Ukimya wa Serikali, hasa Kiongozi mkuu wa nchi ni jambo la hatari, inaonekana waliokuwa wakisema yu nyuma ya udini inadhihirika sasa. Kwa hakika amani ndio njia, iwe iwavyo kwa hatua hizi itafika wakati ambapo hata hao waonekanao kuwa sababu ya amani kwa kutokuwa wepesi wa hasira watachoka na hapo amani itakuwa historia iliyopita. Tuwe makini, tuchukue hatua maana hakuna kupona kwa kizazi hiki ikiwa ujinga huu wa kizandiki utaachwa uendelee.