsaidia, hivyo anahama CCM, ili kuwakomoa na kujiunga Chadema ili tuu kuwaringishia CCM, but she has no value at all to add to Chadema, kwa sababu hasira zitaisha, na atarejea CCM!, just time will tell!.

Haki ya Wema Kujiunga Chama Chochote, ila The Timing ni Wrong Timing.
Wema Sepetu, kama Mtanzania mwingine yeyote, anayo haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa kwa sababu zozote, au bila sababu zozote kwa mapenzi yake, sambamba na haki ya kujitoa chama chochote kwa sababu yoyote au bila sababu yoyote, ila timing ya kujitoa chama fulani, na timing ya kujiunga chama fulani ni muhimu sana, kwa maoni yangu, hii timing aliyoitumia kujitoa CCM na kujiunga Chadema, is a wrong timing!, hata kama aliipenda Chadema siku nyingi tuu na alipanga kujiunga nayo, kujitoa CCM baada ya kulazwa selo wiki moja, kunatafsiriwa ni amejitoa kwa hasira baada ya kutetea CCM na kutesekea, malipo yake ndio haya, hivyo kwa hasira ameamua kujitoa, na kujiunga Chadema ili kuwakomoa CCM na kuwaringishia. It is a wrong timing, kwa sababu, Wema bado ana kesi mahakamani, usishindane na mwenye nguvu!, ungejua Godbless Lema hana kosa lolote zaidi ya kuisema tuu ndoto aliooteshwa, lakini kwa vile alipishana na Gambo, akamtunishia msuli, saa hizi yuko wapi?. Msije shangaa mtoto wa watu akafutiwa dhamana, au akazushiwa chochote na kupigwa mvua, Chadema haiwezi kumsaidia lolote!. Angesubiri yaishe kwa amani, kisha akajitimkia zake kwa uhakika, haya mambo, hayahitaji hasira.

Haki ya Chadema Kupokea Mwanachama Yoyote, Tatizo ni Umuhimu/Ukaribu Mkubwa
Mchungaji Mwema huwaacha kondoo wake 99 akaenda kumtafuta kondoo mmoja aliyepotea, na hata mbiguni, huwa ni furaha mwenye dhambi mmoja akitubu, vivyo hivyo Chadema kina haki ya kufurahi kila kinapovuna mwanachama mmoja, nikimaanisha CCM inazidi kubomoka na kukimbiwa, na Chadema inazidi kujengeka kwa kuongeza. Pia Chadema kama chama cha siasa, kina haki ya kumpokea mwanachama yoyote kutoka popote, tatizo langu ni attention kubwa aliyopewa Wema, siku ya kwanza juzi pale Mahakama ya Kisutu, Wema ndio akae next to Mwenyekiti?!, hata Mdee, Bulaya na viongozi wengine walipunguzwa umuhimu, baada ya Mwenyekiti, Wema!. Leo mpirani kwenye mechi ya Simba na Yanga, Wema ametinga gari moja na Mwenyekiti!. Kweli Wema ni Super Star, ila kichama ni mwanachama tuu wa kawaida kama mwanachama mwingine yoyote, asionekane anapapatikiwa sana, ananyenyekewa sana, mtu kajiunga na Chadema jana tuu, leo anashuka gari moja na Mwenyekiti!, its too much of a VIP treatment, kesho atawaaibisha atakaporejea nyumbani CCM!.

Wema ni Asset or Liability? .
Wema ni mtaji, kibiashara tunaita ni asset kwa sababu hakuna ubishi kuwa Wema ni super star, Wema ni maarufu, Wema ana followers zaidi ya milioni 2 ambao kama kweli hawa wote watamfuata Wema Chadema, then Chadema itakuwa imepata mtaji mkubwa.

Wema Ni Faida Kidogo na Hasara Kubwa Hivyo ni Liability.
Pamoja na ukweli kuwa Wema ni asset, sio fixed asset, hii ni movable asset, current asset na liquid asset ambayo mtaji unahamishika, unaotumika na kuweza kuyeyuka wakati wowote.

Kwa Nini Wema ni A Liability?.
Mfano wa Gari Bovu.

Gari likiwa jipya linakuwa na thamani kubwa katokana na upya wake hivyo unaweza kulifanyia biashara likakuingizia faida hivyo utaliita mtaji. Lakini gari likiwa limechakaa na kuanza kuchoka, ukilinunua linaweza kukuingizia faida kidogo lakini running costs na maintainance cost zikawa kubwa na kumeza faida yote, hivyo kujikuta unafanya biashara ya hasara au biashara kichaa.
Ni Biashara Kichaa
Wema ndani ya Chadema ni biashara kichaa. Whoever aliyetoa fungu kumnunua Wema akijua amewekeza kwenye biashara ya faida, kiukweli kwa sasa Wema ni biashara kichaa.

Wema ni Jina Tuu, Muuza Sura, au Muuza...?!, Je Chadema ina Wanunuzi?!.
Hii ni kufuatia Wema Sepetu amebaki jina tuu na kuuza sura, au kuuza..., kwa sababu kwa sasa, Wema hana shughuli nyingine yoyote ya maana anayoifanya inayomuingizia kipato cha kuendesha maisha yake zaidi ya kuuza sura na zile huduma zetu zile!, Jee Chadema inao wanunuzi wa huduma hizo kwa kwa dau la Wema?.

Kwa sasa Wema hana movie, haimbi, hana ofisi, na hana mtu, hivyo alijiunga CCM akitegemea kukwaa viti maalum kama walibwende wenzake, Vicky, Juliana, Lucy, Catherine na wengine ila CCM walingundua siku nyingi kuwa upstairs yuko totally empty wakamtosa! ,hata hivyo aliendelea kuikumbatia CCM kwa ajili tuu ya kuvuta fungu nene in an exchange ya zile "huduma" kwa baadhi ya watu, haswa kwa uzuri ule, urembo ule na weupe ule, ambao ni ugonjwa wa watu wa kanda fulani akitegemea "yule jamaa mwenyewe" ndie angefika bei!,lakini "wale jamaa" walikuwa makini maana kila apitaye kwa Wema ni matangazo, hivyo jamaa akipita na matangazo yangefuatia ingekuwaje?!. (kama kumezea mate, kiukweli msema kweli mpenzi wa Mungu, hata mimi!, hebu jifikirie hata ungekuwa wewe?), hivyo akadondokea kwa yule Msukuma mwenye kisu kikali akamtuliza kipindi chote cha kampeni. Baada ya ushindi kazi yake ikaisha akatemwa!.

Thamani ya Wema ni Nini na Lini? .
Thamani ya Wema ni mtaji wa followers milioni 2 kwenye team Wema. Jee mtaji huu unafaida gani wakati wa kipindi hiki?. Kwa maoni yangu, thamani ya Wema ni kwenye uchaguzi tuu, kwa vile uchaguzi wa 2020 bado ni mbali, maintainance cost kumeintain Wema mpaka kipindi hicho zitakuwa too much kwa Chadema ku afford, ni CCM pekee ndio wenye fedha za mchezo unless wanaChadema individually wenye kisu kikali kama Mbowe, au 'Mzee Wetu' waamue kumshika mkono chini ya himaya zao, kwa mujibu wa zilepicha zile za mahakamani, kiukweli walipendezea, ila...tatizo waliopo watakubali?!.

