Ni kweli kabisa utaona kwa sasa ni rahisi kufanya biashara ukiuza online.Nchi nyingine hasa za Asia wamefanikiwa sana katika biashara ya kuuza vitu online kwa sababu ya uaminifu wao.
Kwa hapa Tanzania,tuna tatizo kubwa sana ambalo sina uhakika kama hata jamii inaliona kama tatizo.Suala la kutokuwa waaminifu.Suala la kutojali kumuumiza mtu mwingine kwa kumdhulum.
Hili lipo kwenye vizazi vyetu na ndio maana hata watu wanaoingia serikalini,asilimia kubwa ni wezi na wasio na huruma hata kidogo.
Kusema kweli kwa wengi halionekani kama ni tatizo.Ndio maana hata Dar inaitwa "bongo" bongo maana yake ni utapeli.Kutumia akili "siyo ya ubunifu katika vitu" bali akili ya kuwatumia "washamba" kujinufaisha.Kuwaliza watu ambao hawajaamka kujua dunia hii ni ya watu "makatili" Watu ambao nafsi zao bado zina dhamiri safi.Kuwaliza watu kama hao ndio inaonekana ujanja.
Kuna umuhimu wa suala hili kulifanya mjadala wa kitaifa.Watu wanaokuwa na tabia ya ujanja ujanja wa kiswahili,waonekane ni wabaya kwenye jamii,tofauti na sasa ambapo utapeli ni sifa njema.
Ukisikia Sinza kwa wajanja haimaanishi hawa watu ni wema.Maana yake ni wale wanaokuuzia vitu feki kwa bei ya vitu halisi.Ni wale wanaofeki hadi maisha yao ili waonekane wa mjini kuliko watu wengine.Ni pale utakuta watu wanauza miili yao hadi makaburini.Hizi ndizo sifa za "wajanja"
Ni muhimu tubadilike ili tusiwaogopeshe watu kutumia fursa ambayo dunia ndiyo inaitumia kwa sasa.Siyo mtu anaagiza mitumba gredi A,kisa kaagiza mtu wa Katavi,anatumiwa vitu vya hovyo gredi D.Tuweni waaminifu.Tumwogope Mungu