Ulirchdov
JF-Expert Member
- Apr 4, 2019
- 356
- 258
Habari zenu ndugu wanajukwaa!!
Nianze kwa kusema kwamba siku zote ukiwa mwoga kuna mtu au watu unawaweka kwenye hatari kwani hao watu wanakuona kama mwokozi na mtetezi wa haki zao unapokosa ujasiri wa kuwatetea basi hukosa imani na wewe au kuangukia katika matatizo ambayo kama ungesimama imara kwa ujasiri ungeweza kuyaepusha.
Tunaishi maisha ambayo tumezungukwa na ndugu, jamaa, wapenzu, marafiki, wakwe, mashemeji, majirani na wengine wengi ambao kila mtu ana tabia yake mnaweza mkaishi kwa amani siku mbili siku ya tatu mnakuwa kama maadui, ni lazima tuwe jasiri na wenye misimamo ambayo itatusaidia kuishi na watu wa hulka tofauti hasa panapotokea tatizo ambalo kwa namna moja wao ndo chanzo, tumia msimamo wako ila hakikisha haki inapatikana kwa pande zote na sio kuegemea upande mmoja.
Angalia watu waliopo nyuma yako wanaotegemea ujasiri wako ili waweze kuishi kwa amani, wanakuangalia wakiamini kupitia msimamo wako matatizo yanayosababishwa na watu wanaowazunguka yanaweza kutatuliwa.
Kamwe usiogope kufanya maamuzi ili kulinda haki za watu wengine, kuna watu hawawezi kupambana ila hutumia mikwara kama njia ya kujilinda hivyo basi ukiogopa mikwara yao utajikuta umepigika na siku zote utakuwa mtu wa kuonewa kwasababu ya uoga wako, simama imara onesha msimamo wako ili wajue umejipanga lakini katika kufanya hayo yote zingatia heshima, kuwa na hekima pia busara, ustahimilivu,usiendeshwe na hisia au mihemko
Siku zote katika maisha unaweza usiwe na uwezo kifedha lakini hiyo hali isikufanye ukawa mwoga au ukakosa msimamo wa kutetea haki yako na wale waliopo nyuma yako, simama imara.
Najua yapo mengi ambayo umeyafanya kwa ujasiri na msimamo hatimaye hali ikawa shwari.Je, ni kitu gani cha kutetea haki katika familia au jamii yako uliwahi au umewahi kukifanya kwa ujasiri? Karibu utwambie ili tuweze kujifunza mwisho wa siku tuweze kuhamasika kuwa jasiri na kuuweka uoga pembeni kwa mstikabali wetu pamoja na wale waliopo nyuma yetu ambao wanaweza kuwa wazazi, watoto, rafiki, ndugu, na wengineo ambao wanatuangalia kama watetezi wao.