Ujerumani yaipa Tanzania zaidi ya Tsh 50bn kwa ajili ya maendeleo ya jamii Loliondo na kuboresha miundombinu Selous

REDEEMER.

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
8,925
14,880
Kigwa.png

Jana nilizungumza na ujumbe wa wadau wetu wa maendeleo kutoka Ujerumani, wakiongozwa na Balozi wa Ujerumani Tanzania, Mhe. Dkt. Wachter. Wajerumani wako tayari kutusaidia zaidi ya bilioni 10 kwa ajili ya mradi wetu wa maendeleo ya jamii kule Loliondo, ambapo tunakusudia kuboresha malisho ya mifugo, maji ya mifugo na watu, soko la mifugo na mbegu za kisasa za mifugo pamoja na mambo mengine kama kutengeneza mpango wa matumizi bora ya ardhi. Pia tutapata zaidi ya bilioni 40 za kitanzania kutoka Benki ya maendeleo ya Ujerumani kwa ajili ya kuboresha miundombinu kwenye pori la akiba la Selous.
 
Hao wajerumani si ndio wanawatumia cdm kuvuruga nchi au imekuwaje tena? Sasa nadhani mmeamini wazungu wataendelea kutuongoza tu mpaka mwisho wa dunia hii. Na ile hadithi kwamba nchi yetu tutatengeneza nguo zetu tukishazivaa ndio tupelekee wazungu wakavae mitumba ni ulevi wa madaraka. Lugha zile ni za masikini jeuri.
 
Mbona hasemi kuwa mazungumzo haya yalianzishwa na watangulizi wake na hatimae huko Ujerumani wakakubaliana kutoa fedha hizo? Tusitafute kiki kwenye mambo yaliyoanzishwa na wengine huku tukiwatukana na kuwapakazia hao walio tangulia.
Anataka kutuambia maongezi ya jana ndiyo yameleta maamuzi hayo wakati wenye authority ya kukubali mchakato huo wako Ujerumani? Wenzie walishaandaa writeup za mradi huo hivyo yeye kuja kutaarifiwa kuwa fedha ziko tayari sio kumaanisha kuwa ndiye aliyesababisha. Kigwangwala aache hizo, akiona vyaelea ajue vimeundwa!
 
Kila taifa linataka kumpa Magufuli mapesa kila mzungu akisikia Magufuli anafanya utumbuzi anatoa pesa mfukoni ya kumpongeza hawa wazungu wameshachanganyikiwa na speed ya Magufuli hivyo tutegemee kila siku kumwagiwa mipesa tu BOT sasa wapanue account
 
Serikali ya Ujerumani imekuwa ikitoa misaada kwa zaidi ya miaka 50 kwa Serengeti National Park hiyo kiki umefeli Mheshimiwa. Umeshawatolea kashfa kubwa watalii wa Marekani kuwahusisha na mambo yenu ya CCM subiri tuone hii wizara utakavyoiua.
 
Mbona hasemi kuwa mazungumzo haya yalianzishwa na watangulizi wake na hatimae huko Ujerumani wakakubaliana kutoa fedha hizo? Tusitafute kiki kwenye mambo yaliyoanzishwa na wengine huku tukiwatukana na kuwapakazia hao walio tangulia.
Anataka kutuambia maongezi ya jana ndiyo yameleta maamuzi hayo wakati wenye authority ya kukubali mchakato huo wako Ujerumani? Wenzie walishaandaa writeup za mradi huo hivyo yeye kuja kutaarifiwa kuwa fedha ziko tayari sio kumaanisha kuwa ndiye aliyesababisha. Kigwangwala aache hizo, akiona vyaelea ajue vimeundwa!
Germany wameona kazi kubwa Kigwangala ameifanya Loliondo hivi karibuni ndio maana wameamua kumuunga mkono na speed yake ya kuwajibisha majangili
 
Mwongo sana wewe

Billioni 10 tu ndio zimetolewa na German

rekebisha heading ili kuwe na heshima
 
Hii ni Kazi ya Kagasheki na Nyalandu

Wagerman wamekurupuka tu wakaja na billion 10?

Poor propaganda
 
Mbona hasemi kuwa mazungumzo haya yalianzishwa na watangulizi wake na hatimae huko Ujerumani wakakubaliana kutoa fedha hizo? Tusitafute kiki kwenye mambo yaliyoanzishwa na wengine huku tukiwatukana na kuwapakazia hao walio tangulia.
Anataka kutuambia maongezi ya jana ndiyo yameleta maamuzi hayo wakati wenye authority ya kukubali mchakato huo wako Ujerumani? Wenzie walishaandaa writeup za mradi huo hivyo yeye kuja kutaarifiwa kuwa fedha ziko tayari sio kumaanisha kuwa ndiye aliyesababisha. Kigwangwala aache hizo, akiona vyaelea ajue vimeundwa!
Nyalandu ndiyo aliomba na kufanikisha kila kitu
 
Wewe unajua nini sasa, Tweet ya Kigwangala inasema billioni 10, wewe unasema billioni zaidi ya 50?

Unaweka chumvi ya Lake Natron...!! Bwaha bwahaaaaa

Poor propaganda
Hilo aliandika fungu la billion 10 na hapo sreenshot ameandika na billion 40 kila fungu linaenda kwenye kazi tofauti.
 
Mbona hasemi kuwa mazungumzo haya yalianzishwa na watangulizi wake na hatimae huko Ujerumani wakakubaliana kutoa fedha hizo? Tusitafute kiki kwenye mambo yaliyoanzishwa na wengine huku tukiwatukana na kuwapakazia hao walio tangulia.
Anataka kutuambia maongezi ya jana ndiyo yameleta maamuzi hayo wakati wenye authority ya kukubali mchakato huo wako Ujerumani? Wenzie walishaandaa writeup za mradi huo hivyo yeye kuja kutaarifiwa kuwa fedha ziko tayari sio kumaanisha kuwa ndiye aliyesababisha. Kigwangwala aache hizo, akiona vyaelea ajue vimeundwa!
Kwani vingapi havikuwa vikisemwa na watangulizi wake na bado hatukuhoji? Nchi ni yetu sote na si lazima kusema yote, kikubwa pesa tumepewa watanzania sote kama kushukuru tushukuru na kama hatutaki tuache
 
Back
Top Bottom