Ujenzi Bwawa La Nyerere wafikia asilimia 90, uzalishaji kuanza mwezi Juni 2024

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
WAZIRI wa Nishati, January Makamba ameeleza kuwa Ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP) umefikia asimilia 90 huku shughuli ya kufunga mitambo ya kufua umeme pamoja na nyumba yake ikiwa imefikia asilimia 70

Akizungumza wakati akiongoza viongozi wa Baraza la Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki (TEC), kutembelea mradi huo Waziri Makamba amesema kumekuwa na mwenendo mzuri wa mtiririko wa maji yanayoingia katika bwawa hilo ambapo sasa mita za ujazo katika bwawa hilo zimefikia 163.7 za usawa bahari kutoka mita 163.61 alizozitangaza wiki iliyopita jijini Dares Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya mradi huo.

"Maana yake leo tungekuwa tumefunga mitambo ya kuzalisha umeme tungeanza shughuli hi. Lakini mmeona kazi ya kufunga mitambo ya kufua umeme inaendelea pamoja na nyumba ya mitambo hii shughuli yake imefikia asilimia 70," alisema.

Waziri Alisema matarajio ni kuona Februari mwakani wakianza majaribio ya kuzungusha mitambo hiyo na kabla ya Juni mwaka 2024 kuanza rasmi shughuli za kuzalisha umeme wa megawati 2,115 utakaoingizwa katika gridi ya Taifa.
 
Kwa hiyo na SGR itaanza wakati huo!! Maana na yenyewe kila siku ni danadana tu.
 
Unawaamini hao makitu , ikifika 2024 utaambiwea ni April 2025
 
Back
Top Bottom