Nimerudi kwenye msoto tena nishaurini

Nguva Jike

JF-Expert Member
Jan 22, 2018
995
1,260
Habari za asubuhi ndugu zangu wa JF.

Kwa miaka kadhaa nilikula msoto sana wa kimaisha kiasi cha kukosa hata pesa ya nyanya geto.Sometimes chai ya asubuhi ilinishinda,lunch ilikuwa inapiga chenga.

Akili ikanituma nijifunze kujenga nyumba.Nikamuomba fundi fulani niwe namsaidia mwisho nikawa fundi kamili nikaanza kupata kazi mitaani mpaka nami nikajenga nyumba yangu ya vyumba vitatu kimoja self-contained room.

Zali zalina shirika fulani wakakodisha nyumba yote nikaanza kuishi maisha mazuri sana kwa kodi waliyonipa.Heee! mwaka jana nyumba ikapitiwa na nguzo za umeme nikafanyiwa tathmini nibomoe nyumba loooh! wapangaji wakahama nimerudi kwenye msoto sipati hata shilingi ya tundu.

Aisee jamani nishaurini madili ya kujenga sipati mafundi wengi kama utitiri kodi sipati walionifanyia uthamini hawajanilipa hata senti wapangaji wanaogopa kupangisha itabomolewa.

Ushauri wenu please.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom