Ujenzi TAZARA flyover: Ni mwaka sasa sijaona kilichofanyika

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
37,896
43,791
Ni zaidi ya mwaka sasa tangu ujenzi wa Tazara flyover uanze, lakini leo nimepita pale nakuona patupu kabisa, hakuna kilichofanyika zaidi ya kublock njia na ile mijiwe mikubwa ya zege na kusababisha usumbufu kwa watumiaji barabara.

Nilitegemea kuona walau mashimo ya nguzo yakiwa yameanza kuchimbwa na hata nondo zikianza kusukwa ndani ya hayo mashimo. Kwa mwenye uelewa naomba anielimishe, nini kinaendelea pale kwa sasa, wapo kwenye hatua ipi ya ujenzi? au huu ujenzi work schedule yake ni miaka 100?

Update: Niliona kitu kama hiki

=======================================
UPDATE: (14/02/2017)
Baada ya Mheshimiwa waziri kusikia malalamiko yangu, jana alienda kutembelea ujenzi huo na kuwahimiza waongeze kasi ya ujenzi ili wananchi waanze kufaidika na kuepuka gharama kubwa wanazoingia kwa kukaa foleni muda mrefu.
1.JPG

source: Michuzi blog

=======================================
UPDATE: (16/06/2016) Ujenzi umekamilika kwa 40%; Makonda amewahimiza waongeze speed, ikiwezekana wafanye kazi usiku na mchana, pengine hakuridhishwa na kasi aliyoiona

======================================

UPDATE: (16/07/2017)Wafanyakazi wagomea udalali wa kikatili wanaofanyiwa na LABA contractors, wagoma

======================================

UPDATE: (02/08/2017)
Picha halisi ya flyover imeshaanza kuonekana, ujenzi unaleta matumaini kwa sasa, picha inajieleza
tapatalk_1501649695253.jpeg

================================
UPDATE: 15/09/2018
Serikali yaruhusu magari kutumia Tazara Fryover - JamiiForums

Msemaji mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amethibisha rasmi kuanza kutumika kwa Mfugale Fryover iliyopo Tazara ikiwa katika hatua za mwisho kuzinduliwa mwezi ujao (10) na Mh Rais.
 
bado wafadhili wanatafutwa wa kuendelea na Lot nyingine, ila Lot 1 kama unavyooena sasa tunamsubilia mfadhili wa Lot 2 na kuendelea.

teh teh Tanzania ya viwanda.
Mbona kipindi kile Mh. Rais JPM alisema kwamba serikali imeshalipa bilioni 100 kwa hao waJapan kwa ajili ya huo ujenzi?
 
Ungetafuta contract document na ukaona scope of work then ndo ungekuja kulalamika JF. Halafu hapa sio TANROADS au Wizara ya Ujenzi. Mh Mbarawa yuko twitter ukimuuliza swali within half an hour anakujibu. Serikali hij unauliza swali unapata majibu. Usikimbilie kulia lia huku
 
Ukisikia Kiherehere ndo icho!subiri ujionee nini maana ya HAPA KAZI TU..!! Hata barabara za mwendo kasi wengine walikuwa na kihehere kama hiki..!Oooh hatuoni kitu,wanatuwekea foleni mjini..!sasa wameona nini maana ya barabara mwendo kasi...lawama zao hata pongezi wanashindwa kutoa...
 
Acha mambo yaende pole pole mkuu,haraka haraka unaweza kujengewa flyover ambayo ikinyesha masika inatitia,baada masika mbili flyover chalii halafu tuanze lawama
Waache wajuzi waendelee na pilika zao
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Mama yetu Tanzania tuzid kumuombea

hivi james mbatia yupo mzee wa kuwatungia mtihani wa math ma profesa wa chuo kikuu cha udsm ktk maswali kumi wanapata moja mtihani wa darasa la saba.
 
nini kinaendelea pale kwa sasa, wapo kwenye hatua ipi ya ujenzi? au huu ujenzi work schedule yake ni miaka 100?
Wew ndio umepita leo na umeshaeleza kila kitu.

Ni zaidi ya mwaka sasa tangu ujenzi wa Tazara flyover uanze, lakini leo nimepita pale nakuona patupu kabisa, hakuna kilichofanyika zaidi ya kublock njia na ile mijiwe mikubwa ya zege na kusababisha usumbufu kwa watumiaji barabara. Nilitegemea kuona walau mashimo ya nguzo yakiwa yameanza kuchimbwa na hata nondo zikianza kusukwa ndani ya hayo mashimo. Kwa mwenye uelewa naomba anielimishe, nini kinaendelea pale kwa sasa, wapo kwenye hatua ipi ya ujenzi? au huu ujenzi work schedule yake ni miaka 100?
 
wINRpR9.jpg

huwa unapita tazara gani mkuu
 
Ungetafuta contract document na ukaona scope of work then ndo ungekuja kulalamika JF. Halafu hapa sio TANROADS au Wizara ya Ujenzi. Mh Mbarawa yuko twitter ukimuuliza swali within half an hour anakujibu. Serikali hij unauliza swali unapata majibu. Usikimbilie kulia lia huku
vp Mbona povu tena?
 
Ni zaidi ya mwaka sasa tangu ujenzi wa Tazara flyover uanze, lakini leo nimepita pale nakuona patupu kabisa, hakuna kilichofanyika zaidi ya kublock njia na ile mijiwe mikubwa ya zege na kusababisha usumbufu kwa watumiaji barabara. Nilitegemea kuona walau mashimo ya nguzo yakiwa yameanza kuchimbwa na hata nondo zikianza kusukwa ndani ya hayo mashimo. Kwa mwenye uelewa naomba anielimishe, nini kinaendelea pale kwa sasa, wapo kwenye hatua ipi ya ujenzi? au huu ujenzi work schedule yake ni miaka 100?
DAR ES SALAAM | Tazara flyover | U/C - Page 10 - SkyscraperCity
Fuatilia link hii, uone wenzako wanavyojadili mambo kwa fact. Siku nyingine hutakuwa na haja ya kupita tazara kupoteza mafuta bure. Maana hiyo link wanajadili na itaendelea hadi commissioning ya hiyo project
 
Back
Top Bottom