Ujio wa interswitch afrika mashariki tuwe makini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujio wa interswitch afrika mashariki tuwe makini

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Aug 19, 2011.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kuna wenzetu humu wamewahi kupata matangazo toka kwa watu wanaotumia majina ya INTERSWITCH au kujifanya mawakala wa INTERSWITCH , unaambiwa ukingie kwenye tovuti ya interswitch na kubadili taarifa zako au ingiza mpya kwa sababu mtandao wa interswitch unaboreshwa zaidi . INTERSWITCH NI NINI ?
  Interswitch ni kampuni ya Nigeria inayotoa huduma za kibenki na fedha kwa njia ya electroniki na watoa huduma nyingi Nigeria zikiwemo benki ya kampuni za simu zimejiunga na mtandao wa Interswitch kwa ajili ya huduma za kifedha kwa njia ya elekitroniki . Kadi nyingi za ATM katika nchi ya Nigeria zimeunganishwa kwenye mtandao huu wa INTERSWITCH . Kampuni ya Interswitch Nigeria kwa sasa imeinunua kampuni moja iliyokuwa inaunganisha huduma za malipo ya fedha kwa elektroniki ya Uganda na kubadilishwa Jina na sasa inaitwa INTERSWITCH EAST AFRICA . TATIZO LIKO WAPI ? Watu wengi wa afrika magharibi haswa Nigeria wametumia jina la interswitch kwa ajili ya kuibia wengine fedha zao kwa njia ya mtandao pindi wanapojaza taarifa zao kwa njia ya mtandao wakidhani ni huduma halali ya Interswitch Nigeria lakini Kampuni hii muda mwingi imekuwa kimya . Kampuni hii sasa imeingia kwenye soko la afrika mashariki na kuanzia na huko Uganda kwa kununua kampuni moja lakini kama ni Uganda tu kwanini wanalazimika kutumia neno EAST AFRICA badala ya Interswitch Uganda ? sheria za usajili wa kampuni zinasemaje kuhusu suala hili ? Kwa sababu taasisi za fedha kama BOT na benki nyingine nchini hazijatoa taarifa kuhusu ujio huu na benki nyingine za afrika magharibi kwenye ardhi ya afrika mashariki kuna uwezekano watu wengi zaidi kuingia mkenge na kutoa taarifa zao zitakazowezesha wahalifu wa mtandao kutekeleza majukumu yao ya kihalifu kwa urahisi zaidi . Ndugu zangu tuwe makini na huduma hizi na tunaomba benki kuu ya Tanzania kutoa taarifa za kuelimisha mapema kwa umma wa watanzania kuhusu huduma hizi hapa kwetu kuna huduma inaitwa UMOJA SWITCH sina uhakika kama na yenyewe inaweza kununuliwa na INTERSWITCH ya Nigeria siku za karibuni . Ingawa tunapenda wote ukuaji wa teknologia unaorahisisha utendaji wa kazi na upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa njia rahisi zaidi lakini pindi tekinologia hii inavyotumika kinyume hasara yake ni kubwa sana na inaweza kudongosha uchumi wa makundi mengi ya watu na kufilisi wengine .
   
Loading...