Uhusiano wangu kimapenzi na 'Hamida' wangu

Uhusiano wangu kimapenzi na 'Hamida' wangu

JBourne59

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2020
Posts
952
Reaction score
8,863
Utangulizi.

'Mama watoto' aliridhia mimi kuandika simulizi hii kwa masharti makuu mawili. Moja nijitahidi kutoacha mlango / milango wazi itakayoruhusu watu kuunganisha dots...

Masharti mengine kwa kuwa ni sehemu ya codes, sintoyaeleza.

Hivyo katika simulizi hii nitaongeza 'chumvi' ama 'kuongeza maji' ili kuleta ladha kusudiwa.

Hamida ni mke wangu ambaye "hajaniacha "

Angalizo:
Picha ni kwa hisani ya "Google"
Haina uhusiano na simulizi hii.

Pia simulizi hii haina uhusiano na Hamida aliye-trend kwenye mitandao ja kijamii hivi karibuni.

Majina yote ya watu katika simulizi hii hayatokuwa halisi.

IMG-20200125-WA0000.jpeg

James Jason
 
SEHEMU YA KWANZA
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
...
"Hodiii!, hodi hodi humu ndani"

Nilibisha hodi huku nikigonga mlango kwa kutumia kipande cha chuma kilichoning'izwa maalum kwa ajili hiyo.

"Karibu, fungua mlango umeshindikwa tu"

Sauti nyororo ilisikika kutoka ndani.

"Starehe"

Nilijibu huku nikisukuma mlango mzito wa mbao ulio nakshiwa kwa ustadi mkubwa. (Neno 'starehe' enzi hizo ndio lilitumika kujibu pindi ubishapo hodi na kukaribishwa)

Nilipofungua mlango nikakutana na korido ndefu nyembamba (wakati huo iliitwa 'ukumbi' japo siyo kama kumbi tuzijuazo leo), pembeni kulia na kushoto kulikuwa milango, wa kushoto ulikuwa mpana ambapo ulikuwa wazi ukiwa umesitiriwa na pazia zuri jepesi lenye 'kuangaza' (transparent) la rangi nyeupe, upande wa kulia mlango ulikuwa umefungwa, na milango mingine mitatu pia ilikuwa imefungwa.

Mbele mwisho wa korido kulikuwa na mlango ambao ulikuwa wazi kiasi cha kuweza kuona nafasi kubwa iliyokuwepo na sehemu ya uzio wenyeji waliita uani (sikuhizi ukisema uani watu watajuwa ni maliwatoni)
************

"Karibu tupo huku varandani"
Ile sauti nyororo iliendelea kunikaribisha na sauti hiyo ilitokea upande ule wa pazia jepesi angavu ambapo nilivyoingia nikatambua kuwa pale palikuwa ndiyo sebuleni.

Kabla ya kuingia nilivua viatu vyangu (raba - Morogoro shoes), havikutoa harufu mbaya kwa kuwa ndiyo nimevivaa kwa mara ya kwanza baada ya kuvinunua, vilikiwa vya rangi ya bluu na soksi zangu nyeupe. Hapo mlangoni kulikuwa na viatu vya sandarusi vyenye ukubwa tofauti pea tatu... nikajuwa utaratibu wa kuingia humo ni pamoja na kuvua viatu.

Nilipekenyua pazia kulia na kushoto na kupiga hatua kuvuka kivingiti cha mlango na kukanyaga zulia zuri la manyoya manyoya.

Ndani niliwakuta wanawake wawili na mtoto mmoja mdogo wa chini ya miaka mitano. Wale wanawake mmoja alikuwa mwafrika, amejitanda vizuri ushungi huku akiwa ameshika ukili (alikuwa anasuka mkeka).

Wote walikuwa wamekaa chini na kuegemea mito midogo, hapakuwa na viti bali meza ndogo iliyo chinichini sana jirani na zulia.

Yule mwanamke wa pili alikuwa mweupe, asili ya Asia, na sikuweza kufahamu maramoja kama alikuwa Mwarabu ama Mhindi. Alikuwa anakoroga maji ya rangirangi akichanganya sukari na yale maji, bila shaka alikuwa anaandaa "ashkrim", watoto walikuwa wanaita hivyo. Zilikuwa zile "icecream" (malai) ambaozo maji huwekwa kwenye "kijikopo" kidogo kisha kuchomekwa kijiti cha chelewa ambapo maji yakiganda kile kijiti huwa ni sehemu ya kushika ashkrim hiyo.

"Karibu uketi"

Alisema yule mwanamke 'mwarabu' huku akiendelea na kazi yake.

Ndipo nikajuwa kuwa ile sauti nyororo ni ya huyo mama.

"HAMIDAAAA"

Aliita yule mama wa kiarabu.

Mara nikasikia sauti mlango fulani ukifunguliwa na kisha hatua za kivivu zikija upande wetu kutokea koridoni.

Pazia lilisogezwa pembeni akachungulia msichana aliye jitanda ushungi.

"Abee"
Yule binti aliitikia huku akimuangalia yule mama mkoroga malai.

"Hebu kamletee mgeni kinywaji"

Yule binti aliondoka bila kusema neno.

"Mzee Mjumbe nimemkuta?"

Niliuliza hivyo baada ya kuwasalimia kama ilivyo desturi na kujitambulisha.

"Tangia alivyoenda msikitini bado hajarudi, bila shaka atakuwa pale Shibam wanapocheza keram na zuna"

Alijibu yule mama huku ameinama akiendelea na kazi yake.
*************************

Michezo ya Keram, Zuna, Karata, Bao ilikuwa maarufu sana kwenye 'kijiwe' cha kahawa na tangawizi pale Shibam na sehemu nyingine jijini Dar es Salaam. Mambo na mipango mbalimbali ilijadiliwa hapo ikiwemo siasa, michezo nk.

Mara yule binti alirudi huku ameshika magi iliyojaa sharubati na mkono wa kushoto ameshika bilauli ya bati.

Alimimina ile togwa kwenye ile bilauli mbele yangu kisha akanipatia. Ilikuwa togwa ya mtama uliokobolewa na kutengenezwa kwa ustadi mkubwa.

Maeneo ya FAYA (fire brigade) hivi sasa, zamani palikuwa na mti wa muembe mkubwa ambapo palikuwa maarufu sana kwa biashara ya togwa hadi eneo hilo likapewa jina la "mwembe togwa"

Pia haikuwa ajabu kukuta sinia yenye maji iliyowekwa chupa za 'fanta' ndani mkiwa na togwa, imezibwa na kipande cha gazeti iliyokunjwa vema kwenye kila chupa, wengine waliweka chupa moja tu ama stuli iliyofunikwa kawa bila kitu ndani, wateja hutambua moja kwa moja kwamba hapo kuna biashara fulani.
**********************

Niliipokea ile bilauli na kuigigida (kuinywa kwa haraka) kwa nilikiwa nataka niondoke niwahi kupeleka ujumbe sehemu nyingine kwa kuwa hapo tayari niliwaachia moja ya barua nilizokuwa nazo.

Nilikuwa nina karatasi kadhaa (barua) za kuwasambazia wajumbe wa nyumba 'kumi kumi' (waliitwa hivyo) kutoka kwa Katibu Kata, Kata ya Magomeni...

Niliwaaga wale wenyeji mle sebuleni na kuanza kuondoka. Yule binti naye akachukuwa ile bilauli pekee na kuacha magi yenye togwa iliyobakia pale sebuleni...
***********

Wakati navaa viatu pale koridoni, Hamida (siyo jina lake halisi) naye akawa anakuja kutoka uani (siyo maliwatoni) huku ameshika bilauli nne mkononi...

Nikawa namuangalia huku nikiwa nafunga kamba za viatu. Mara ghafla mtandio ukateleza akabaki kichwa wazi...

Moyo ulinilipuka paa! Kwa kumuona Hamida vizuri waziwazi...

Aliinama haraka haraka na kuchukuwa mtandio wake lakini kwa bahati mbaya tena zile bilauli zikamponyoka na kuanguka sakafuni...

=
=
=
.......
****
Hivi ndivyo nilivyokutana na Hamida wangu...

Itaendelea!

James Jason
 
inasikitisha sana, jikaze tu mzee mapenzi yanaumiza sana
Haisikitishi, bali inafundisha na kuburudisha.

Mapenzi yanaumiza ukitendwa,
Mapenzi yanaumiza ukipenda usipopendwa, lakini mkipendana, hata soda moja ya 250ml mnaweza kunywa wawili (wewe na mpeziwo) na wote mkaridhika na kufurahia.

