REDEEMER.
JF-Expert Member
- Feb 22, 2015
- 8,925
- 14,880
Jana nilizungumza na ujumbe wa wadau wetu wa maendeleo kutoka Ujerumani, wakiongozwa na Balozi wa Ujerumani Tanzania, Mhe. Dkt. Wachter. Wajerumani wako tayari kutusaidia zaidi ya bilioni 10 kwa ajili ya mradi wetu wa maendeleo ya jamii kule Loliondo, ambapo tunakusudia kuboresha malisho ya mifugo, maji ya mifugo na watu, soko la mifugo na mbegu za kisasa za mifugo pamoja na mambo mengine kama kutengeneza mpango wa matumizi bora ya ardhi. Pia tutapata zaidi ya bilioni 40 za kitanzania kutoka Benki ya maendeleo ya Ujerumani kwa ajili ya kuboresha miundombinu kwenye pori la akiba la Selous.