Uhusiano wa Franco na Mobutu

Kuna bendi nyingi zilijaribu kupiga na kuimba na kujizolea mashabiki wengi ndani na nje ya Afrika lakini bado Tp OK Jazz ilikuwa mbele tu
 
Kuna bendi nyingi zilijaribu kupiga na kuimba na kujizolea mashabiki wengi ndani na nje ya Afrika lakini bado Tp OK Jazz ilikuwa mbele tu
Kwangu mimi TP OK Jazz haitatokea tena. Ilikuwa bendi ya aina. Leo Simaro anatimiza 80 years-probably mtunzi bora kupita wote DRC.
 
Tp OK ilikuwa shule tosha,
Na sidhani kama ilikuwa rahisi kwa muimbaji kuingia bila kupita kwenye mahojiano ya kina.

Wengi walikuwa wataalamu wa sauti na upigaji wa vyombo,
Kuna ala sijawahi kuzisikia kokote kwenye bendi za Afrika ama nje ya bara letu tofauti na Tp OK Jazz tu.
 
Kwangu mimi TP OK Jazz haitatokea tena. Ilikuwa bendi ya aina. Leo Simaro anatimiza 80 years-probably mtunzi bora kupita wote DRC.
Zaiko langa langa,
Afrisa International,
Sokous stars,
Loketo,
Veve, orc kiam,
Mangelepa,
Wenge musica bcbg,
Extra musical,
Wenge el Paris,
For stars,
African all Stars,
Bella Bella,
Bokello Isenge,
Victoria Eleyson,
Lipua lipua,
Empire Bakuba nk zilikuwa juu kila moja kwa wakati wake lakini Tp OK ilikuwa juu siku zote.
 


Asante sana mkuu kwa kumbukizi muruwa kabisa. Inaelekea Madilu ni alikuwa anatembelea sana nyota ya Franco baada ya kifo chake maana naona karibu nyimbo kadhaa za Franco kazifanyia remix. Naomba baadae utuwekee uhusiano wa hawa jamaa wawili Madilu na Franco. Na vp kuhusu Tabu ley na Mbiliabel nao walikuwa na mahusiano gani ya kimuziki na Franco.
 
Hicho ulichokieleza nimekielezea vizuri kwenye comments zangu zilizofuatia ukizipitia utaona,na hakuna mahali nimesema Tabu ley alikuwa ok jazz
Mkuu nilikuwa nakazia kile ulichokisema kwani kuna wengine walifikira tofauti na ndo maana umekula like. Pole kama haikuja kwa maudhui hayo.
 
Reactions: OTG
Kuna ndugu yangu mmoja alikuwa anapenda kujiita Franco Luambo Makiadi. Wakati huo nikiwa bado mdogo nikienda kumtembelea nilifurahia sana vituko vyake,alikuwa anajisahau na hata kujitambulisha kwa jina hilo alipotakiwa.

Alifanana tabia na Franco kwa kila kitu.

Enzi hizo kulikuwa na furaha za kweli. Nimemiss sana nyakati hizo
 
Madilu System alikuwa mwanamuziki wa Afrisa International ya Tabou Ley, ilipofika safari ya kwenda ulaya akachujwa kwa mizengwe akiwa Airport. Akaona enough is enough akaomba kujiunga na OK Jazz na Franco hakuwa na hiyana. Akawa mwimbaji pamoja na waimbaji vinara wa OK Jazz- Josky, Ntessa na wengineo. Alifanya hivyo kwa miaka takribani 2/3. Ilipotokea safari ya ulaya dakika ya mwisho akapata namba. Franco wakati huo ndo amemaliza project yake ya "Lisanga ya Banganga" ambayo ilitoa santuri si chini ya 6 akiwa na Tabou Ley, Mavatiku Vissi na Josky Kiambukuta. Akiwa huko ulaya akapata idea ya wimbo wa Non au "Libala oh Libala 1982/83. Akamjaribu Madilu kama ataweza kuuimba. Baada ya kuelekezana ndo mwimbo ule ukasukwa na madilu akapiga duet na Franco na pia kuimba solo vipande vingine. Sauti ya Madilu ikapaa na OK Jazz wakaonekana wamekuja vipya-Franco akanogewa ndo akawa anatunga nyimbo za style ile (pamoja na Mamouu, Mario etc). Hapo Madilu ndipo alipopanda chati hadi kufikia 1986 Josky na Ntessa wakazira kwani waliona Franco macho yake yako kwa Madillu tu. Wakatoka OK Jazz wakatoa nyimbo kama Selengina. Ntessa alirudi kwa style ya Collaboration na OK Jazz (Album kama mbili), Josky alijiunga tena na kuongoza kikosi cha waimbaji wa OK Jazz. Baada ya kutokuelewana kati ya Familia ya Franco (Dada Yake) na Papa Simaro Lutumba 1993 Familia wakamvua Simaro uongozi, ndipo wanamuziki wote wakaiacha OK Jazz wengi wao wakianzisha Bana OK chini ya uongozi wa Simaro. Madilu akaamua kwenda solo, lakini akahakikisha mdundo wake na karibu nyimbo zake zinafuata beat ya OK Jazz na Solo ya Luambo. Alijitahidi pia akajenga bendi yake Bana Syste ambayo ukisikiliza album zake utaona role model wake ni Luambo. Si tu alitembelea nyota ya Franco bali aliishi muziki wa Odemba (style ya OK Jazz). Mwenyewe alidai kila anapoingia studio-anamuona Luambo kazini akimwongoza. Ndogo ndogo inasema mama wa Madilu ni dada wa mke wa Simaro (Maman Kelani).
 


Duuuuh,asante sana mkuu. I salute you. Najiona kama nipo ukumbini nawaona wakongwe wakifanya yao enzi hizo muziki umeshika hatamu. Kuna haja ya kuwa na jukwaa letu la kupeana mavitu ya enzi hizo kma haya.
 
madiluu kafundshwa mzk na luambo makiadi,na walikuwa pmj ktk band ya okk jazz hadi akifariki madilu akachukua usukani
tabu ley alimuoa mbiliabel mwaka 1987 na wakafunga ndoa kwenye ndege japo ndoa yao haikudumu
 
Mkuu nilikuwa nakazia kile ulichokisema kwani kuna wengine walifikira tofauti na ndo maana umekula like. Pole kama haikuja kwa maudhui hayo.
mkuu ID yako imenikumbusha mwanamzk wa okk jazz alieitwa simaro lutumba masiya
alicharaza wimbo matata unaitwa Maya
 
ukweli mtupu
 
umechambua vizur kwel hongera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…