ujambazi CBA Nyerere Rd: Picha kamili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ujambazi CBA Nyerere Rd: Picha kamili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkurabitambo, Sep 7, 2012.

 1. M

  Mkurabitambo JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  WATU wanaodhaniwa
  kuwa ni majambazi
  wamevamia na kutumia
  mbinu za uhalifu wa
  hali ya juu na kupora
  magunia ya fedha
  kutoka Benki ya
  Biashara ya Afrika
  (CBA), iliyopo barabara
  ya Nyerere, jijini Dar es
  Salaam.
  Tukio hilo linaloweza
  kufananishwa na filamu
  za kimafia, lilitokea
  jana kati ya saa 2.30 na
  saa 2.45 asubuhi.
  Waliondoka na magunia
  hayo wakiwa
  wameyapakia kwenye
  magari yao ya kifahari,
  bila kuua wala kujeruhi
  mtu.
  Kamanda wa Polisi
  Kanda Maalum ya Dar
  es Salaam, Suleiman
  Kova alithibitisha tukio
  hilo na kusema fedha
  walizoiba zinakadiriwa
  kuwa zaidi ya Sh400
  milioni.
  “Hatufahamu kiasi
  kamili lakini,
  tulivyowahoji maofisa
  wa benki wanasema ni
  zaidi ya Sh400 milioni
  ambazo zimeibiwa,”
  alisema Kova.
  Alifafanua kwamba
  tayari meneja wa benki,
  msaidizi wake na mlinzi
  aliyekuwa zamu
  wanashikiliwa na polisi
  kwa ajili ya mahojiano.
  Mashuhuda
  Baadhi ya mashuhuda
  wa tukio hilo walisema
  watuhumiwa hao wa
  ujambazi, waliingia
  kwenye benki hiyo,
  huku wakiwa wamevalia
  vitambusho vya benki
  kujifafanisha na
  wafanyakazi wa benki
  hiyo, mbinu ambayo
  iliwahadaa watu
  waliokuwa kwenye eneo
  hilo wasishtuke kwa
  lolote.
  Vitambulisho hivyo
  viliwafanya walinzi wa
  benki hiyo kutokuwa na
  wasiwasi na
  watuhumiwa hao,
  jambo lilitoa fursa kwao
  kutekeleza uhalifu
  katika mazingira ya
  urahisi zaidi.
  Baada ya kuingia ndani
  ya benki, majambazi
  hao wakiwa na bastola
  yaliwaweka chini ya
  ulinzi walinzi wa benki
  hiyo .
  Wakati hayo yakitokea
  mmoja wa majambazi
  hao aliamuru
  wafanyakazi wa benki
  hiyo kuendelea
  kuwakaribisha wateja
  wao na kila aliyekuwa
  akiingia aliwekwa chini
  ya ulinzi.
  Mtuhumiwa mwingine
  wa ujambazi akiwa na
  bastola, alimfuata
  mtunza funguo wa
  chumba maalum cha
  kuhifadhia fedha na
  chumba cha Mashine za
  Kutolea Fedha (ATM) na
  kumwambia, atoe
  funguo.
  “Tena jambazi huyo
  alimtaja kwa jina
  mtunza funguo huku
  akisema naomba
  funguo za strong room
  tumekuja kuchukua
  fedha zetu,” alisema
  mmoja wa mashuhuda
  akimkariri jambazi huyo
  na kusema alipewa
  funguo bila kizuizi.
  Baadaye majambazi hao
  walifanikiwa kufungua
  kwenye vyumba hivyo
  na kuchukua fedha zote
  na, kuzihifadhi kwenye
  magunia manne.
  Wakati shughuli hiyo
  ikiendelea majambazi
  wengine waliharibu
  mitambo ya kamera
  zinazoonyesha watu
  wanaoingia na kutoka
  kwenye benki hiyo.
  “Tunajua mnaturekodi
  kwenye kamera zenu na
  sisi tunaifahamu vizuri
  teknolojia hii, ndiyo
  maana tunalazimika
  kuharibu mtandao
  mzima,” mmoja wa
  jambazi alikaririwa
  akisema huku akifungua
  mtambo wa kamera.
  Baada ya kumaliza
  kuharibu mitambo ya
  kamera, waliondoka na
  maguni ya fedha na
  kwenda walikoegesha
  magari yao ya kifahari
  na kupakia.
  Walioshuhudia
  walisema, majambazi
  hao walikuwa
  wakitumia magari
  matatu ya aina ya
  Toyota Land Cruiser,
  Nissan Patrol na Toyota
  Noah na kwamba,
  wakati wakitekeleza
  ujambazi huo madereva
  wote walikuwa
  wamebaki kwenye
  magari hayo yaliyokuwa
  yameegeshwa karibu na
  benki hiyo.
  Baada ya magari hayo
  kupakia magunia hayo,
  madereva hao
  waliyaondoa magari
  hayo kwa kasi kuelekea
  eneo la katikati ya jiji.
  Wameendelea kusema
  kwamba wakati
  majambazi hayo
  yanaondoka katika
  eneo hilo mnamo saa
  2.45 asubuhi, hakukuwa
  na msongamano wa
  magari katika barabara
  ya Nyerere kama
  kawaida.
  “Unafahamu muda huu
  eneo hili huwa na
  msongamano wa magari
  lakini, tunashangaa
  wakati tukio hili
  linatokea hakukuwa na
  magari hadi tukadhani
  labda kuna msafara wa
  viongozi,” alisema
  mmoja wa mashuhuda.
  Baada ya tukio hilo
  kumalizika maofisa wa
  Jeshi la Polisi walifika
  katika benki hiyo
  iliyopo kwenye jengo la
  Jamana wakiongozwa
  na Kamanda wa Kanda
  Maalum ya Mkoa wa
  Dar es Salaam,
  Suleiman Kova.
   
 2. awp

  awp JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  dili hilo
   
 3. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee babaangu jeshi la policcm wanajisahau sana ndio maana majambazi wana wana2mia mwanya huo kufanya uwalifu,,

  ngoja nikapate mbege
   
 4. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  wajomba wana technic kuliko kova na mwema
   
 5. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  wapo busy na chadema
   
 6. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Kuhusu camera za security, majambazi hao hawaelewi vizuri jinsi zinavyofanya kazi.

  Camera zinatuma picha zake moja kwa moja kwenye server na hata kama ukiharibu camera, bado wanaweza kupata picha zilizorekodiwa kabla ya kuharibu mitambo. Picha zote zinakuwa uploaded kwenye DriveHQ FTP server palepale zinapochukuliwa na zinabaki.

  "Even if an intruder destroys a security camera, he cannot destroy the recorded data, which can be immensely helpful for tracking down the intruder."
   
 7. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Hii lazima itainvolve mlolongo wa watu..kuanzia bank mpaka polisi.
   
 8. a

  abby Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa polisi wetu wangeambiwa ni CDM wameingia hapo mbona wangefika haraka sana!!!!!!!
   
 9. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Gud Shule. Thanks mkuu
   
 10. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  kama hawakuvaa ski mask kwa kujidanganya kuharibu camera basi imekula kwao...naipenda set it off starring jada,latipha na vivica fox i suppose
   
 11. f

  fakisi Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Trafiki watakuwa walisafisha njia (barabara) ili jamaa wapite, inawezekana vipi Nyerere ikawa empty saa 2:45 asubuhi halafu wanaelekea mjini!
   
 12. m

  mamajack JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  polis wako mapumzikoni wanasubiri kikwete awape amri ya kuua kwenye mikutano ya chadema.wanakula bata.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nchi inayoendelea hupiga hatua za maendeleo kwenye nyanja zote.
   
 14. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  ingekua ni chadema issue polisi. wote wangehamia cba hadi baba yao mkuu

  priorities differ
   
 15. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  nadhani hata Traffic aliyekuwa pale kwenye Taa (Banda la ngozi) anaweza kuwa alihusika kuyaryhusu magari ili njia iwe nyeupe kwa wazee wa kazi wapite
   
 16. n

  nganashee Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 2, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ata me nadaut
   
 17. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Polisi wamefacilitate zoezi la kuzuia magari ili watu wao wapite kirahisi hivyo polisi waliokuwa eneo hilo ni sharti wachunguzwa
   
 18. roby2006

  roby2006 JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 399
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mjini mipango
   
 19. m

  mdoe mchaina Senior Member

  #19
  Sep 7, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa kazi ya ile chopa ya polisi ni nini au ni kwa ajili ya mafuriko tu .kweli tuna safari ndefu kufika hakuna hata kituo kimoja cha televition chenye chopa .mambo kama haya tungekuwa tunayaona live .
   
 20. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Sio camera zote ndugu yangu! Camera nyingi huwa wanakusanya tapes na kuzipeleka kwenye back up houses. Ninachoshangaa ni kwamba hizo strong room imefunguliwa na mlango mmoja na haikuwa na combinations!
  What a weak security!
   
Loading...