Ujenzi Bandari ya Bagamoyo kuanza mwakani

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
277
801
Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo katika mwaka ujao wa fedha 2023/24, ikiwa itafikia makubaliano na wawekezaji kuanza kazi kabla ya muda huo.

Wazo la ujenzi wa bandari wa Bagamoyo lilianza wakati wa Serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete. Hata hivyo, Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani ilitupilia mbali mradi huo.

Juni 10, 2019, Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli alieleza wakati akizungumza na wafanyabiashara Ikulu jijini Dar es Salaam, kwamba alizuia ujenzi wa bandari ya Bagamoyo, kwa sababu kuna masharti magumu yaliyotolewa na mwekezaji wa mradi huo.

Magufuli aliyefariki dunia Machi 19 mwaka jana, alisema miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kuwa baada ya ujenzi huo wa bandari kukamilika, Tanzania haitaruhusiwa kujenga na kuendeleza bandari nyingine yoyote Pwani ya Bahari ya Hindi kuanzia Tanga mpaka Mtwara.

Hata hivyo, Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani Machi 19 mwaka jana, baada ya kifo cha Magufuli, alirejesha mradi huo na sasa mamlaka za Serikali zimeanza mchakato wa kujenga bandari ya Dar es Salaam huku kukiwa na matarajio makubwa.

Juzi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa alibainisha hawatalazimika kusubiri zaidi wawekezaji kuanza ujenzi wa bandari hiyo.

“Wawekezaji wataungana nasi mbele ya safari,” alisema Mbossa wakati wa mkutano na bodi ya wakurugenzi wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) uliofanyika katika makao makuu ya TPA.

Alibainisha kuwa kampuni kadhaa za kimataifa zimeonyesha nia ya kuendeleza na kuendesha mradi wa bandari ya Bagamoyo wenye thamani ya Dola za Marekani 10 bilioni (takriban Sh23 trilioni).

Mbossa hakutaja majina ya kampuni hizo kwa madai bado ziko katika hatua ya awali ya ushiriki.

“Tumedhamiria kujenga bandari ya Bagamoyo katika jitihada za kupunguza msongamano wa mizigo katika bandari ya Dar na kuvutia wateja wetu,” alisisitiza.

Mei 6 mwaka huu, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk Ashatu Kijaji akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2022/2023 alisema, Serikali imefufua majadiliano ya uendelezaji wa bandari hiyo.

Alisema katika mwaka 2021/2022, wizara imefufua majadiliano na wawekezaji wa Kampuni ya China, Merchants Holdings (International) Co. Ltd (CMHI) na Oman Investment Authority (OIA) ambayo awali ilikuwa inaitwa Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali ya Oman (SGRF).

Dk Kijaji alisema majadiliano hayo yanahusu eneo dogo la Mradi wa BSEZ kwa kuendeleza eneo la hekta 3,087 kati ya hekta 9,887 ambapo unahusisha ujenzi wa Bandari (Sea 38 Port).

Aidha, katika maelezo yake ya juzi, Mbossa alisema takwimu rasmi zinaonyesha bandari ya Dar es Salaam inahudumia tani milioni 17.025 za mizigo kwa mwaka na mpango wa sasa ni kuongezeka hadi tani milioni 30 ifikapo 2030.

Chanzo: MWANANCHI
 

Black Sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
22,932
31,864
Safi sana yaani nchi kubwa haina bandari kubwa hata Tatu
Ajira zitapatikana na mizigo itaongezeka pia Zahma za bandari ya Dar zitapungua
Tunaahitaji hiyo bandari kwa ushindani na kukuza uchumi na kupunguza msongamano na utapeli dar
 

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,082
2,770
Kilicho wazi ni kuwa jambo hilo liko katika hatua changa kabisa. Kuna hakihali ya uwekezaji. Mradi wa 23T haupaswi kuanza mwekezaji hajapatikana. Hii habari “tutaanza na atatukuta mbele” ni fedheha!! Na wakienda namna hiyo, itachukua miaka zaidi ya 10 kujenga bandari hii!

Waanze ujenzi baada ya mwekezaji kupatikana. Nchi haina uwezo wa kufanya SGR, JNHP na Bandari ya Bagamoyo kwa wakati mmoja na ikaendelea kufanya miradi mingine midogo mingi na kukidhi recurrent expenditure!!
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Top Bottom