figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,197
- 64,634
Uingereza yavunja ukimya kuhusu hukumu ya Tundu Lissu, yataka haki na maridhiano
Kwako Wakili Msimiš¤£
====
Serikali ya Uingereza imeelezea wasiwasi wake kuhusu kuhukumiwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, na kuitaka Tanzania kuzingatia haki ya kupata usikilizwaji wa kesi kwa haki, maridhiano ya kisiasa, demokrasia na utawala wa sheria.
Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza, Waziri anayesimamia masuala ya Afrika na Maendeleo ya Kimataifa, Kirsty McNeill, amesema:
"Tuna wasiwasi mkubwa kufuatia kutiwa hatiani kwa kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Bw. Tundu Lissu, kwa mashtaka ya uchochezi."
Taarifa hiyo ya Serikali ya Uingereza aidha imesema:
"Tunarejelea matokeo ya Kikundi Kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu Uzuiliaji Holela (Maoni Na. 74/2025), ambacho kilihitimisha kuwa kuzuiliwa kwa Bw. Lissu kulikuwa kwa kiholela, hakukuwa na msingi wa kutosha wa kisheria, kuliambatana na wasiwasi mkubwa kuhusu haki ya kupata usikilizwaji wa kesi kwa haki, na kulikiuka ulinzi uliopo katika Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu pamoja na wajibu chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa, ambao Tanzania ni mwanachama wake."
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Tanzania ina wajibu wa kuheshimu sheria za kimataifa za haki za binadamu, ikiwemo kulinda haki ya kupata usikilizwaji wa kesi kwa haki, uhuru wa kujieleza, ushiriki wa kisiasa na kutendewa kwa usawa mbele ya sheria.
Aidha, Uingereza imesema inaunga mkono mtazamo wa Tume ya Rais ya Uchunguzi kwamba maridhiano ya kisiasa ni hatua muhimu katika kuponya majeraha yaliyosababishwa na vurugu zilizohusiana na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, pamoja na kurejesha amani, kuaminiana na mshikamano nchini.
"Tunatoa wito kwa mamlaka za Tanzania kuzingatia ahadi hii muhimu ya kufikia maridhiano, kukuza demokrasia ya vyama vingi, na kuzingatia kanuni za usikilizwaji wa kesi kwa haki, taratibu sahihi za kisheria, na utawala wa sheria," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Ijumaa, Novemba 6, 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania (Masjala Ndogo ya Dar es Salaam) ilimhukumu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, kifungo cha miaka minne jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la uchochezi.
Awali, Lissu alikuwa akikabiliwa na shtaka la uhaini kinyume na Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Jopo la majaji watatu lililoongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru lilimuachia huru katika shtaka hilo baada ya kubaini kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha bila kuacha shaka kuwa alikuwa na nia ya kutishia Serikali.
Hata hivyo, mahakama ilimkuta na hatia katika kosa la uchochezi na kumhukumu kifungo cha miaka minne jela.
Jumatatu, Novemba 9, 2026, uongozi wa CHADEMA kupitia wanasheria wake, akiwemo Dkt. Rugemeleza Nshala na Paul Kisabo, uliwasilisha taarifa ya nia ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Chama hicho kinasubiri nakala ya hukumu ili kuwasilisha sababu za rufaa pamoja na ombi la dhamana.
Pia unaweza kusoma: