Ujasusi wa Kisoka

vengu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
730
529
Chondechonde viongozi wa Tanzania wakati ndio huu. Wakati nchi nyingi hapa Africa zinastruggle kutafuta kujulikana kisoka hapa nyumbani MWenyezi Mungu ametubariki kwa namna nyingine na ya kipekee, kuna mambo machache ambayo serikali yetu ikiwa makini nchi itafika mbali hata kama hatuna vipaji kama wenzetu wa west Africa na kwingineko.

Ikumbukwe ni juzi tu Tanzania imeshika nafasi ya tano katika ubora wa ligi barani Africa Sasa ni wakati muafaka serikali kukaa chini na wadau wote wa mpira wa miguu na kupanga mikakati mafhubuti ambayo itafanya tuzidi kuwa juu kama EPL kwa Africa.

Mambo ya msingi yanayotakiwa kufanywa na serikali ni kujenga viwanja Bora vya michezo(hivi vya CCM vingi havifai),kuhamasisha wadau kujenga academy Kila mkoa kwa ajili ya vijana wetu, kutumia mbinu za kijasusi Ili kujua wenzetu wamefanikiwaje katika ligi zao, kupunguza utitiri was Kodi katika vifaa vya michezo na makampuni yanayojihusisha na ufadhili wa soka.

Nina mengi mengine yako moyoni, chondechonde serikali wakati ndio huu kabla wenzetu hawajaamka sisi, tujikite huku.
 
Hii kusema ligi ya Tanzania ni ligi bora kwa Afrika ni kwa vigezo gani?

Je, nikiorodhesha nchi 9 tu zipi tumezipita? Misri, Moroko, Afrika kusini, Senegal, Tunisia, Aljeria, Angola, Ghana, Nigeria.

Vigezo ni kabumbu linalo chezwa na timu zetu, wingi wa watazamaji, au kitu gani?
 
Ghana na senegal ligi zao hazina mpira wa kutisha sana ata naijeria wepesi tu
 
Hii kusema ligi ya Tanzania ni ligi bora kwa Afrika ni kwa vigezo gani?

Je, nikiorodhesha nchi 9 tu zipi tumezipita? Misri, Moroko, Afrika kusini, Senegal, Tunisia, Aljeria, Angola, Ghana, Nigeria.

Vigezo ni kabumbu linalo chezwa na timu zetu, wingi wa watazamaji, au kitu gani?
Ukiangalia ligi za wenzetu unaweza kusema afadhail ya ligi yetu
 
Back
Top Bottom