Ujio wa Lissu na siri katika namba

4IR

JF-Expert Member
Apr 21, 2014
995
1,000
Kumekuwepo na nadharia (conspiracy theories) kuhusu namba kwenye Muda (Mwezi, Siku na Saa) kubeba siri nyingi za matukio mbalimbali yanayotokea dunia. Matukio yanaweza kuwa ni vifo nk.

Je, ni kweli kuna siri katika namba au fikra zetu tu katika kujenga taswira kuhusu matukio? Lissu alishambuliwa Trh 7/9/2017 mchana, na amerejea nchini Trh 27/7/2020 saa 7 mchana. Nimetafakari uwepo wa namba 7 katika matukio, kuna siri ktk hili?

Wataalamu wa haya mambo karibuni kwenye mjadala.
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
8,784
2,000
Kuna makubwa sana kuhusu Lissu, kwanza namba 7 ambayo ni ishara ya ukamilifu, ni namba iliyotumika sana kwenye Biblia ikiwakilisha ukamilifu au Umungu. Hivyo yaweza kumaanisha mpango wa Mungu katika yale Lissu anapitia au kuwakilisha. Hatujui kikamilifu ni nini hasa.

Pili namna alivyopokelewa, hakuna aliyetarajia, manake hata wakuu na majeshi yamejikuta yameduwaa tuu, mimi mwenyewe sikuamini, hili nalo ni ishara ya mtu asiyeshikika.

Tatu kushambuliwa kwake kwa risasi zaidi ya 16 katika mwili wake na leo anatembea tena bila msaada au magongo ni ishara ya ajabu ya umungu katika mtu huyu.

Nne tukio zima la kurudi kwake, yaani Lissu anarudi nchini anapokelewa kifalme na Mkapa (mfalme) anazikwa. Hapa ndipo zilipo siri zote na hai hitaji kusema zaidi nadhani inaeleweka nini fumbo hilo linamaanisha.
KINYOMI CHA LISSU,NI KITONE KWENYE NYOMI LA LOWASSA 2015.

Leo 20:15pm 27/07/2020

Najaribu tu kutafakari nani atavaa viatu vya Mzee Lowassa wa 2015.

Leo nimeona Mapokezi ya Lissu, na wafuasi wake wakirusha picha za Lowassa za 2015.

Bora ya Membe kasema yeye atakuwa mnogeshaji.

Aliyekuja leo kapokewa na wajumbe na roho za wajumbe mnazijua.

Tupo kwenye Maombolezo ya Hayati Benjamin Mkapa, ila kila nikikumbuka ile nyomi ya Lowassa pale jangwani 2015 hakuna cha Lissu wala cha Membe atakaye lipiku nyomi lile.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga.
Nawasifu sana CHADEMA . Walitii sheria bila shuruti. CHADEMA walionywa kuwa; Asifike mtu pale uwanja wa ndege kumpokea mgeni wao. Wale uliowaona ni malofa tu waliokuwa wanatamani kuchakazwa.

Makada wa CHADEMA wapo nyumbani kwao wanangojea October 28 na vichinjio vya wameandaa. Ulitaka waende ili muwanyang'anye vichinjia huku mkiwaacha wamechakazwa? Limebuma hilo tego lenu.
Za Lowassa zilikuwa kampeni, ya Lissu ni mapokezi. Hebu ngoja tuone itakavyokuwa wakati wa kampeni. Lakini, wakati mwingine ni heri kuwa na watu wachache wapigakura wako kuliko maelfu wanaokuja kukushangaa na kucheza mziki tu
Mnavyopeana matumaini sasa. Poor nyalandu sijui akipitishwa atasindikizwa na nyomi gani
Kumekuwepo na nadharia (conspiracy theories) kuhusu namba kwenye Muda (Mwezi, Siku na Saa) kubeba siri nyingi za matukio mbalimbali yanayotokea dunia. Matukio yanaweza kuwa ni vifo nk.

Je, ni kweli kuna siri katika namba au fikra zetu tu katika kujenga taswira kuhusu matukio? Lissu alishambuliwa Trh 7/9/2017 mchana, na amerejea nchini Trh 27/7/2020 saa 7 mchana. Nimetafakari uwepo wa namba 7 katika matukio, kuna siri ktk hili?

Wataalamu wa haya mambo karibuni kwenye mjadala.
Kwani namba kama namba kasemaje...
maendeleo hayana chama
Ukiamini inaweza kufanya kazi, ukiipuuza nayo haitakuwa na maana wala nguvu yoyote
Hakuna siri yoyote

Ni wewe tu umeoverthink
 
kipapi

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
916
1,000
Kumekuwepo na nadharia (conspiracy theories) kuhusu namba kwenye Muda (Mwezi, Siku na Saa) kubeba siri nyingi za matukio mbalimbali yanayotokea dunia. Matukio yanaweza kuwa ni vifo nk.

Je, ni kweli kuna siri katika namba au fikra zetu tu katika kujenga taswira kuhusu matukio? Lissu alishambuliwa Trh 7/9/2017 mchana, na amerejea nchini Trh 27/7/2020 saa 7 mchana. Nimetafakari uwepo wa namba 7 katika matukio, kuna siri ktk hili?

Wataalamu wa haya mambo karibuni kwenye mjadala.
Mungu aliumba dunia kwasiku 7
Katika juma kuna siku 7
Mtoto akizaliwa anatolewa nje baada ya siku 7
Hata mbingu inasemekana zipo 7
Samehe 7 x 70
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom