Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 12,897
- 20,190
Kuna baadhi yetu tumekuwa tukihusisha watu masikini kwamba ni wavivu, huenda hii ilikuwa kweli zama za kale za kuhitaji nguvu na jitahada za kulima ili upate mkate wako wa kila siku (sababu hata uwindaji huenda ulihitaji ujuzi zaidi kuliko uchapakazi); Pia huenda kipindi hicho mtu alikuwa na watoto wengi sana na kuwafanya vijakazi wake au hata watumwa wa kumfanyia kazi (Tujiulize hapo mvivu alikuwa nani)?
Na Mfalme Je, alikuwa mwerevu, mvivu au utajiri wake ulitokana na faida ya kuzaliwa na wazazi fulani? Je angezaliwa na wazazi masikini asingekuwa mchapakazi au huenda angefanikiwa zaidi kwa kufanya mapinduzi, au angekuwa mbishi na ubishi wake ungepelekea maisha yake kuwa mafupi?
Unaweza kusema kwamba masikini wengi huenda ni wavivu wa kufikiri (tukichukulia watumwa, wengi waliofikiri huenda fikra zao ndio zilikuwa mwisho wa maisha yao); na hii leo hawa chawa wanaokula kwa kukosa principles unaweza kuwaweka katika kundi gani? Na matapeli je?
Je ni kweli leo uchapakazi unalipa? Je ni kweli matajiri wanafanya kazi kuliko masikini au wanacheza na system iliyopo (ni werevu wa kupambana na system) au wanadiriki kupitia njia za mikato ili kupata utajiri wao?
Je mimi nikiwa mwerevu/mjanja na sioni faida ya (inefficiency) kwa kutumia jembe la mkono, au kulima mwenyewe na kuwatafuta watu wanilimie ili mwisho wa siku nipate kingi ni mvivu? Sababu huenda wanaolima wanafanya kazi kuliko mimi lakini sidhani kama ni vema kuwaita hao ni wavivu (wavivu wa fikra maybe, lakini huenda wamekosa mtaji - au wamekwama kwenye poverty cycle)
Je wale ambao wapo kwenye Poverty Cycle sababu hawana ajira yenye ujira (ingawa wamepewa ujuzi), hawana kasehemu ka kulima na wakilima hakuna soko; wakiomba tenda hawapewi sababu hawana connection - ni vipi watatoka kwenye umasikini na je ni vema kuwaita hawa wavivu; huenda wamekata tamaa na sio vipofu kuona kwamba chochote wanachofanya ni Rat Race.
Ofcource kuna wazembe na Wavivu lakini sio masikini wote ni wavivu (wengi ni wachapakazi) na sio Matajiri wote ni wachapakazi..., wengi hata hawahitaji kuchapa kazi. (the system works for them)
Tujikumbushe alivyosema Confucius; In a country well governed, poverty is something to be ashamed of. In a country badly governed, wealth is something to be ashamed of.