Nini Kitatokea Kwa Wema Chadema? .
Kusipotokea sponsor wa kugharimia maitainence ya Wema, then kitakacho fuata ni kile kile kilichotokea kwa Nakaaya Sumari, Jackline Wolper, Anti Ezekiel na wengine wanaojiunga na vyama vya siasa sio kwa mapenzi ya vyama hivyo bali as a means ya kuendeshea maisha yao, wakigundua tuu kuwa Chadema ni juani, na CCM ndio kivulini, soon wataungua na jua kali na kujirudia zao kivulini.
Hivyo naomba sana wana Chadema, msije kushangaa soon ikaitishwa press conference nyingine Wema akaomba msamaha na kudai ni hasira tuu za kulazwa selo, hivyo ni shetani tuu alimpitia na kuhama CCM, hivyo ataomba asamehewe na atapokelewa na Ngosha mwenyewe kurejea CCM! .
Sasa kama Chadema ndio chama tegemewa na usajili wenyewe ndio kama huu wa Warembo, Wanyange, Walimbwende wasio na msimamo kama Wema, unategemea nini kwa 2020?!.

Kiukweli 2020 ni CCM tena na sio inashinda kwa sababu inapendwa sana, bali CCM inashinda kwa sababu Tanzania bado hatuna any credible serious opposition ya kuwa trusted na Ikulu yetu, unless watu wachoke mpaka basi na kuamua liwalo na liwe, hata kama ni kufanya majaribio ya kuijaribishia tuu Ikulu, bora tujaribishe tuu hivyo hivyo! .

Paskali.
 
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali kuhusu
Ujio wa Mrembo, Mnange na Mlimbwende Wema Sepetu Chadema: Is She An Asset or A Liability?. Haya mambo ya Chadema kuparamia warembo na walimbwende, na watu wenye majina makubwa, waliisha umwa na nyoka huko nyuma, hawajifunzi tuu? . Kiukweli I was surprised kumuona Wema seated next to Mwenyekiti Mbowe! or It just happened tuu hakuna aliye panga?!View attachment 474539 .

Kwa Maoni Yangu.
Nimeona baadhi ya viongozi, wanachama na washabiki wa Chadema, wakifurahia ujio wa mlimbwende Wema Sepetu kujiunga Chadema as if Chadema wamelamba dume, kiukweli Chadema wamelamba garasa, an empty shell.

Wema ni Asset or Liability? .
Wema ni mtaji, kibiashara tunaita ni asset kwa sababu hakuna ubishi kuwa Wema ni super star, Wema ni maarufu, Wema ana followers zaidi ya milioni 2 ambao kama kweli hawa wote watamfuata Wema Chadema, then Chadema itakuwa imepata mtaji mkubwa.

Wema Ni Liability-Hasara Tupu!.
Pamoja na ukweli kuwa Wema ni asset, sio fixed asset, bali movable asset, current asset na liquid asset ambayo mtaji unahamishika, unaotumika na kuweza kuyeyuka wakati wowote.

Kwa Nini Wema ni A Liability?.
Mfano wa Gari Bovu.
Gari likiwa jipya linakuwa na thamani kubwa katokana na upya wake hivyo unaweza kulifanyia biashara likakuingizia faida hivyo utaliita mtaji. Lakini gari likiwa limechakaa na kuanza kuchoka, ukilinunua linaweza kukuingizia faida kidogo lakini running costs na maintainance cost zikawa kubwa na kumeza faida yote, hivyo kujikuta unafanya biashara kichaa.
Biashara Kichaa
Wema ndani ya Chadema ni biashara kichaa. Whoever aliyetoa fungu kumnunua Wema akijua amewekeza kwenye biashara ya faida, kiukweli kwa sasa Wema ni biashara kichaa.

Wema ni Jina Tuu, Muuza Sura, au Muuza..., Chadema ina Wanunuzi?!.
Hii ni kufuatia Wema Sepetu amebaki jina tuu na kuuza sura, au kuuza..., kwa sababu Wema hana shughuli yoyote ya maana inayomuingizia kipato, hivyo alijiunga CCM akitegemea kukwaa viti maalum kama walibwende wenzake, Vicky, Juliana, Lucy, Catherine na wengine ila CCM walingundua siku nyingi kuwa upstairs yuko totally empty wakamtosa! ,hata hivyo aliendelea kuikumbatia CCM kwa ajili tuu ya kuvuta fungu nene in an exchange ya zile "huduma" kwa baadhi ya watu, haswa kwa uzuri ule, urembo ule na weupe ule, ambao ni ugonjwa wa watu wa kanda fulani akitegemea "yule jamaa mwenyewe" ndie angefika bei,
lakini "wale jamaa" walikuwa makini maana kila apitaye ni matangazo, hivyo akadondokea kwa yule Msukuma mwenye kisu kikali akamtuliza kipindi chote cha kampeni. Baada ya ushindi kazi yake ikaisha.

Thamani ya Wema ni Nini na Lini? .
Thamani ya Wema ni mtaji wa followers milioni 2 kwenye team Wema. Jee mtaji huu unafaida gani wakati wa kipindi hiki?. Kwa maoni yangu, thamani ya Wema ni kwenye uchaguzi tuu, kwa vile uchaguzi was 2020 bado ni mbali, maintainance cost kumeintain Wema mpaka kipindi hicho zitakuwa too much, ni CCM pekee ndio wenye fedha za mchezo unless wanaChadema individually wenye kisu kikali kama Mbowe, au 'Mzee Wetu' waamue kumshika mkono chini ya himaya zao, kwa mujibu wa zilevpicha zile za mahakamani, kiukweli walipendezea, ila...tatizo waliopo watakubali?!.

Nini Kitatokea Kwa Wema Chadema? .
Kusipotokea sponsor wa kugharimia maitainence ya Wema, then kitakacho fuata ni kile kile kilichotokea kwa Nakaaya Sumari, Jackline Wolper, Anti Ezekiel na wengine wanaojiunga na vyama vya siasa sio kwa mapenzi ya vyama hivyo bali as a means ya kuendeshea maisha yao, wakigundua tuu kuwa Chadema ni juani, na CCM ndio kivulini, soon wataungua na jua na kujirudia zao kivulini.
Hivyo naomba sana msije kushangaa soon ikaitishwa press conference nyingine Wema akaomba msamaha na kudai ni hasira tuu za kulazwa selo, hivyo ni shetani tuu alimpitia na kuhama CCM, hivyo ataomba asamehewe na atapokelewa na Ngosha mwenyewe! .

Sasa kama Chadema ndio chama tegemewa na usajili wenyewe ndio kama huu wa Wema, unategemea nini?!.

Kiukweli 2020 ni CCM tena na sio inashinda kwa sababu inapendwa sana, bali CCM inashinda kwa sababu Tanzania bado hatuna a credible opposition ya kuwa trusted na Ikulu yetu, unless watu wachoke mpaka basi na kuamua liwalo na liwe, hata kama ni kufanya majaribio ya kuijaribishia tuu Ikulu, bora tujaribishe tuu hivyo hivyo! .

Paskali.
Let's the talk
 
Mimi jamani sina chama kabissaaa!ila nimejiuliza sipati jibu isingekuwa kukamatwa na mabangi kulazwa sero asingeenda chadema au.mimi binafsi nilikuwa nampenda ila tabia zake tu naona ni mtu wa kurukupa.baada ya yote yaliyomtokea ningekuwa Mimi ningetulia nimalizane na kesi then nijuwe what next...anyways maisha ni yake
 
Kiukweli 2020 ni CCM tena na sio inashinda kwa sababu inapendwa sana, bali CCM inashinda kwa sababu Tanzania bado hatuna a credible opposition ya kuwa trusted na Ikulu yetu
Hapa tu ndio nimekukubali sana.....Na hili la kuwa na UPINZANI BUTU ndio linaloturudisha nyuma sana kimaendeleo...
Tunakuwa na chama cha upinzani ambacho kimeshindwa kuwa na mawazo mbadala wa kupambana na serikali ya CCM.....
 
