Uingereza Kujadili mswada wa kujiua

Uingereza Kujadili mswada wa kujiua

Maserati

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2014
Posts
11,602
Reaction score
20,101
Bunge la uingereza lipo katika majadiliano ya haki ya kifo kwa mgonjwa ambae ataona ameugua sana na ugonjwa wake hauna dawa wala hawezi kupona, hivo mgonjwa ana haki ya kupata msaada wa kifo kutoka kwa madaktari ambao wata sign hati ya mgonjwa husika.
Unalionaje hili??

wana jf wote mnakaribishwa.

130603132556_house_of_lords_parliament_britain_640x360_ap_nocredit.jpg

Bunge la mabwana nchini Uingereza

Askofu mkuu wa zamani wa Cantebury Lord Carey amesema kuwa ataunga mkono sheria ambazo zitahalalisha watu wanaougua kupitia kiasi nchini Uingereza na Wales kupata usaidizi wa kujiua.
Katika taarifa yake ndani ya gazeti la Daily Mail Lord Carey ameondoa pingamizi yake dhidi ya mswada huo kufuatia hali inayowakumba watu wanaougua.

Lakini Askofu mkuu wa Cantebury anayehudumu kwa sasa Justin Welby ameutaja mswada huo kama ulio na makosa na hatari kubwa.

Wabunge wataujadili mswada huo siku ya ijumaa.
Mswada huo uliowasilishwa na mbunge wa chama cha leba Lord Falconer utawapa fursa watu wazima nchini Uingereza na Wales kupata usaidizi wa kujitoa uhai.

Fursa hiyo itashirikisha wale walio na chini ya miezi sita kuishi.
Madaktari wawili watalazimika kuthibitisha iwapo mgonjwa anaugua kupitia kiasi na kwamba wameafikia uamuzi wao wenyewe wa kujitoa uhai.

Takriban wabunge 110 wameorodheshwa kuzungumza wakati bunge litakapojadili mswada wa wanachama binafsi siku ya ijumaa.

Wakati Askofu Lord Carey alipokuwa Askofu mkuu wa Cantebury, alikuwa miongoni mwa watu waliopinga mswada wa Lord Joffes wa kuwasaidia wagonjwa wanaougua kupitia kisia kujitoa uhai ambao ulipingwa katika bunge la mabwana mnamo mwaka 2006.
Anasema kuwa inawezekana kuwa mcha mungu na vilevile kuwasaidia wale wanaotaka kujitoa uhai.

lakini katika taarifa yake hii leo katika gazeti la Daily Mail Lord Carey alisema ''ukweli ni kwamba nimebadilisha uamuzi wangu''.

Chanzo:BBC
 
Kibongo bongo hata waugueje sidhani kama kuna atakaetamani kufa!

ila itakuwa nzuri sana! tutapunguza gharama nyingi sana za uendeshaji kwa magnjwa yasiyoeleweka!

Please God grant us access to kill legally... not like boko haram and the alike..
 
Na her umejsema.sasa huo s utakupa u alqaida tena??
 
Heee ila kwa upande mwingine kunasaidia,japo binafsi naona bora mtu afe kwa muda wake na siyo kuuliwa na daktari,..
 
Duuu hapAna bwana hiyo ni dhambi iliyohalalishwa
 
Mmmmh... Hapo madaktari wenye roho za ibilisi watapata dili...

Mmh sidhani kama hii itakuwa njema, make ni kinyume cha maagizo ya Mwenyezi Mungu kwa imanj za kikristo!!
 
Last edited by a moderator:
Mmmmh... Hapo madaktari wenye roho za ibilisi watapata dili...

Mmh sidhani kama hii itakuwa njema, make ni kinyume cha maagizo ya Mwenyezi Mungu kwa imanj za kikristo!!

Umeona eeeeh twin wangu..n dhambi
 
Wamechelewa sana, hyo sheria ilitakiwa ije mapema sana
 
Kwa kuwa maisha yetu ni copy and paste toka kwa wazungu, hii lazima itakuja tu.Akyanani tutaanza na kingunge,we toka mim niko nasoma chekechea mpaka namaliza chuo ye bado yupo madarakani.Niko kazin kwa miaka 9,ye bado yuko madarakani.Nakwambia hakuna ugonjwa mbaya kwa binadamu kama huu wa "madarakarism".
 
nimefurahije?

sio ugonjwa usiotibika tu, hata ukishaona umezeeka vya kutosha, iwe haki mtu kutoa maisha yake. kwakweli sitaki kuzeeka hadi point mtu hujui kama unaExist. au point ya kusaidiwa chooni!!!!!

au hata mtu akiona hana interest ya maisha, iwe legal yeye kujiua kama hana watoto. kwanini tulazimishane kuishi?? throught my life I was just not interested in living!!! all common suicide methods just scared the devil out of me. lakini nilijua kuna dawa huko hospitalini zinaweza kunirestisha in peace.

Waingereza wamesikia kilio changu. Na Tanzania tutafika tu.
 
Huyo wa kuanza nae ndo umenfurahsha.ha ha ha ha ha. .
 
Mmmh. housegirl usje wekea sumu watu kwenye chakula...ha ha ha ha ha ha
 
Last edited by a moderator:
Mkuu sio Tanzania ni Uingereza au wewe ni mwimgereza?

Aaagh wap. Bulldog m'bongo huyo..but anasema hvo coz anajua hata kwa nchi zetu hyo must applicable. ..
 
Last edited by a moderator:
kuna faida gani ya kuuguza mgonjwa aliye kwenye comma kama Arial sharon?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom