Uhusiano kati ya midori na vioja ndani ya nyumba

Habari wakuu
Kumekuwa na kawaida katika nyumba mbalimbali iwe masebuleni au vyumbani midori ikionekana imesheheni, baadhi hupamba midori katika meza na makabati, wengine huthubutu hata kuwa na midori vitandani au katika viti (sofa) ikiwa lengo ni kukufanya ujisikie raha fulani hivi unapoongea na ndugu, jamaa au marafiki pale unapomshikashika huyo mdori iwe kwa kumvuta sikio, ulimi ama mkia, na kila mtu huwa na upendeleo wa aina ya mdori kuwa nao ndani baadhi hupenda midori ya ndege mbalimbali mpaka bundi,na midori ya wanyama mpaka fisi.

KISA: Wiki iliyopita jirani yangu alipatwa na sintofahamu yenye ushabiihano na midori,ilifikia wakati akilala husikia kama vitu vinacheza cheza sebuleni,mara chakula kuliwa na asiyejulikana n.k.

Siku moja akaamua kuchungulia akiwa ametoka chumbani na kuiona midori ipo bize na kuruka ruka,alipojitokeza sebuleni midori yote ilirejea sehemu yake.

Alipoirudisha midori hiyo alikoinunua ndio ukawa mwisho wa tatizo.

Naomba kujuzwa kuna uhusiano gani kati ya midori na mauzauza hayo.
Kuweni makini na midoli nyumbani! Acha kabisa kumpa mtoto wako uchafu huu! Choma moto midoli yote nyumbani haraka! Choma moto picha za wasanii na wananichezo kwenye kuta za nyumba yako!
 

JE UNAJUA KUWA MIDOLI UNAYOIJAZA NYUMBANI KWAKO INA MAJINI NDANI YAKE?​

Natumai uko salama ndugu msomaji na leo nataka nikujuze kuhusu midoli ambayo wengi huipenda kuwanunulia watoto wao,au kuijaza ndani kama mapambo


kwanza kabisa ndiyo maana hata mjumbe wa Mwneyez Mungu Mtume Muhammad s.a.w alikataza watu wasiweke midoli majumbani mwao pana hekima kubwa sana hapa isiyojulikana'

Mapepo/majini wao ni roho ambazo zinaweza kujigeuza na kuingia kwenye mwili wowote wanaoupenda na ndyo maana binadamu wengi pia huingiwa na majini hao,sasa miongoni mwa vitu ambayo majini hupenda kuingia kwenye maumbo hayo ni midoli, mapepo hupenda kukaa ndani ya misanamu na kufanya huo kama mwili na makazi yake.

ukitaka kuamini haya ninayoyasema kwa kujionea mweneyewe kwa macho yako fanya hivi

uwe unachukua mdoli wako na uwe unaliambia maneno haya huku unalitazama kwenye macho yake kwa siku 41 mfululizo utaona maajabu makubwa sana na usije ukashangaa unaihama nyumba kwa hofu.


sema maneno haya ''wewe blodmeli nibadilishie kinyago hiki''


ONYO
KAMA NI MUOGA,UNA MAGONJWA KM PRESHA,WASIWASI,NK USIJARIBU




Nasema haiwezekani kifaa kitengenezwe kwa mbao au plastic useme eti ina shida?

Majini, Shetani na Binadamu ni Roho/Nafsi wakati hiyo midoli ni vifaa vinatengenezwa kwa material ya kawaida tu

Tulichokatazwa kwa Waislam na Wakristo ni KUABUDU au KUSUJUDIA HIZO SANAMU NA MIDOLI BADALA YA MUNGU PEKEE

Hivi vingine mnavyotuletea ni Uongo na Uzushi.
 
Nasema haiwezekani kifaa kitengenezwe kwa mbao au plastic useme eti ina shida?

Majini, Shetani na Binadamu ni Roho/Nafsi wakati hiyo midoli ni vifaa vinatengenezwa kwa material ya kawaida tu

Tulichokatazwa kwa Waislam na Wakristo ni KUABUDU au KUSUJUDIA HIZO SANAMU NA MIDOLI BADALA YA MUNGU PEKEE

Hivi vingine mnavyotuletea ni Uongo na Uzushi.
Hayaja kukuta wewe bado mdogo kwa mambo ya elimu ya giza. Laiti yangelikukuta siku moja ungepata kuamini Tafuta Mdoli wowote uliopo nyumbani kwako kisha ushike na kusema maneno haya kila siku sema maneno haya ''wewe blodmeli nibadilishie kinyago hiki'' kwa siku 41 halafu njoo hapa ulete mrejsho wako usije kuikimbia nyumba unayoishi.
 
Kuna mwalimu fulani hivi wa injili nilisikiliza mahubiri yake miaka ya nyuma,aliwahi kuonya kuwa tuwe makini na midori pamoja na sanamu tunazonunua na kuziweka kama mapambo majumbani mwetu,alisema kuna zingine huwa zimebebeshwa roho fulani,alitoa mfano wa familia moja ilikuwa imenunua sanamu fulani hivi nje ya nchi na wakaipamba sebuleni kwao,basi nuksi za magonvi na kuugua kwa sana hazikuwa mbali nao,mpaka kuna siku baba mwenye nyumba akaishuku sanamu hiyo kuwa kinaweza kuwavm ndicho chanzo akaamua kuiondoa hiyo sanamu hapo nyumbani kwao na kwenda kuichoma moto mbali huko karibu na mto,kikiendelea kumnukuu mwalimu huyo wa injili alimalizia kusema m,huo ukawa ni mwisho wa hayo matatizo katika hiyo familia.
Wasio amini katika ulimwengu wa roho wanapata shida sana kukuelewa.
 
Unanikumbusha zile movies za anabelle....Kuna anabelle comes home, anabelle, anabelle creation, hizi three anabelle unakutana na madude ya ajabu, midoli na visanamu vina roho chafu na za kutisha zinasumbua nyumba unaishi Kwa hofu kwelikweli, ka mdoli kapo ukutani unatoka unarudi ndani mdoli anatabasamu, mara hayupo unasikia kelele chooni au kanacheka huko downstairs, mara mdoli amekunja miguu yaani ni tabu tupu nilifanya utafiti binafsi baada ya kuona hizo movies na zile za conjuring movies haya mambo yapo na Wala siyo kama mtu kachanganyikiwa, nilidhani ni movies ila kumbe yapo haya ukifuatilia au kufanya ka utafiti kadogo tu.
 
@eng.zezudu @vocalfremitus MIN-me mpandaone fuatisheni formular ya @herbalistdrmzizimkavu "WEWE BLODMELI NIBADILISHIE KINYAGO HIKI" kwa siku 41 huenda kuunywea mkate uzi huu,ubishi,kutoamini yasionekana kwa macho ya kawaida kutawatoka,nadhani mtakuwa mashahidi wazuri hapo mbeleni.
DUNIA INA MAMBO YA KUSTAJABISHA
 
Hayaja kukuta wewe bado mdogo kwa mambo ya elimu ya giza. Laiti yangelikukuta siku moja ungepata kuamini Tafuta Mdoli wowote uliopo nyumbani kwako kisha ushike na kusema maneno haya kila siku sema maneno haya ''wewe blodmeli nibadilishie kinyago hiki'' kwa siku 41 halafu njoo hapa ulete mrejsho wako usije kuikimbia nyumba unayoishi.
Hahahaha...hivi vituko na ujinga sijui mtaacha lini

Mimi ndio napaswa kukuuliza umri wako kwanza
 
Back
Top Bottom