Ujangili wa programu na maendeleo ya teknohama nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujangili wa programu na maendeleo ya teknohama nchini

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Apr 20, 2011.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Miaka michache iliyopita tuliwahi kuwa na mazumzo na watu Fulani kuhusu Punguzo la Programu za komputa zinazotumika sana na Watu nchini haswa zile za Kampuni la Microsoft kama Microsoft Office , Microsoft Windows , Kampuni la Autodesk Kwenye AutoCAD na Adobe Kwenye Adobe CS pamoja na nyingine nyingi .
  Katika mazungumzo hayo kampuni hizo zilitaka kuwemo Sheria Mtandao na Nyingine za Hati miliki zitakazolinda Programu zao na wateja wao kwanza pindi watakapotumia Programu hizo au Kila Kampuni kuingia Mkataba maalumu na serikali utakaolinda maslahi ya Bidhaa zao nchini kwanza ndio masuala ya Bei na Punguzo nyingine kuongelewa .
  Kusema za ukweli uuzaji na usambazaji wa Programu na Leseni Bandia za Programu umechangia kudhoofisha sana maendeleo ya Teknohama nchini pamoja na kukuza misingi ya Wizi wa Milki ya Programu hizo pamoja na Leseni zake .
  Sasa hivi kuna watu wengi nchini haswa walio katika taasisi za elimu ya juu wana kosa fursa za kujifunza zaidi masuala mbalimbali ya teknohama kutokana na hali hii ya wizi wa Leseni za Programu mbalimbali na aina nyingine ya Hujuma za Kiteknohama .
  Kama umewahi kutembelea vyuo vikuu karibu vyote vya Tanzania na kuangalia aina ya programu wanazotumia kwenye shuguli zao za kila siku na komputa zao wanazitoa wapi na kama program hizo ni halali au batili ?
  Je wewe mwenyewe kwenye komputa unayotumia una programu ngapi ambazo si halali na batili au umezipata kupitia mfumo ambao sio sahihi ? labda leseni unayotumia kwenye program hiyo ni ya mtu mwingine ukaweka kwako kwa kujua au bila kujua ?
  Je unavyonunua programu kwenye maduka au sehemu zozote zile unajua haki zako za msingi ni zipi ? kama mtumiaji wa program husika je unapata haki zote kama Huduma kwa wateja , Updates Na Kadhalika ?
  Wiki hii kumetokea Tukio la Mzaha kidogo lakini la Maumivu sana kwa mfanyabiashara ambapo mfanyakazi mmoja aliiba Leseni/Keys/Product Keys za Progamu zinazouzwa na Kampuni hiyo kisha kwenda kuuza na zingine akaendelea kuwa nazo kwenye Laptop Yake .
  Mtu huyo amegundulika baada ya Mmoja ya watu kuuziwa Bidhaa hiyo kwa njia za kienyeji kuichomeka kwenye Mtandao na kugundulika imeuzwa wakati Risiti na Maelezo mengine Hakuna kwenye Hifadhi ya Kampuni .
  Ilivyogundulika hivyo mwenye kampuni ilibidi sasa awasiliane na Waliotengeneza Programu hiyo na kutoa leseni zake ili masuala mengine ya kisheria yaweze kuchukuliwa dhidi ya wale waliohusika .
  Watengenezaji wa Programu Walitaka kujua kuhusu Sheria Mtandao za Nchi yetu ( CYBERLAWS ) Zile za Hati Miliki na nyingine nyingi ambazo zingeweza kuwaongoza katika kufuatilia suala hili vizuri na kwa haki , hivyo vyote havikuwepo kwahiyo mfanyakazi aliachichwa kazi tu .
  Kwa kosa kama hili watengenezaji wa Programu hiyo wanaweza kuvunja mkataba wa usambazaji wa programu zao kwa nchi ya Tanzania kwa watu wanaopenda kuwa mawakala wa kuuza na kusambaza programu husika pamoja na kusitisha misaada mingine inayohusiana na masomo kwa mawakala wa kuuza na kusambaza programu zao
  Hilo ni moja ya matukio mengi yanayoendelea nchini ambayo yanasababisha Suala zima la Teknohama kuwa gumu katika maendeleo yake haswa yanapokuja masuala ya Biashara inayohusiana na Programu za Matumizi ya Kawaida ya Watu kama Uchoraji , Ujenzi na masuala mengine ya Uhandisi .
  Ndugu zangu jamaa na marafiki pale tunavyojitoa kwa dhati kupambana na Ufisadi na Hujuma nyingine dhidi ya Uchumi na Maisha yetu pia tupambane dhidi ya Ujangili wa Programu na Leseni Bandia Kwa Maslahi yetu .
  Serikali inakosa mapato makubwa kutokana na Watu kutonunua Programu hizi kupitia njia halali kwahiyo hawalipi kodi wala makato yoyote , Ajira nyingi zinapotezwa ambapo wale wanaomaliza mavyuo na mashuleni walitakiwa wawe sehemu ya mauzo na usambazaji wa program hizi au utoaji wa huduma kwa wateja .
  NA JE HAWA WANAFUNZI WANAOJIFUNZA MASUALA YA UTENGENEZAJI WA PROGRAMU KWENYE VYUO WATAKAA KWENYE SOKO GANI LA AJIRA KAMA MAMBO NDIO YAKO HIVI ?
   
