Uingizaji wa magari nchini yaliyo chini ya Miaka 10. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uingizaji wa magari nchini yaliyo chini ya Miaka 10.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Borat69, Aug 16, 2012.

 1. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Jioni hii Waziri Mkuu ametamka bungeni ya kuwa Kama wabunge walio wengi wamepinga miaka(8) ya magari yanayoingia nchini,basi SERIKALI haitakuwa na kigugumizi kurudisha ile miaka (10) ya awali katika vigezo vya uingizaji wa magari nchini.

  Kwa kauli hii inaonekana SERIKALI huwa inakurupuka na kubadili vipengele bila ya kufanya tafiti na upembuzi yakinifu.
  Kuna Wananchi na uhakika watakuwa wamekumbwa na ushuru wa hali ya juu bila sababu za kimsingi.

  Kwa wale mnaojua naomba kupata uelewa hili suala la kuingiza magari yasiyo chini ya Miaka 10 litaanza kutekelezwa lini?

  Source: Bunge Via TBC.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Huyu pinda huyu...
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nchi hii mauzauza hayaishi,,hata ile ya miaka 8 nashangaa walishaanza kuitumia wakati kikao cha Bunge hakijaisha na kupitisha rasmi
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  "Watanzania ni waoga sana!! Mnaogopa nini"--Mbowe

  •Sasa angalia hyo gari ya 2005 bei yake kaka,mie nadhani wanataka wao ndio watembelee magari mzuri sisi tutembelee gari za 1985!
   
 5. d

  dkn Senior Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ulikuwa wizi wa hii serikali, nachojua baada ya bunge kupitisha budget mara moja hiyo sheria ya miaka 8 ikaanza 1st July. labda na uelewa mdogo, budget siyo finance bill au finance act ambayo TRA walichukulia ni rasmi.
   
 6. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo inaposhangaza!!! Ile ya miaka 8 ilianza kutekelezwa rasmi July 1st baada ya Serikali kupitia Wizara ya fedha kuamua hivyo. Ina maana kuna watu walipigwa za uso na hizo kodi za dharura bila kutoa muda maalum na wa kutosha kutekeleza hayo maamuzi.
  Inauma sana.
   
 7. howard

  howard Senior Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mimi nimepigwa za kichwa maana nimeingiza gari baada ya 1st july sasa sijui watarudishia au ndio imekula kwetu, bongo vituko
   
 8. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Hapo mkuu nafikiri itakuwa imekula kwako kaka. Kuanzia mwanzo hao TRA hawakuwa na mamlaka ya kutoza kodi mpya mpaka Bunge lihitimishwe na kupitisha taratibu na sheria mpya. Ila kwa kuwa WaTanzania tumezoea kuburuzwa na kuletewa mizengwe kwenye mambo ya msingi,haya mambo ni "Upepo tu yatapita" au "Liwalo na liwe".
   
 9. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  hivi wakuu kwa gari la cc chini ya 2000 saloon car ushuru ni asilimia ngapi wakuu naombeni msaada.lets say gari hadi nimeiagiza kutoka japani hadi hapo bandarini nimetumia dola 1800. je ushuru nitalipa kiasi gani gani na gharama zingine zote hadi itoke na iwe barabarani
   
 10. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Kitu cha muhimu pia ni gari ya mwaka gani? Halafu kwa hapo uliposema gari umetoa Japan mpaka hapa bandarini,usafirishaji(freight) tu itakugharimu Kama $ 1400 mpaka Dar..Ina maana hiyo gari utakuwa umenunua $ 400! Wanachofanya hawa wajanja (TRA) wanaangalia value ya hiyo gari mwaka iliyotoka ilikuwa ni bei gani. Halafu wanangilia invoice yako inasemaje. Baada ya hapo unapigwa 25% import duty, 20% excise duty, 5% chini ya CC 2000 na 10% juu ya CC 2000, 18% VAT. Ukipiga hesabu ndio ushuru utakaolipa. Na value ukiweka chini sana kwenye invoice TRA huwa wana-uplift kutokana na system zao.

  Port charges Tshs 255,000.
  Shipping Line $ 80.
  Kwenye ushuru ukipata figure ongeza hapo Tshs 350,000 ya Registration (Card ya gari).
  Tshs 40,000 ya vibao vya namba (number plates).

  Kila la heri mkuu.
   
 11. Jakowili

  Jakowili Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Duuh,wanatupiga sana za uso,ndg yangu ametuma Scania Tipper mende,ya mwaka 2000,ila nilichosikia tangu mwaka jana nikuwa magari kuanzia 7ton kuendelea yameondolewa ushuru kinacholipiwa ni 18percent vat tu,je kuna ukweli ukweli juu ya ili ama kuna malipo mengine yamejificha zaidi ya hapo,naomba ufafanuzi wako zaidi mtaalam,ninaitajika kulipia vitu gani zaidi?
   
 12. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  kapinda
   
 13. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nakushauri tu upate muda upitie website ta TRA. Mle utapata kila kitu.
   
 14. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Naomba ufafanuzi kwa wenye uzoefu maana nikipiga mahesabu kwa huu utaratibu mpya wa TRA naona kama gari ya over 10 years ushuru utakuwa kidogo kutokana na uchakavu mkubwa. Nipo sahihi wakuu?
   
Loading...