James Jason
 
Chumvi kwenye chai

Sent using simu mbovu
 
Dah kama sio mambo ya kula kimasihara hii simulizi tungeipata wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaitwa multiplier effect, bila ule uzi kweli huyu jamaa tusinge jua umahiri wake kwenye uandishi picha,

Jamaa ni mwandishi mzuri, halafu mjini hapo yupo kitambo

"James Jason," naomba tu hii isiwe na mwisho wa kusikitisha kama Ile ya Lindi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wanajua kuvaa uhusika sana kama Matt Damon, kafanya watu tuamini kua yeye ndio Jason Bourne.
Jeremy Renner alijitahidi kuvaa uhusika wa wa Jason ila watu hatukumuelewa. Ikibidi waandaaji wamrudishie Matt Damon.

NB. Maelezo haya hayana mahusiano na Uzi wa muhisika ila yametokana na ID na Avatar ya mtoa uzi
 
Mzee faza baharia wa toka kitambo nimesabskraibu tayari nasubiri muendelezo

Niko hapa nimetega nachukua notes
 
SEHEMU YA PILI
******************

Kabila langu ni Taturu, baba yangu alibahatika kufanya kazi na Padri fulani mkoa wa Singida, hivyo masikio yangu yalinusurika kutobolewa, mimi pamoja na mdogo wangu niliyemuachia ziwa.

Miezi kadhaa nikiwa nimerudi nchini kutoka masomoni Ulaya, nikiwa mwajiriwa wa RTC maarufu kama UGAWAJI enzi hizo (siyo TRC), nilimtafuta Rose (wa Lindi; stori yake ipo kwenye uzi wa kula tunda kimasihara), Rozi hakujibu barua zangu tangia nilipo kuwa Ulaya. Miaka mitano ilikuwa imeshapita sasa.

=

Rose nilimuacha Lindi na kurudi Dar es Salaam baada ya kuwa naye Lindi kwa uhusiano wa mapenzi motomoto ya miezi miwili. Nikiwa Dar tulikuwa tunawasiliana kama kawaida lakini sikupata bahati ya kuonana naye ana kwa ana hadi leo hii ninapoandika haya.

=

Nilikata tamaa ya kuendelea kumtafuta, kazi yangu nayo ilichangia kwa kuwa nilikuwa bize mno hususani baada ya kurudi masomoni na kupandishwa cheo...

Labda mchumba wake aliendeleza uhusiano wao na kumuoa, hivyo aliamua kukata mawasiliano, hii ndiyo dhana kuu niliyobaki nayo, nahisi mtoto wake wa kwanza ni damu yangu.
************************

James mimi nilikuwa "kiwembe" sana kabla ya kukutana na Rose, umri wa kuoa ulikuwa umeshafika hivyo nilidhani kwake Rose ningehitimisha useja.

Baada ya kukata tamaa niliamua kuendeleza wimbi la 'ubazazi', kutembea na kila binti mrembo niliyemtaka...

Uingereza 'sikutembea' hovyo, nilikuwa na girl friend mmoja tu mwanchuo mwenzangu aliyetokea Hispania, Sue Parterson. Miss Sue ndiye aliyenipatia kitabu "Frech Sex Art Manners" kilichoandikwa na G. Valensin, nilijifunza mengi lakini uhusiano wangu na binti Paterson haukuwa wa malengo ya mbali, hivyo niliachana naye miaka miwili kabla ya kurudi nchini (nilidumu yaye kwa miaka miwili na miezi tisa hivi) ambapo nilienda Kaskazini zaidi kuchukuwa post graduate diploma fulani.

Enzi hizo kabla ya kwenda Ulaya hususani Uingereza, kulikuwa na utaratibu wa kupata semina fupi pale British Council, kwa ajili ya kuwaweka sawa kukabiliana na mazingira ya huko. Nakumbuka pamoja na mambo mengine tulifundishwa kufunga tai [emoji1787] (japo nilikuwa najuwa kabla)

Nilivyorudi Tanzania, nikapewa nafasi nzuri katika RTC (Regional Trading Company), nikatumia kufahamika kwangu na umuhimu wangu kujipatia mabinti warembo kila uchao hadi siku hiyo moyo uliponilipuka kwa kumuona Hamida.
*************************************

Makatibu Kata walitusaidia sana katika kazi zetu, nikazoeana na Katibu kata mmoja ambaye alikuwa Kata ya Magomeni.

Kulikuwa na mkutano uliandaliwa kati ya Uongozi wa Kata na wajumbe wa nyumba kumi kumi kuhusiana na hali ya upatikanaji wa bidhaa katika mkoa.

Nchi ilikuwa imetoka vitani, (Tanzania vs Uganda), hali ya uchumi ilikuwa imeyumba hivyo wajumbe walitakiwa kuwaandaa waananchi katika mashina yao kukabiliana na hali inayoanza kujitokeza.

Mzee Katibu Kata rafiki yangu nilipomtembelea afisini kwake, (nyuma ya Hotel Travertine hivi sasa) ndipo akaniomba nimsambazie barua kwa baadhi ya wajumbe Magomeni Mapipa; alikuwa hajisikii vizuri (alikuwa ana homa)

Magomeni Mapipa enzi hizo palikuwa maarufu sana, hapo ndipo kulikuwa na U-turn kubwa kwa ajili ya magari aina ya 'Ikarus' kugeuzia.

Mabasi haya pamoja na mabasi mengine yalikuwa yanamilikiwa na Shirika la UDA (Usafiri Dar es Salaam) ambapo walikuwa na mabasi yaliyotengenezwa na kampuni mbalimbali ikiwemo Mercides Benz (German), Isuzu (Japan), Ikarus (Hungary) nk.

Wanafunzi walikuwa wanapenda sana kupanda Ikarus, na waliyaita "ikarus kumbakumba" maana likija moja lilikuwa linapakia abiria wengi kwa mara moja. Mfano wake ni kama haya mabasi ya Kichina ya BRT yale marefu.
*****************************

Wakati nimechuchumaa nafunga viatu kamba huku nikimuangalia Hamida akiwa ameinama kuokota mtandio wake pamoja na bilauli zile, yule mama mwenye sauti nyororo nikimsikia akisema " Kwema huko?, taratibu mnatushtua na presha hizi..."

"Ziliniponyoka, ngoja nikazisuuze tena nizilete"

Hamida alijibu, nikaisikia sauti yake nyororo akiongea sentesi nzima.

Maa shaa Allah kumbe naye ana sauti kama ya yule mama Mwarabu.

"Kwaheri Hamida"

Nilijikuta nimeropoka huku nikirudi kinyumenyume kuelekea mlango wa kutokea nje. Hamida hakujibu kitu, aliinama na kugeuka akaelekea uani (siyo maliwatoni), mtandio alijifunika kichwani lakini kwa kuutupia tu.

Niligeuka na kuvuta mlango kwa ndani na kutoka nje.
***********

Mzee Burhani ni mjumbe wa nyumba kumi katika mtaa huo nilipotoka, ni mzee kwenye hekima na mcheshi sana, muislamu safi na mwenye kuipenda familia yake na jamii aiongozayo kwa ujumla.

"Salama leko"

Nilisalimia kama waislamu wanavyosalimia, waliitikia lakini mzee mmoja wa makamo akaniambia, wewe James inabidi ujifunze kusalimia vizuri...

Hatusemi salama leko bali tunasema Assalaam aleikum. Pale pale nikarudia

"Assalaam aleikum"
Wakaitikia tena kwa wingi.

"Inabidi usilimu kijana."
Mzee Burhani alidakia.

"Hahhaha" nilicheka, kisha nikamwambia kuwa ule ulikuwa ni 'mguu wake'

Kwakuwa haikuwa siri nilimueleza kuwa nilipitia nyumbani kwake na kuacha barua na kumpa yaliyo ndani kwa ufupi, kisha nami nikajisogeza kwenye benchi nikaketi huku nikiangalia wanavyocheza keram.
_____

Itaendelea...

Hii kitu kuanzia kwenye meli, mpaka Lindi, mpaka Uingereza, mpaka hapa Magomeni kwa akina "Hamida", ingekuwa kwa wenzetu huko yaani ingetengenezwa bonge la series fulani.
Mkuu am enjoying it sana, ukizingatia na uandishi wako nao ni superb.
Tafadhali fikisha salamu na shukrani nyingi kwa shemeji yangu "Hamida".
Mimi ni mdogo wako kiumri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu JBourne59 hii stori yako ni nzuri, ni burudishi na yenye mafunzo tele. Kwa sababu ilianzia kwenye jukwaa la Mapenzi, Mahusiano na Urafiki, na pia inahusiana na mambo hayo, nilikua nashauri uiweke kwenye jukwaa lile (MMU) ili wadau wengi zaidi wa MMU wafaidi.

Pia itakua ni namna bora zaidi ya kumuenzi rikiboy kwa uzi wake kuzaa simulizi hii mujarab na pia kumuenzi baharia mwanafunzi (yule wa bao 23, ambazo kumbe zote ni offside).

Vinginevyo nimetega macho na masikio kwa ajili ya kujifunza na kuburudika na simulizi hii mwanana...
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom