Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Mafundi wa kampuni ya ujenzi ya RJR wakiwa kazini kwenye
makutano ya barabara za Mandela na Nyerere jijini Dar es Salaam
Flyover inayotazamiwa kuoteshwa hapo makutano ya Mandela na Nyerere (TAZARA)
NIPASHE ilifika jana eneo hilo ambalo litajengwa barabara hizo na kukuta makandarasi wakiendelea na zoezi la kuhamisha mabomba. Akizungumza na gazeti hili, Msimamizi wa zoezi hilo, Peter Mitondo, tayari wamekamilisha uondoaji wa mabomba ndani ya Tazara na sasa wapo kwenye barabara kuu za magari.
Alisema uhamishaji huo wa mabomba ya maji kwenye barabara ya Tazara ili kupisha ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu.
Alipoulizwa ujenzi huo utachukua muda gani kukamilika, msimamizi huyo alisema hafahamu kwa kuwa mkandarasi atakayehusika atakuwa mwingine. Alisema mkandarasi wa sasa anayehusika kwenye kuyaondoa mabomba hayo ya maji ni kampuni za pamoja ambazo ni RJR, RJ na Jos Harsen.
Source: Nipashe