 2. redSilverDog

  redSilverDog JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 486
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  daah! nitaisoma baade. Kama unaona utaandika ndefu atleast kuwa na pragraph, na pangilia vzuri. 2saidie 2naosoma..
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Shy ebu tambie wewe kwanza kama mtaaalam wa ICT kompyuta yako ina program gani unazotumia katika kazi zako na gharama yake jumla ni shilingi ngapi? Maana wewe sio mwanafunzi.?

  Alafu eleza kwa nini micorosoft bado wamewekeza china na USSR ambapo kuna ppiracy kubwa ya bidhaa zao na sio Tanzania kenya uganda ambapo ppiracy ni ndogo.?

  alafu endelea China na USSR zina cyber law nzuri sana kuliko Tanzania lakini kwa nn ujangili wa kompyuta bado upo?
   
 4. Blacksmith

  Blacksmith Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yang Shy,
  muda huu ni ulimwengu mpya kwani sasa tuna OpenSource software kwa ajili ya kazi zote kuanzia Drawings,Web Server,Web Design n.k. ambazo zina uwezo mkubwa tu na usalama zaidi.Ukizingati hali ya kiuchumi kwa taifa letu ni kusikitisha nadhani ilikuwa ni wakati wa kukumbatia hii aina mpya badala ya kupoteza fedha pasipo lazima, kwa mfano nchi za Ulaya (EU) zinatambua OpenSource Software na zinatilia changamoto matumizi yake mpaka maofisini.

  Je sisi watanzania tunauwezo kiasi gani ? kiasi cha kujifanya tunao uwezo wa kununua hizo product za mamia ya dollar.
   
 5. Osaba

  Osaba JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 1,720
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Window 7 ultimatum inauzwa software dola300 hadi 450 na cd moja ni kwa pc moja so kama una computer 10 unataka kufungua cafe na wewe unataka kufunga window 7 ginuine si ndio umeuwa mtaji wote?
   
 6. Blacksmith

  Blacksmith Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ubuntu ni free of charge inaweza kufanya yote ambayo unafikiria kufanya kwenye computer tatizo pekee ni uduni wa elimu yetu na tatizo la kutokutaka kujifunza kipya.

  kama mheshimiwa alivyogusia swala la Internet Cafe nadhani Opensource ingekuwa ni mwokozi kwani usingesumbuliwa na virus:shetani: kama inavyotokea kwenye windows
   
 7. redSilverDog

  redSilverDog JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 486
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kwani opensource maanake bure au uhuru?
   
 8. Blacksmith

  Blacksmith Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa unauliza nini hapo ndugu?

  unao uhuru wa kutumia bila malipo hivyoni bure
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  End user wangapi wanaojua kutumia ubuntu?
  Hata uko ulaya wenye elimu bado cafe zinatumia windows . may be na mac. Ni sababau ya interface. tumabiane ukweli interface ya ubuntu bado sio nzuri kama ya windows

  Unaweza kufukuza wateja kwa kuweka ubuntu kwenye cafe. Ubuntu ina kazi yake maalum. ubuntu hai na siobest na nzuri kwa graphics na media. na ubuntu sio tatizo kwa wataalamu lakini ni tatizo kwa end user. Unless itabidikwenye cafe uweke na wasadizi zaidi wa kuwasaidia wateja.
   
 10. redSilverDog

  redSilverDog JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 486
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  sio maanake! kama unataaka kujua uliza nikufahamishe...
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hizi gharama inatakiwa zilipwe na serikali na mashirika makubwa lakini user wadogo wadogo wa tanzania wasiingie gharama kama hizi. Microsoft wala hawana muda wa kumshtaki mtazamaji au mtazamaji internet cafe.

