Ujasusi ndani ya Boeing

Mkuu Umesema kweli kabisa ila Engine hata ikinunuliwa haiwezi kufungwa kwenye ndege bila Boeing kuihakiki, hawawezi kuwa wajinga kiasi hicho wanunue Engine kisha waifunge kimya kimya bila kuifanyia check up yoyote.
Pia report ya kweli kabisa Boeing hawawezi kuitoa, wanachofanya ni kuhakikisha kuwa hawakimbiwi na wateja, tazama Trump alivyochanganyikiwa na kuanza kulaumu ma pilot wa Africa.
Kutengeneza madirisha ya Oval shape hayo ni maboresho Kwa ndege na si kwamba hadi litokee tatizo ndo Wanafanya check up ,check up ni lazima mkuu kwa kila kifaa cha Aviation.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani anajua kuwa jiwe ni diplomasia ziro so lzm awe mpole
Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Report haikutoka Boeing, black box zilipelekwa Ufaransa kusomwa na taasis ya kimataifa, sio issue ya Boeing tena wala Trump maana Trump lazima aitetee sababu ni shirika la taifa lake na lingachangia kodi kwa kiasi kikubwa hata ukiangalia secretary wake alimtoa huko Boeing kama wewe ni mfatiliaji wa mambo, Ethiopia walikataa kupeleka raw data kwa Boeing na FAA kwa kuhofia uchakachuaji wa taarifa hivyo Black Box zilipelewa Ufaransa kama nilivyoelewa awali, taarifa za awali za mwenendo wa ndege hazijaonesha tatizo la engine kuna website inayojitegemea ambayo huwa inachukua live feed data za ndege kupitia satellite labda ungeingia huko nako uangalie (binafsi ninafatilia sana maswala ya aviation kwa miaka kadhaa sasa ndo maana niko aware na kinachoendelea) , kuhusu madirisha pointi yangu iIikuwa kujaribu kukuonesha HATUA ya usafiri wa anga kuwa ajali ziliwapa changamoto ya kujua wapi walikosea na nyingi ya ajali hizo HAIKUWA ISSUE YA UJASUSI so hiyo idea yako ya ujasusi isiwe ndo kigezo kikuu , angalia channel ya smithsonian kwenye youtube au nenda kwenye tovuti yao utapata idea ya ninachoongea ila kama utakuwa unajibu bila kuangalia taarifa zingine kwingine utakuwa unazunguka pale pale kwenye engine kitu ambacho hata tu flight simulator anayefatilia habari za aviation anaweza kukuambia sio lazima rubani au mdau wa aviation
 
Maelezo yako ni sahihi kabisa. Watengenezaji wakubwa wa engine za ndege ni
1. Rolls Royce co, (UK)
2. General Electric Co. (US)
3. Pratt & Whitney co. (Canada/US).

Shida ya Boeing 737 Max 8 & 9 ni kwenye mfumo wa kompyuta wa kuongozea ndege, inasoma vibaya maelekezo. Wameanza marekebisho, hope watarudi hewani miezi michache ijayo.
 
Ukitaka kuamini kuwa ujasusi ulihusika, Jiulize kwa nini Air Force One ilitengenezwa chini ya uangalizi wa wataalamu wa serikali? Kwanini wasingeiamini tu Boeing yenyewe iwatengenezee na kuwakabidhi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuu ukweli ujasusi ni hatari....vipi sisi Tanzania hatutumii huo ujasusi?
 
Ukitaka kuamini kuwa ujasusi ulihusika, Jiulize kwa nini Air Force One ilitengenezwa chini ya uangalizi wa wataalamu wa serikali? Kwanini wasingeiamini tu Boeing yenyewe iwatengenezee na kuwakabidhi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Bro, Serikali inaposimamia haimaanishi ni kwaajili ya kuzuia ujasusi kama ingekuwa hivyo Lockheed martin na Boeing wasingetengeneza ndege za kivita maana jet fighter karibu zote zimetengezwa na kampuni binafsi ikiwemo Boeing, na hata wanapohitaji ndege mpya huwa wanatoa tenda na mara nyingi wanapelekewa ndege iliyokamilika na kukaa kuijadili, labda urudi tena usome historia ya fighter jet nyingi za marekani utanisoma nachokizungumza, ujasusi unawezekana ila nachokiona unaenda sana kwenye ujasusi bila kuangalia factors muhimu nachoshauri soma kwanza issue zinazohusu mambo ya aviation ukimaliza ndo uende kwenye mambo ya ujasusi maana utakuwa unaenda one step ahead huku nyuma unawaacha watu na taarifa ambazo nyingi ni za kupikwa itakuwa kama story za vijiweni tu sasa kwa wauza kahawa - njoo na data sahihi weka links tuendelee mbele
 
Ukitaka kuamini kuwa ujasusi ulihusika, Jiulize kwa nini Air Force One ilitengenezwa chini ya uangalizi wa wataalamu wa serikali? Kwanini wasingeiamini tu Boeing yenyewe iwatengenezee na kuwakabidhi?

Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaa bhana, duniani kote Raisi ndio first citizen lazima alindwe kwa gharama yeyote.... Kila kitu anachofanya,kula,kwenda,tumia,watu anaokutana nao lazima viwe classified au kuchunguzwa kwanza kuimalisha ulinzi..... Na kwa taarifa yako siyo Air Force One pekeee ambayo Ni uundwaji wake unasimiwa kwa Hari juu na kwa Siri kutunza mbinu za kiulinzi...

Magari anauotumia Raisi ie Cardilac One,Marine One, Blueprint za ikulu, kwa Raisi siyo mtu wa mchezo mchezo

Hata huku kwetu Africa unaona ulinzi wa Marais wetu walivyo na ulinzi wa ya Hali ya juu, japo hatujaendelea sana kiteknolojia kuweza tengeneza gari na ndege za maraisi wetu kwa usiri wa kusimamiwa na sisi wenyewe lakini unatosha kulingana na aina za maadaui (wa ndani ya Africa)ambao wanaweza kushambulia maraisi wetu....

Sasa Kama wewe ulitaka ndege ya Raisi wa marekani ikanunuliwe Kama unavyoenda kununua ndege ya abiria au mtu binafsi..kweli mkuu

Huku kwetu Africa TU gari za maraisi wetu hazinunuliwi hivyo Kama unavyoenda nunua sijui Benz au BMW la mtu binafsi..
Wanazotumia Marais Ni military version, nadhani unajua kitu au vitu vikiwa vya kijeshi maana yake Ni siri/ulinzi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa anazingua au anajichanganya.......
Pia hata hao Lockheed Martin na makampuni mengine yote yanayotengeneza vifaa vya ulinzi au jeshi project hizo lazima ziwe jini ya idara ya ulinzi ya marekani na zinakuwa classified partly hivyo sio rahisi KUPATA taarifa zote 100% vitu hivyo ndo maana ya ulinzi niwa na Siri huwezi ukaacha maadui zako wakajua 100% ya mbinu zako na vifaa vyako vya kujilinda na vya kivita...

Kwa hiyo hata fighter jets system zake, design na operation capabilities zake siyo 100% public knowledge, na hata washirika/ marafiki wa marekani wanao nunua vifaa vya kijeshi/ndege/Rada toka marekani siyo TU wanapewa/uziwa version ambazo zinautofauti kwa namna moja au nyingine na zile ambazo wanatumia wenyewe/jeshi ya marekani alikini pia unasign non disclosure agreement kuhakikisha vifaa hivyo hawezi guswa na maadau wa marekani yaani warusi, wachina na the alike.......



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi naona bro anatuelekeza kwenye story za kahawa...ngoja tumsikilizie...
 
Mkuu akili za kuambiwa changanya na zako, hivi unajua mambo ya aviation yanafanyika kwa tahadhari kubwa Sana?
Kwa hiyo waliufunga Huo mfumo wa Computer bila verification yoyote? Hiyo siyo baskeli ndugu, Kaa chini ufikiri kwa kina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hapa Tunaongelea intelligence, unadhani ndani ya Lockheed Martin hakuna majasusi?
Unadhani ndani ya jeshi la Marekani hakuna majasusi?
Wapo kila kona ya Dunia, na wakipata upenyo hukamilisha kazi walizotumwa, mada hii ni nzuri sana imenipa mwanga zaidi juu ya uelewa wa watu na mambo ya kijasusi kupitia michango yao.
Nimebaini wengi wetu ni weupe mno kichwani.
Nina changamoto kubwa mno kwenye part 3 sehemu ya mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijajua unapinga nini na una support nini, unazunguka kupinga at the end unarudi upande wangu tena.
Kumbe unakiri hujuma zipo ndo maana Rais lazima alindwe Kwa nguvu zote, sasa Kwanini hujuma pia zisifanyike kibiashara?
Sielewi hasa logic yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Unataka niweke data zipi? Za video ikionyesha hujuma dhidi ya Boeing 737?
Hebu jaribu twende pamoja kwenye mada yangu mbona ipo clear mno, uliwahi kuona wapi ndege mpya kabisa zikaanguka mfululizo kwa similarities zile zile za ajali? as if the manufacturers were students

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla hujarudi naomba unisaidie kufahamu ni nani aliyekuwa akipiga picha ndani ya ndege ya Ethiopian wakati ikiwa katika msukosuko na hatimaye kuananguka u wakati matukio ya ndege zingine hajarekodiwa kama ile na rubani alikuwa wapi maana kwenye cockpit hakuwepo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…