Ujenzi: Namna sahihi ya kupunguza gharama wakati wa kujaza kifusi

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,526
3,802
Habari wakuu,

Napenda kufahamu yoyote mwenye uzoefu wa namna sahihi ya kupunguza gharama wakati kujaza kifusi wakati wa ujenzi wa nyumba baada ya kumaliza msingi.

Hii ni baada ya kuona jirani yangu amemaliza msingi na jana amemaliza kujaza kifusi ambacho kimemcost sh milioni moja na laki nane. Kifusi trip moja ni sh 90,000 na yeye alijaza vifusi trip 20.

Kwa yeyote mwenye uzoefu atufahamishe aliwezaje kupunguza gharama za kujaza kifusi.

Karibu kwa mawazo yenu
 
Kwanza usijenge msingi mrefu kwenda juu.

Pili, kama huna shimo la choo chimba kubwa liwe na upana angalau futi 6 kwa 6 hadi 10 kwa 10 halafu udongo wake utumie kujazia kwenye msingi.

Tatu, gharama hutegemea pia na utambarare wa kiwanja.

Nne, kama kwenye kiwanja chako kichuguu kitumie kujazia.

Kupanga ni kuchagua usiige kunya kwa tembo mkuu.
 
Asante sana mkuu
 
kuhusu udongo kutoa kwenye shimo la choo inategemea na mazingira kama kuna udongo ufinyanzi aufai hatakidgo sababu itasababisha nyufa kwenye nyumba,
ndo maana wengi uagiza udongo toka mbali

Sent from my Nokia 2 using JamiiForums mobile app
 
Chimba shimo la maji taka. Udongo wake ni mwingi sana unaweza kujaza nyumba nzima au sehemu kubwa tu.
 
Inategemea pia na mahali ulipo, huku kwetu kifusi 60,000 kwa hivyo hapo kwenye 20 unaokoa laki 6
 
Kama unajenga bondeni usiogope kunyenyua msingi walau kozi 5; usiogope gharama.

Othewise ushauri wa jamaa kuhusu shimo la choo kutumika kujazia kifusi wengi tumelitumia.
 
Kama unajenga bondeni usiogope kunyenyua msingi walau kozi 5; usiogope gharama.

Othewise ushauri wa jamaa kuhusu shimo la choo kutumika kujazia kifusi wengi tumelitumia.
Au ajenge msingi wa steps kama kiwanja kina slope kubwa
 
Unachimba choo Udongo usipotosha unachimba kisima cha MAJI Udongo usipotosha unachimba bwawa la samaki
Udongo wa kujazia msingi usipotosha nitag
 
Hii stage ndo inanitesa kwa sasa, nimeshaingiza gari 6 mpaka Sasa lkn naona msingi bado unadai, hivyo nimeamua kuchimba shimo la choo
 
Kama unajenga bondeni usiogope kunyenyua msingi walau kozi 5; usiogope gharama.

Othewise ushauri wa jamaa kuhusu shimo la choo kutumika kujazia kifusi wengi tumelitumia.
Bondeni kwa kozi tano mkuu mbona chache sana
 
Hili halikwepeki halina ujanja, ni miongoni mwa gharama za ujenzi.

Ukianza ujenzi lazima ufahamu kuwa kuna kifusi kitahitajika, hiki kinategemea urefu wa msingi wa nyumba yako.

Gharama itapungua endapo kifusi hicho kitakuwa hakitoki mbali na eneo unalofanyia ujenzi wako. Na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom