Clever505
JF-Expert Member
- Jul 27, 2020
- 2,024
- 3,038
Mi siamini kabisa maneno ya Quran. Naona ni mashairi tu ya kutungwa. Sasa unapotetea mada kwa kuunga unga Aya za Biblia takatifu na Quran naona unaharibu tu point yako. Ndio maana tangu mwanzo nilikwambia usichanganye Aya za Biblia na Quran kwenye point moja.Taurati ni Sheria na hukumu Kwa ajili ya Wana wa Israel
Quran 17:2
Na tukampa Musa Kitabu, na tukakifanya uwongofu kwa Wana wa Israili. (Tukawambia): Msiwe na mtegemewa ila Mimi!
Na sio Taurati tu manabii wote waliotokana na kizazi Cha Isaka na Yakobo Hadi nabii wa mwisho ambaye ni Yesu walikuwa ni manabii Kwa ajili ya Wana wa Israel tu
Mungu anamfunulia Nabii Mika Ujio wa Yesu
Mika 4:2
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.
Yesu anathibisha kuwa utabiri wa nabii Mika upo sahihi na umetimia
Mathayo 15:24
Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
Quran ikaja kugongelea msumari kuwa Yesu alikuwa mtume Kwa ajili ya Wana wa Israel
Quran 61:6
Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati,
Manabii 3 hao Yani Mika , Yesu mwenyewe na Muhammad wote kauli zao zinafana kuwa Yesu ni mtume Kwa ajili ya Wana wa Israel
Manabii walioandikwa ndani ya Bibilia ni manabii waliyotoka katika kizazi Cha Ibrahim, Isaka na Yakobo lakini manabii walikuwa wengi katika miji mbalimbali ambao humo katika Bibilia hawapo Historia inasema manabii walikuwa zaidi ya laki 2
Na Ile miji ambayo haikupelekewa nabii kabisa hawakuadhibiwa na Wala hawataenda motoni Kwa sababu sio kosa lao
Kama ilivyo Kwa waliokufa wakiwa watoto au waliozaliwa machizi wataenda peponi haijalishi walikuwa katika uislam au ukristo au upagani
Pia Miungu alishasema hatawaadhibu watu ambao hakuwapelekea mtume
Quran 17:15
Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume.
Nina maswali mengi kinoma ila hebu turudi nyuma kidogo, ulisema Yesu ndo Isa. Kivipi Isa ni Yesu wakati ni watu ambao matendo yao ni tofauti.