Ujenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujenzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mchakachuliwaji, Nov 30, 2010.

 1. M

  Mchakachuliwaji Member

  #1
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NIna hamu ya kujenga nyumba ya ghorofa. Nataka ghorofa moja tu na balcony ya juu.
  Natamani nyumba kwa ground floor iwe yenye rooms mbili zote self contained, jiko, library, living room pamoja na bafu/toilet inayojitegemea na kwa ghorofa ya kwanza natamani iwe na rooms tatu za self contained. Juu nataka kuwe wazi kwa juu lakini kingo za ukuta mix na grils.

  Sina ramani wala chochote ila nimeanza kufyatua tofali ya block na zimefikia 6000. Hela zipo za kuendelea kufyatua.

  Ratio ya cement na mchanga ni mfuko mmoja makarai 30 na hii ni kutoka kwa wazoefu mitaani (hakuna ghorofa huko mitaani nilikopata hii ratio!). Cement ni kutoka Tanga.

  Nimekadiria around 120,000 USD kama gharama yote na nitakamilisha mwaka huu ujao katikati. Hela sizipatia kwa mkupuo ndiyo maana nikaanzisha kufyatua kwanza ili baadaye nikipata nyingi nyingi ndiyo nianze bargaining (labda january katikati).
  Kiwanja low density nimeshanunua.

  Ombi:

  1. Tafadhali watalaam nishaurini nisije nikawa nachemka hasa kwenye ratio ya machanga na cement. Bora kama nimechemka nibadilishe matumizi ya matofali yaliyopo ili nianze upya. Nimesema hivi kwani nimemsikia mtu anasema sema sana kuwa hiyo ratio ana mashaka nayo.
  2. Je ni tofali ngapi, kwa makadirio, nahitaji kuwa nazo kuwa na hiyo 'DREAM HOUSE'

  Natanguliza shukrani nyingi.
   
 2. minda

  minda JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hiyo ratio ya 1:30 sio mbaya japo mi sio fundi ujenzi. nasikia inakubalika hata mpaka 1:35 lakini isizidi hapo>
   
 3. M

  MZEE SERENGETI JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Magufuli anaweza kuwa Msaada Zaidi.hana noma kabisa.
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ghorofa sio sana Tofali, Tofali ni nyama za kujazia tu, bali ghorofa ni ZEGE, (Nondo, Cement /Mchanga/Kokoto(ratio nzuri) ), Ningekushauri umtafute mtaalamu wa Soil kwanza aangalie hilo eneo lako (aina ya udongo, mfinyanzi, mchanga nk) na pia aangalie hilo eneo ni kavu ama ni eneo yowevu, ukishapata hayo majibu mtafute mtaalamu wa ujenzi akushauri utumie Nondo za milimeter ngapi kwenye Msingi, Colum na jamvi lenyewe,

  badala ya kuvyetua tofali ningekushauri uanze kukusanya Nondo, kokoto, Mchanga na weka pesa ya cement, Tofali wala sio kitu cha kuumiza kichwa kama unajenga ghorofa
   
 5. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ukitafuta wale wasanifu majengo watakuchorea ramani safi sana kulingana na haja yako
   
 6. M

  Mchakachuliwaji Member

  #6
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana. Ngoja nimsake huyo mtu wa soil kwanza.
   
 7. N

  Newvision JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza hongera for progressive ideas but at each step of your undertaking "consult reliable people in the field". Najua utahitaji beams na nondo zenye ubora siyo zile za chuma recycled la sivyo zitapinda. Asante nadhani wataalamu tunao hap JF watakupa nyeti zote
   
 8. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Asante sana kwa kunisaidia na mimi pia. Hizo nondo zikoje zikoje?
   
 9. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo umenikuna lugha uliyoitumia kwenye red uko BAKITA??hebu tudadafulie neno YOWEVU!
   
Loading...