Watanzania wengi wamerogwa na CCM na akili Yao wengi si wasomi na wasiosoma wote ccm wamewaroga akili ,hatuna uthubutu ni watu wanaoishi tu kwa hofu,kutisha watu,

Kenya ukiangalia kwa mfano viongozi wote hao walikuwa Kanu lakini baada ya chama cha Kanu kutolewa viongozi wako mchanganyiko kwenye vyama tofauti,wengine wako ODM, Jubilee, CORD nk,nyie hapa kupitia CCM kuwaroga akili mnakuja kusema wapinzani watoe watu wapi kuja kupata wanachama.leo ccm inashinda chaguzi kwasabbu ina majinga wengi na ndio wapiga kura wengi.

Wewe unashauri CHADEMA wao wachuje watu, wakati ushindi wa chaguzi ni wingi wa kura, wingi kura inatokana na wingi wa wanachama,sasa hao wasafi ni asilimia ngapi kushinda wajinga wengi,tunaangalia sera za chama na sio akina nani wapo kwenye chama.

Msitishe watu wanazi wa ccm watu kujiunga kwenye vyama mbalimbali wacheni wawe free, wanazi wa CCM tunawajua kwa kijicho na hofu zenu za kupaka upinzani matope
 
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali kuhusu
Ujio wa Mrembo, Mnange na Mlimbwende Wema Sepetu Chadema: Is She An Asset or A Liability?. Haya mambo ya Chadema kuparamia warembo na walimbwende, na watu wenye majina makubwa, waliisha umwa na nyoka huko nyuma, hawajifunzi tuu? . Kiukweli I was surprised kumuona Wema seated next to Mwenyekiti Mbowe! or It just happened tuu hakuna aliye panga?!View attachment 474539 .

Kwa Maoni Yangu.
Nimeona baadhi ya viongozi, wanachama na washabiki wa Chadema, wakifurahia ujio wa mlimbwende Wema Sepetu kujiunga Chadema as if Chadema wamelamba dume, kiukweli Chadema wamelamba garasa, an empty shell.

Wema ni Asset or Liability? .
Wema ni mtaji, kibiashara tunaita ni asset kwa sababu hakuna ubishi kuwa Wema ni super star, Wema ni maarufu, Wema ana followers zaidi ya milioni 2 ambao kama kweli hawa wote watamfuata Wema Chadema, then Chadema itakuwa imepata mtaji mkubwa.

Wema Ni Liability-Hasara Tupu!.
Pamoja na ukweli kuwa Wema ni asset, sio fixed asset, bali movable asset, current asset na liquid asset ambayo mtaji unahamishika, unaotumika na kuweza kuyeyuka wakati wowote.

Kwa Nini Wema ni A Liability?.
Mfano wa Gari Bovu.
Gari likiwa jipya linakuwa na thamani kubwa katokana na upya wake hivyo unaweza kulifanyia biashara likakuingizia faida hivyo utaliita mtaji. Lakini gari likiwa limechakaa na kuanza kuchoka, ukilinunua linaweza kukuingizia faida kidogo lakini running costs na maintainance cost zikawa kubwa na kumeza faida yote, hivyo kujikuta unafanya biashara kichaa.
Biashara Kichaa
Wema ndani ya Chadema ni biashara kichaa. Whoever aliyetoa fungu kumnunua Wema akijua amewekeza kwenye biashara ya faida, kiukweli kwa sasa Wema ni biashara kichaa.

Wema ni Jina Tuu, Muuza Sura, au Muuza..., Chadema ina Wanunuzi?!.
Hii ni kufuatia Wema Sepetu amebaki jina tuu na kuuza sura, au kuuza..., kwa sababu Wema hana shughuli yoyote ya maana inayomuingizia kipato, hivyo alijiunga CCM akitegemea kukwaa viti maalum kama walibwende wenzake, Vicky, Juliana, Lucy, Catherine na wengine ila CCM walingundua siku nyingi kuwa upstairs yuko totally empty wakamtosa! ,hata hivyo aliendelea kuikumbatia CCM kwa ajili tuu ya kuvuta fungu nene in an exchange ya zile "huduma" kwa baadhi ya watu, haswa kwa uzuri ule, urembo ule na weupe ule, ambao ni ugonjwa wa watu wa kanda fulani akitegemea "yule jamaa mwenyewe" ndie angefika bei,
lakini "wale jamaa" walikuwa makini maana kila apitaye ni matangazo, hivyo akadondokea kwa yule Msukuma mwenye kisu kikali akamtuliza kipindi chote cha kampeni. Baada ya ushindi kazi yake ikaisha.

Thamani ya Wema ni Nini na Lini? .
Thamani ya Wema ni mtaji wa followers milioni 2 kwenye team Wema. Jee mtaji huu unafaida gani wakati wa kipindi hiki?. Kwa maoni yangu, thamani ya Wema ni kwenye uchaguzi tuu, kwa vile uchaguzi was 2020 bado ni mbali, maintainance cost kumeintain Wema mpaka kipindi hicho zitakuwa too much, ni CCM pekee ndio wenye fedha za mchezo unless wanaChadema individually wenye kisu kikali kama Mbowe, au 'Mzee Wetu' waamue kumshika mkono chini ya himaya zao, kwa mujibu wa zilevpicha zile za mahakamani, kiukweli walipendezea, ila...tatizo waliopo watakubali?!.

Nini Kitatokea Kwa Wema Chadema? .
Kusipotokea sponsor wa kugharimia maitainence ya Wema, then kitakacho fuata ni kile kile kilichotokea kwa Nakaaya Sumari, Jackline Wolper, Anti Ezekiel na wengine wanaojiunga na vyama vya siasa sio kwa mapenzi ya vyama hivyo bali as a means ya kuendeshea maisha yao, wakigundua tuu kuwa Chadema ni juani, na CCM ndio kivulini, soon wataungua na jua na kujirudia zao kivulini.
Hivyo naomba sana msije kushangaa soon ikaitishwa press conference nyingine Wema akaomba msamaha na kudai ni hasira tuu za kulazwa selo, hivyo ni shetani tuu alimpitia na kuhama CCM, hivyo ataomba asamehewe na atapokelewa na Ngosha mwenyewe! .

Sasa kama Chadema ndio chama tegemewa na usajili wenyewe ndio kama huu wa Wema, unategemea nini?!.

Kiukweli 2020 ni CCM tena na sio inashinda kwa sababu inapendwa sana, bali CCM inashinda kwa sababu Tanzania bado hatuna a credible opposition ya kuwa trusted na Ikulu yetu, unless watu wachoke mpaka basi na kuamua liwalo na liwe, hata kama ni kufanya majaribio ya kuijaribishia tuu Ikulu, bora tujaribishe tuu hivyo hivyo! .

Paskali.
Nilikuwa nakuheshimu kumbe nawe sometimes empty ? Hv
 
Mimi kila siku nasema wapinzani hawajui siasa bali wanajua harakati tu

Siasa ni Sayansi tena ni zaidi ya Nuclear science au Rocket science lakini ndiyo sanyasi pekee ambayo kwa Africa watu wa kujua mikakati na mipango wanaiweza vizuri kuliko watu wanaotumia akili nying ktk kupanga mambo
Sayansi ambayo naweza sema imewashinda vyama vya upinzani , wakati CCM wakiitumia vizuri sayansi hiyo vyama vya upinzani vinaangaika badala ya kufanya siasa vinajikuta vinafanya harakati si siasa tena, kwani wameshindwa kufungua pandora box la siasa
CCM ndio chama pekee ndani ya Africa ninachoongozwa na mfumo (system) ambayo kila mwanaccm ni lazima aifate kwani siku zote mfumo ndio unafatwa na watu so mfumo unawalazimisha wanaccm waufate leo mfumo wa CCM autegemei mtu au akili za watu ila watu ndo wanaoutegemea mfumo wa ccm hii imekuwa ni tofauti na vyama vya upinzani bado vinategemea akili na utashi wa mtu kukiongoza chama na wanachama
Mfumo wa CCM ambao umekuwa installed 5 February 1977 mfumo(System) ambayo ni kama treni , (Reli) ndio mfumo wenyewe (Treni) ndio CCM (dereva) ndio mwenyekiti wa ccm (wahudumu wa treni) ndio viongozi wa ccm( abiria) ndio wapenzi na wanachama wa ccm je unadhani baadhi ya wahudumu au abiria wakishuka treni itashindwa kwenda?

Siku zote treni ndio inafata (Reli)si reli ndio inafata treni na kazi ya (Dereva) ni kuhakikisha treni inafata reli so dereva yeyote anaweza kupewa treni na kuindesha kwani siku zote hakuna dereva bingwa wa kuendesha treni na ndio maana kwenye kuendesha treni huwezi kufanya( drift)

Siku wapinzani wakiweza kufungua Pandora box la siasa wanaweza kuchukua nchi hii bila hata ya kuwachukua watu wa CCM au Viongozi wa CCM we niambie ni kiongozi gani wa upinzani alikwenda CCM na wakampa VIP treatment au kumchukulia kama mtaji wao kisiasa zaidi ya upinzani kuwapa VIP treatment wanaotoka CCM kuja Upinzani?

Upinzani wanatakiwa kuwa kama iphone yani hawatoi choice ya mnunuzi nje ya mfumo wa android kwa sababu nje ya mfumo wa adroid ni IOS na ukizungumzia IOS unakwenda moja kwa moja kwa iphone tu lakini ukizugumzia android unakwenda kwenye brand zaidi ya kumi (Samsung, Sony , Lenovo, Tecno, Motorola ,Huawei na kuendelea )

Kwenye Project yeyote kuna kitu kinaitwa project cost Wema hana faida yeyote hasa muda huu ambao bado miaka 3 ndio unafanyika uchaguzi kitu kingine bwana
Pascal Mayalla mashabiki milion 2 kwenye insta je tuna hakika gani kama wote ni watanzania na niwapiga kura na wote wana vigezo vya kupiga kura pia je si ghost followers ? na je wote watamfata Chadema?
 
Kuna vitu ambavyo nashangaa sana katika siasa zetu. Mtu kuhamia chama kingine inaonekana jambo la ajabu mpaka kuanza kupima nguvu yake.

Kwanini tuwaze Wema ni liability au asset wakati Mwajuma wa pale morogoro anaweza jiunga na chadema na tusiangalie yote hayo?

Kura yake moja kwa chadema inatosha. Ninapo ona Mwandishi kama ww unakuja na hoja za hovyo humu ninakuwa sina utetezi kwa ile kauli ya Mkapa kuhusu Waandishi wa Kibongo.

Trump alikuwa Republican akahamia Democratic akahama akawa Independent na Mwishoe akarudi Republican na akashinda Urais. Lkn kwa wenzetu hukusikia hata siku moja hii ikawa hoja katika uchaguzi wa mwaka jana, kwan wao wanaona ni jambo la kawaida mtu kuhama chama kutokana na itikadi ya chama. Na mtu hubadilika kimawazo kila siku, leo anaweza ona itikadi hii inamfaa lkn kesho mawazo yakabadilika.

Wema kuhamia Chadema au Mpendazoe kurudi CCM ni jambo la kawaida ktk demokrasia iliyo komaa.

Naomba uje na hoja za msingi, waandishi wa habari wa kibongo tunajikita katika umbea wa vijiweni na kufanya kuwa habari.
 
Back
Top Bottom