BATTO
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 282
- 207
Kama mnavyojua daladala zetu kutoka mjini mida ya jioni bila kutanua kigimbi utasimama mpaka kwenu...hii ilitokea jana kwenye daladala inayotokea posta kwenda makumbusho..madada wawili masista duu wa mjini baada yakupigana vikumbo mlangoni wakakuta kiti kimoja kimebaki zogo likaanza kila mmoja anasema kile kiti ni chake..
KONDA akaona isiwe tabu..jamani mnawapigia abiria wenzenu kelele..wale madada ndo kwanza wanasukumizana kugombania kiti..akarudia tena KONDA-jamani mimi nasema anayejiona MZEE zaidi ya mwenzake ndo akae..wale madada duu wakatazamana huku wote wakiwa wamesimama..
KONDA-jamani MZEE kati yenu ndo akae...wote kimya..basi kutoka posta mpaka makumbusho kile kiti hakijakaliwa na mtu wale madada duu wote wamesimama kila mmoja anajifanya kijana zaidi ya mwenzake...huku baadhi ya abiria wakimpongeza konda kwa busara aliyoitumia kuamua ugomvi...jamani ujana mtamu nyie usikieni tu.,