mfumo wetu wa biashara unaharibika kadri siku zinavyokwenda, wengi wamamua kuwa wezi/matapeli na serikali inakaa kimya kwa kuwa na viongozi wetu nao ni wa jinsi hiyo. Huwa nachukizwa sana na tabia ya hawa wanaojiita wajasiriamali kufanya biashara ndani ya vyombo vya usafiri, hivi hii ipo duniani kote au ni bongo tu, nisijekuwa nashangaa mambo ambayo ndio mfumo unaotumika duniani kote. Isitoshe hawa wanaofanya biashara hizi hawapatiwi mafunzo juu ya maelezo ya bidhaa husika, kigezo pale ni utaalamu wako wa kupiga soga. Huu ujasiriamali wa kuwa wachuuzi ninashindwa kuielewa sera hii, nilifikiri ujasiriamali ilikuwa ni ujasri katika kuzalisha mali, sasa ni ujasiri katika kufanya usanii......!!!????