Ujenzi: Je, hii nyumba ya TAKUKURU Dodoma inafikia thamani tajwa ya Tsh. 143 milioni?

Covid-19

Senior Member
Mar 2, 2020
162
364


Karibuni waumini wa majadiliano katika mjadala huu ambao mh Rais amesema angeweza kujenga nyumba hii kwa mill 43.

Kwa mtazamo wangu, licha ya kutoiona nyumba hii kwa ndani huwezi jenga chini ya million 90 na kama gharama za vifaa, mchanga na cement eneo husika zipo juu kufika mill 100 sioni ajabu kwa upande wangu.

Karibuni mafundi kwa majadiliano.

FB_IMG_1595439481702.jpeg
 
Ukinipa M 143 nakuletea nyumba kama hiyo mbili na vimilioni vichache vinabaki.
Huwezi mkuu, nyumba za serikali hazijengwi na vifaa vya ujenzi vya hovyo hovyo.
Tofali grade one tena za kulaza mara nyingi, ratio ya cement ya hali ya juu na bati gauge 26.
Huwa mnakurupuka mnalinganisha na vibanda vyetu vya mtaani.
Pili huwa kuna bei elekezi ya ujenzi mfano mdogo...
...majengo ya hospitali cost/sqm huwa ni 850,000
...magodauni cost/aqm ni 500,000
Na hapa kuna washauri/consultants lukuki
Mfano.. Quantity surveyors
...architects
....structural Eng
Na kadhalika na hawa wote wanalipwa ghali, hapa bado hujajua finishing ya ndani na SAMANI zake.
Msiwe mnakurupuka bila kuwa na ufahamu sahihi

Huwezi kuzunguka nyumba eti ukapata gharama za ujenzi.
Pitia manunuzi na pitia kitabu cha consultants uone mapendekezo yao katika ujenzi pamoja na samani zilizopo ndani
 
kwa dodoma hiyo si nyumba ya thamani hiyo??, wana dodoma wanajua. Ujinga wa dar wanataka kuuleta dodoma haiwezekani. Rais anatambua ujinga huu, hiyo nyumba kwa dodoma inajengwa kwa thamani ya chini ya milioni 50 yaani hapo hata uuziwe material kwa bei ya juu sana...utaishia kujenga kwa gharama ya chini ya milioni 50.

Utakuta mkurugenzi alipokea milioni 10 kutoka kwa mkandarasi, ndio maana mkandarasi ka balance mambo imetoka hivyo. Mlolongo wa wapigaji upo kwenye wateule wake hadi kwa mkandarasi
 
Hatuwezi ithamanisha hiyo nyumba bila kujua imechimbwa msingi kwenda chini futi ngapi,
Foundation imetumia material yapi, pia tiles hapo ndani katumia zipi, na milango ya hapo ndani ikoje, ratio ya kiserikali inajulikana ni ya ukweli,
Ukikuta ni ujenzi wa serikali ninavyoujua million 120 zinakata.
Na kutokana na material katumia yapi
Huenda walifwatua tofali inchi 6 na ratio ikawa ni tofali 20 kwa mfuko.
 
Mheshimiwa Raisi yupo sahihi kabisa, kwa milioni 40 with effective supervision unajenga kama hiyo
Ila kumbuka huwez jenga nyumba ya taasisi ukasupervise kama yako, hii inaenda na wataalam, tofali hadi upeleke maabara, zege pia, i bet kwa construction process halisi zikifuatwa hii nyumba inafika 110mil.
Kumbuka kila kitu kinatakiwa kiwe standard
 
kwa dodoma hiyo si nyumba ya thamani hiyo??, wana dodoma wanajua. Ujinga wa dar wanataka kuuleta dodoma haiwezekani. Rais anatambua ujinga huu, hiyo nyumba kwa dodoma inajengwa kwa thamani ya chini ya milioni 50 yaani hapo hata uuziwe material kwa bei ya juu sana...utaishia kujenga kwa gharama ya chini ya milioni 50.

Utakuta mkurugenzi alipokea milioni 10 kutoka kwa mkandarasi, ndio maana mkandarasi ka balance mambo imetoka hivyo. Mlolongo wa wapigaji upo kwenye wateule wake hadi kwa mkandarasi
Hujui lolote mkuu na ukubali hilo.
Hiyo ni nyumba ya serikali huwezi kujenga kwa gharama hiyo.
Dodoma baadhi ya vifaa vya msjenzi ni ghali sana tofauti na dar.
Pili hivi unajua hiyo gharama ni pamoja na thamani zake za ndani?
Unajua kuna vyumba vingapi?
Unajua wamerumia tofali za gade gani?
Unajua tofali zimelazwa au kusimamishwa?
Unajua marumaru zimetolewa wapi...Spanish au India?
Tujifunze kuhukumu kwa haki wakuu
 
Back
Top Bottom