Ujasiri wa wanawake kupima UKIMWI huwa unatokea wapi?

Affet

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
1,189
1,663
Habari zenu, mimi ni kijana mwenzenu msomaji mzuri sana humu ila si muanzishaji sana wa nyuzi kuna jambo kidogo huwa linanitatiza wanawake niliowahi kuwa nao wengi huwa na mambo mengi yaani hawajatulia ila sasa kinachonishangaza linapofika suala la kupima.

Mimi ninayejifanya mtulivu ndie muoga namba 1 halafu hawa wao kupima ni kama kunywa maji tu muda wowote popote wapo tayari na hii si kwangu tu hata rafiki zangu wawili watatu kwenye stori stori wamewahi kuongelea hii ishu.

Kwanini wanaume wengi (si wote) tunakuwa waoga sana linapofika suala la kupima?

Karibuni wadau.

1622714878698.png

 
Ni kweli hata Takwimu za upimaji VVU zinaonyesha kuwa Wanawake wengi ndio wanaojitokeza kupima kuliko wanaume.

Pia Wanawake wajawazito wanapoenda kuanza Clinik nao wanalazimika kupima kama sehemu ya vipimo vya lazima hivyo takwimu bado itakuwa kubwa kwao kuliko wanaume.

Na hata ukiangalia njia za maambukizi. Utagundua kuwa wanawake ndio wapo kwenye risk kubwa ya kuambukizwa tofauti na wanaume. Hivyo wanawake makini huwa wanapopata mpenzi mpya lazima watoe sharti la kwenda kupima kwanza.
 
Siku hizi mwanamke anapaswa kwenda na mme wake kiliniki ili wapimwe wote sasa Leo asubuhi jirani yangu aliamkia kwa mwenyekiti wa mtaa ili amwandikie barua kuwa yeye hayupo ili barua hiyo aendenayo mke wake kiliniki aweze kupata vipimo hapo ndipo watu wote walikuwa kwa mwenyekiti wa mtaa nikiwepo na mimi tuliposhangaa kwa nini wanaume wanogopa kupima?
 
Back
Top Bottom