'Ujinga' wa wapemba kutowekeza Pemba!!!!!!!!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Mimi huwa siwaelewi hawa wazanzibari wajiitao wapemba. Yaani wameishia kuwekeza bara huku wakiendelea kulalamika kwamba wanaonewa na waunguja ktk kuendesha nchi ya zanzibar. Uchunguzi umeonyesha kuwa sehemu kubwa ya biashara na majengo yapatikanayo kariakoo-eneo kubwa la biashara bongo yetu-yanamilikiwa au kendeshwa na wapemba.

Kwa thamani ya biashara wazifanyazo na milki ya majengo inayohodhiwa na wapemba, mtu ungetegemea hawa jamaa kuwa wameendeleza kwao pemba kama ilivyo kwa wafanyabiashara watokao mkoa wa kilimanjaro. Lakini ukienda pemba, mwenyewe utashangaa jinsi kulivyo duni kimaendelea kuanzia miundombinu hadi majengo ya makazi ya wakazi wake hali ni tofauti kwani huku bara wapemba ni miongoni mwa watu wanaoishi kwenye nyumba nzuri-nyingi zimejengwa kisasa kabisa.

Nawauliza wapemba, kwani kuna shida gani kama mkiendeleza kwenu pemba, badala ya kuwekeza bara halafu mnalalamika zanzibar mnaonewa ili hali kodi mnazolipa bara ndo zinazoleta hayo 'maendeleo' mnayoyapigia kelele?

Amkeni, jitambueni. Jueni kwa kuwekeza kwenu Tanganyika mnachangia pesa nyingi ktk maendeleo ya Tanganyika pesa mabyo ingechangia maendeleo ya Pemba kama mngewekeza Pemba.

Nimewasilisha!
 
Back
Top Bottom