  Labda microsoft na wengineo wakitaka waazishe kitufe cha donate ili tukichakachua tuwarudishie chenji kidogo kwa donation
   
 12. Blacksmith

  Blacksmith Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jidanganye ndugu,
  A main principle and practice of open source software development is peer production by bartering and collaboration, with the end-product, source-material, "blueprints," and documentation available at no cost to the public.
   
 13. redSilverDog

  redSilverDog JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 486
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  sasa umecopy and paste sio? subiri inaonekana hilo neno "free" hujaeelewa.

  FREE SOFTWARE, SIO SAWA NA FREEWARE!
  OPENSOURCE inatoa FREE SOFTWARE!

  Bahati nzuri i attended one of Richard Stallman's talk! na nina signed book yake!!
   
 14. Blacksmith

  Blacksmith Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  So that makes you Pro! kwa kuwa una Signed book yake.
  nimekupata Professor.
   
 15. redSilverDog

  redSilverDog JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 486
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  so, the only thing u saw up there is the "signed book".. :A S-confused1:
   
 16. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Vile vile cha kuelewa hata iwe freeware au open source , offshelf , inhouse bado kuna some cost some indirectlly some directly
  People should read some articles on Total Cost of ownership.( TCO) Hii ni moja ya njia inayotumika kufanya evalution software au hata harware gani mtu atumie. One of the article ni hii Total cost of ownership - Wikipedia, the free encyclopedia

  Between Richard Stallman's talk! alisemaje ebu tudondoshee
   
 17. redSilverDog

  redSilverDog JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 486
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Richard Stallman alikuwa anaongea kuhusu danger ya software patents.. Vipi softwae watu wenye hizi wanvyoweza kuzia development ya new softwares. Coz ukitaka kutengeza tu, ushaanza kudistribute anatokea mtu anakwambia part ya ile software imo kwenye patent yake. Pia akaongelea kidogo kuhusu Free Software Movement, ambayo yeye anapenda kutenganisha na Open Source.
   
 18. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ok thanks nimeona clip zake youtube nitazingalia baadae. ngoja niende uswazi kucheki mechi
   
 19. Elly B

  Elly B JF-Expert Member

  #19
  May 2, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 1,194
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hili ni wazo la msingi haswa! Tatizo ni kuwa Hii nchi haijaanza kuwa serious na chochote. Kwa sasa tunataka kuona yale mambo ya msingi zaidi kama kuwapatia wananchi elimu bila madaraja na mipaka yanatekelezwa.Hatupendi kuona ndg zetu wagombania kanyagio za kuku(spidi)kila jioni bila kujua kuku ameliwa wapi na nani kamla! Tungefurahi kuona zahanati zenye madokta wazuri wanaolipwa vizuri zinajengwa zaidi ya sasa............................................................yako mengi haya. Usitegemee sheria za kusimamia software hum wakati sheria za kusimamia matumizi ya kodi za watoka jasho wa nchi hii hazijaeleweka.!
  Ukitaka hili litokee subiri aje "muwekezaji"atoe masharti hayo. Au aje mfanyabiashara maarufu aseme! Hizi ni lugha mbili zinazoeleweka haraka kwenye serikali hii mbovu isiyojali wananchi wala kesho yao.

  Mie nafikiri tuna safari ndefu bado kabla ya kufika huko unakosema. Kwa sasa ambapo kila mtu kivyake we acha watu waibe tu,ili hizo chechi chache zilizotakiwa kulipia software zilipwe ada na chakula,labda nyumba na huduma za afya.!Kwa kifupi ni kwamba hatujaweza kuanza kujali vya watu kabla hatujafikia kujali vyetu kwanza...hii unayiona sasa ni survival for the fitest katika mazingira haya tuliyonayo. Ni stuggle ya kuhakikisha na sisi tunakwenda na hiyo dunia ingawa tutakuwa kwa mbaaaali nyuma. Hii ndiyo tofauti ya mtu na Mbuzi........
  Until then mapambano yataendelea.Tukifikia kumaliza haya,tutaanza hayo.Vinginevyo hii ndiyo tafsiri ya kuwa na serikali isiyo na utawala wa sheria. KWA HIYO MI NAFIKIRI HIVI:
  "njoo kwanza huku tupiganie hii katiba mbovu itoke ili hii serikali mbovu itoke ili tuweke serikali ya wananchi inayojali wananchi ili haki zitendeke na sheria zifuatwe na wote kwa manufaa ya wote"

  Kama hujanielewa ni kuwa hatuna sheria ndani ya hii nchi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 20. mazd

  mazd Senior Member

  #20
  May 2, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wambie kaka, naona wanaanza kuleta theory za kutuandikisha makodi burebure--Myself am open-source developer.
   
Loading...