Ujenzi barabara Kimara hadi Kibaha wafikia 52%

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1574342850157.png


UJENZI wa upanuzi wa barabara ya Morogoro kwa njia nane kuanzia Kimara hadi Kibaha, umeelezwa kuwa unaendelea kwa kasi na mpaka sasa umefi kia asilimia 52.85 ya ujenzi. Kwa upande wa muda uliotumika kutekeleza mradi huo unaotarajiwa kukamilika Januari 20, 2021 ni asilimia 51.04.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ngusa, aliliambia gazeti hili jana ofisini kwake kuwa mradi huo unaendelea vizuri, lakini changamoto kubwa ni mvua. “Hatuna mashaka kwamba mradi utakamilika kwa mujibu wa mkataba kwa muda uliopangwa.

Tupo vizuri na ni mategemeo kwamba kwa mwaka mmoja uliobaki, utakamilika ila changamoto pekee ni mvua,” alisema Ngusa. Akifafanua kuhusu maeneo yaliyokamilika, Ngusa alisema makaravati ya kawaida yote 52 yamekamilika na madaraja matano kati ya saba yamekamilika. Madaraja hayo ni mawili ya Kibamba, mawili ya Kiluvya na moja la Mpiji.

Daraja ambalo bado ni la moja la Mpiji na Kibamba. Ngusa alisema hatua za ujenzi zinaendelea katika barabara za michepuko kutokea barabara kuu ya Morogoro inayopanuliwa kwa njia nane katika maeneo ya Kimara Mwisho, Suka, Temboni, Msuguli, Mbezi mwisho, Kwa Yusufu, Luguruni, Kibamba (daraja la juu) na Kiluvya.

Gazeti hili lilipita katika ameneo hayo na kuona njia hizo za michepuko, zikiwekewa mzunguko (round about) ambapo kwa Mbezi mwisho tayari kuna mizunguko minne inayotumiwa na magari yanayotokea Goba, Ubungo na Malamba Mawili kuingia na kutoka Mbezi. Awali, Meneja wa Mradi ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Julius Ndyamukama aliliambia gazeti hili wiki iliyopita kuwa mradi huo umefikia asilimia 50 na kazi inaendelea vizuri.

Mradi huo unaotekelezwa kwa fedha za ndani, unatekelezwa katika mpango wa kupunguza msongamano katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuharakisha shughuli za maendeleo na huduma za jamii.
 
I stand to be corrected. Hizo lane mbili za katikati in kwa ajili ya BRT? Kama ndiyo, mbona hapaonekani provision ya vituo vya mabasi?
 
Kuna kipindi nilisikia kuwa ile flyover ya Kibamba na Mbezi nako itakuwepo,au pale Mbezi ndio wameshamaliza...?
 
kweli sasa Jiji la DSM linakua kwa kasi ya kimbunga!
Jiji sasa linatanuka kuelwkea kibamba na kiluvya ni wakati sasa wa kuwekeza mirada ktk maeneo hayo
 
Back
Top Bottom