Uingereza kufunga ubalozi wake mdogo Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uingereza kufunga ubalozi wake mdogo Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Sep 27, 2008.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Sep 27, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  UBALOZI mdogo wa Uingereza nchini unatarajia kufungwa Visiwani Zanzibar hivi karibuni kutokana na nchi hiyo kukabiliwa na ukata.
  Monday, 22 September 2008

  Akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na ubalozi huo kwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na viongozi mbalimbali wa kisiasa, kidini na kijamii, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Philip Parham, alisema kutokana na hali hiyo wamelazimika kufunga ubalozi wao, ingawa wangependelea kuwapo visiwani.

  Alisema tayari ubalozi huo umeamua kuuza jengo lake 'Hamerton House' ambalo ni la muda mrefu lililopo eneo la Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

  Balozi Parham alisema futari ya mwaka huu ndiyo itakuwa ya mwisho visiwani humo

  kutokana na ubalozi huo kuuza nyumba yao kunakotokana na ukata wa fedha wa nchi yake.

  ''Ni masikitiko yetu kama ambavyo baadhi yenu mnaweza kufahamu, kuwa futari hii itakuwa ya mwisho kabisa kufanyika katika nyumba hii ya Hamerton. Shinikizo la kifedha limetusukuma kuiuza nyumba hii,'' alisema Balozi Parham.

  Alisema ingawa wanafunga ubalozi wao, uhusiano wa nchi yake na Zanzibar utaendelea kuwapo.

  ''Hii haimaanishi kwamba serikali ya Uingereza sasa imeamua kupunguza uhusiano na Zanzibar,'' alisema Balozi huyo. Jengo hilo la kifahari linauzwa kwa Dola za Marekani 750,000.

  Balozi Parham alisema serikali ya Uingereza itaendelea kuipatia misaada mbalimbali kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Alisema Uingereza itajitahidi kusaidia kuhamasisha maendeleo ya kisiasa na kiuchumi viziwani Zanzibar, kwani zaidi ya Sh 11 bilioni zinakwenda katika Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

  Mapema Balozi alisifu ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Waislamu na waumini wa madhehebu mengine visiwani, kitendo ambacho kimezidi kuimarisha maelewano katika jamii.

  Alisema kitendo cha kukaa pamoja na kula futari kinawakumbusha watu jinsi wanavyomtegemea Mwenyezi Mungu bila kubaguana.

  Balozi huyo pia alizitaka Jumuiya za Kiislamu kuleta amani na mshikamano kwa Waislamu wote duniani na watu wasiokuwa Waislamu.

  Alisifu juhudi zinazofanywa na Mfalme wa Saudi Arabia, Sheihk Abdulla ambaye ni Imamu wa misikiti miwili mitakatifu ya Madina na Makka kuwaunganisha Waislamu wote duniani kuwa kitu kimoja.

  Katika hatua nyingine Balozi Parham aliwashangaza waumini wa kiislamu waliokwenda kufuturu aliposema kwamba, yeye anatoka katika ukoo wa Kiongozi wa Waislamu wote duniani Mtume Muhammad (SAW).

  ''Nina mfano binafsi jinsi tamaduni na maadili ya kiislamu na kikristo zilivyoingiliana kwa ukaribu kupitia kwa wahenga wa kihispania na mahalifa wa Ummayad wa Cordoba, mimi nimetoka kabila la Kureish, ukoo wa familia ya Mtume Muhammad (S.A.W) makureish ni mababu zangu wa mara hamsini na moja,” alisema Balozi huyo.

  Balozi Philip Parham alisema kwa kufuatia mstari huo huo wa mababu yeye pia ametokana na Mtakatifu wa Kikatoliki Elizabeth wa Ureno.

  Mgeni rasmi katika futari hiyo alikuwa Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, ambaye aliambatana na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha Mufti wa Zanzibar ,Sheikh Harith Bin Khelef, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Juma Duni Haji na mawaziri mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.


  Source: Salma Said, Mwananchi
   
 2. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Haya ndio matokeo ya bankruptcy of Lehman Brothers in action, matokeo yake ndio haya sasa tunaanza kuona taratibu taratibu taratibu...! Usischangae wakasema wanafunga na ubalozi wa Tanzania halafu wanfungue ubalozi mmoja tu kwa ajili ya Afrika mashariki ili kupunguza matumizi...!

   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ile ya Zenj ilikuwa ni ubalozi au rest house?
   
 4. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2008
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thank God at last they have gone
   
 5. s

  sumar Member

  #5
  Oct 6, 2008
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I don't think they should go like that only. Kwanza watupe uhuru wetu kamil. Walimkabizi nchi Nyerere, sasa watupe wenyewe. Wasijitoe kimasomaso.
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Oct 6, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Labda wamegundua kuwa ZNZ si Nchi, baada ya kusoma makabrasha yanayo husu muungano....! Mmmh! Ni mtazamo tu.
   
Loading...