Ujenzi wa Hoteli Katika uwanja wa Nyamagana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujenzi wa Hoteli Katika uwanja wa Nyamagana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Morani75, Jan 29, 2008.

 1. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimesoma pale kwenye Mwananchi la leo (attached)

  http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4207

  kwa kweli inashangaza pale ambapo Mhe Waziri Magufuli anapojitahidi kupambana na ku-sevu uwanja wetu.... Hivi ni kichaa gani anasema hoteli ni muhimu kuliko uwanja especially wakati huu ambapo Rais anajitahidi kuinua kiwango cha soka?

  Katika hili ninasema "Waziri Magufuli, chukua 5 mzee wembe ni uleule usiachie kitu hapao kama ni hoteli wakajenge kwenye virgin lands ipo mingi sana Mwanza kwanza itasaidia kupanua Jiji.... Nyamagana watuachie tucheze soka na mengine!!!

  HApa ndipo ninapokaa na kuuliza:
  1. Viongozi wetu wanafikiria nini wanapofanya maamuzi?
  2. Priority za Tz zipo wapi?
  3. Hii issue ya kitu kidogo itatupeleka wapi? Nadhani hatutafika kw waKenya!

  Naomba kuwakilisha!!
   
 2. Mchumia juani

  Mchumia juani Member

  #2
  Jan 29, 2008
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 27
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Morani umenena lakini hata hivyo Magufuli kakata mzizi wa fitina kuna watu hawajali maslahi ya wananchi kabisa,Beach zote wamebinafsisha hata mpaka viwanja vya Wazi? Asante sana Magufuli
   
 3. B

  Bobby JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Naungana nanyi kumpongeza Magufuri kwa kazi nzuri ya kuzuia ufisadi huo ambao naona sasa umekosa hata chembe ya aibu.

  Lakini wakati nampongeza nataka nimkumbushe waziri kwamba Nyamagani ni sehemu moja ya mamia ya maeneo ambayo wananchi wanakilio kutokana na kuwa na watu wenye tamaa za kifisi na kuyauza kifisadi maneo ya wazi. Dar kuna maeneo mengi sana (mifano ninayo) ambayo yalipaswa kuwa maeneo ya wazi lakini yameuzwa na kujengwa petrol station,supermarket etc. Hofu yangu ni kwamba hili la Nyamagana limepata solution kwa kuwa limepigiwa kelele nchi nzima na ni sehemu ya kihistoria. Haya mengine mara nyingi kelele za wananchi hazifiki mbali na wenye nguvu za kipesa huwa wanashinda. Natamani Magufuli wa ANBEM afufuke na kuchukua hatua, huyu wa ari, nguvu mpya na kasi mpya ya kuchekacheka na ufisadi simwelewi bado.
   
 4. i

  ishengoma Member

  #4
  Jan 29, 2008
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  magufuri poa kwa kazi hii. I wish i were at that meeting
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nampongeza sana magufuli kwa hayo maamuzi lakini in reality na kama kweli kuna mwekezaji anataka kujenga hiyo complex pale nyamagana si busara kulikataa wazo hilo moja kwa moja. Ziandaliwe terms and conditions na ziwasilishwe kwa wananchi KAMA NI KWELI KUNA NIA NJEMA.PIA ITANGAZWE TENDA KWA WENYE UWEZO KUKOMPETE.

  mfano halmashauri ya jiji itafute eneo lingine kuubwa na hao wawekezaji wajenge uwanja bora ndio wapewe nyamagana.

  Najua wengi mtanipinga kwa haya
  1. Je ni sh. ngapi nyamagana imeiingizia halmashauri ya jiji la mWANZA MWAKA 2007?

  2. Hamuoni kwamba uwekezaji huo kama ni kwa nia njema lakini (win win situation) utalipa facelift jiji la Mwanza?
   
 6. Mushobozi

  Mushobozi JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2008
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 541
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  pesa ngapi zimeingia kwenye almashauri kwa mwaka huo, ila zimeshindwa kuboresha mahitaji madogo ya raia wa kawaida. pesa ni kitu gani kwa maisha na vipaumbele vya watoto wetu. nasikia ndege za minofu ya samaki zinaingiza zaidi ya bilion moja kwa mwezi.
   
Loading...