Panctuality
JF-Expert Member
- Jun 11, 2019
- 726
- 1,044
Habari wakuu
Kumekuwa na kawaida katika nyumba mbalimbali iwe masebuleni au vyumbani midori ikionekana imesheheni, baadhi hupamba midori katika meza na makabati, wengine huthubutu hata kuwa na midori vitandani au katika viti (sofa) ikiwa lengo ni kukufanya ujisikie raha fulani hivi unapoongea na ndugu, jamaa au marafiki pale unapomshikashika huyo mdori iwe kwa kumvuta sikio, ulimi ama mkia, na kila mtu huwa na upendeleo wa aina ya mdori kuwa nao ndani baadhi hupenda midori ya ndege mbalimbali mpaka bundi,na midori ya wanyama mpaka fisi.
KISA: Wiki iliyopita jirani yangu alipatwa na sintofahamu yenye ushabiihano na midori,ilifikia wakati akilala husikia kama vitu vinacheza cheza sebuleni,mara chakula kuliwa na asiyejulikana n.k.
Siku moja akaamua kuchungulia akiwa ametoka chumbani na kuiona midori ipo bize na kuruka ruka,alipojitokeza sebuleni midori yote ilirejea sehemu yake.
Alipoirudisha midori hiyo alikoinunua ndio ukawa mwisho wa tatizo.
Naomba kujuzwa kuna uhusiano gani kati ya midori na mauzauza hayo.