Uhusiano kati ya kodi na shughuli za Maendeleo

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,542
3,451
Kuna uhusiano mkubwa kati ya kodi na shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali.

"Tunapotaka Serikali ifanye shughuli zaidi za maendeleo kwa fedha tunataka Serikali itumie fedha zaidi. Na kama Serikali haina fedha zaidi tunataka izipate, yaani iongeze kodi (Nyerere, 1968, uk. 20) "

Ukitaka Serikali ifanye shughuli nyingi za maendeleo zinazohitaji fedha bila kukubali kodi ni sawa na kuitaka serikali ifanye miujiza. "ni sawa na kudai maziwa zaidi bila kutaka ng'ombe akamuliwe tena"

Serikali ya awamu ya kwanza pamoja na kutambua umuhimu wa kodi kwa maendeleo katika kitabu hiki cha Ujamaa inatamka waziwazi kuwa ilitambua ugumu wa kuongeza kodi kutokana na kutambua kuwa watu hawana fedha zaidi.

Awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeyaonana madhila wanayoyapata walipa kodi wa Tanzania na kutaka utaratibu mzuri wa ukusanyaji kodi uzingatiwe.

Kupitia nafasi hii ni vizuri viongozi wetu wakazingatia utaratibu wa kodi rafiki. Kodi rafiki ina sifa nne zifuatazo;

(i) Urahisi (simplicity). Sheria za kodi zinapaswa kueleweka au kufahamika kwa urahisi kwa walipaji. Sheria hizi hazipaswi kufahamika kwa watawala tu ila jamii pia inapaswa kuzielewa kwa namna rahisi itakayosaidia utekelezaji.

(ii) Ufanisi (efficiency); Mamlaka husika inapaswa kuwa a uwezo wa kukusanya kodi bila kutumia gharama ya muda mwingi,na fedha. Kwa kifupi hapa mamlaka zinazohusika na ukusanyaji kodi zinapaswa kuhakikisha zinaweka mfumo ambao hautazifanya kutumia nguvu kubwa kukusanya kodi.

(iii) Uhakika(certainty) . Walipa kodi wanapaswa kuelewa muda wa kulipa kodi, kiasi cha kodi wanazopaswa kulipa na namna ya kulipa kodi hizo.

(iv) Usawa . Mfumo wa kodi unatakiwa kuzingatia usawa, usimpendelee mtu na wala usimuonee mtu kwa kuweka tozo kubwa kuliko uwezo na kuwa mzigo kwa mlipaji au tozo ndogo zaidi.

Baba yangu alinihadithia alivyokuwa akikimbia na kukimbizwa na mgambo miaka ya 1970 ili kulipa kodi jambo ambalo hatupaswi kulirithi katika zama hizi, tunayona matunda ya kodi hivyo ni vyema mfumo ukabioreshwa ili kuifanya kodi kuwa rafiki na walipaji kukimbilia kulipa kodi badala ya kukimbia kulipa kodi.

16173125757869071971047105653853.jpg
 
Do you mean give and take, tit for tat, exchange of service in which ones transfer is contingent upon.
Quid pro quo ("something for something" in Latin) is a Latin phrase used in English to mean an exchange of goods or services, in which one transfer is contingent upon the other; "a favor for a favor".

Non quid pro quo (as for tax): giving is a must, receiving is not a must.
 
Ngoja tuongezee juhudi Ktk ulipaji kodi kujiletea maendeleo ktk nchi.Shida inakuja kwenye utekelezaji wa Serikali ktk kutuletea maendeleo Wananchi na vipaumbele vya maendeleo walivyonavyo Wananchi.
 
Ngoja tuongezee juhudi Ktk ulipaji kodi kujiletea maendeleo ktk nchi.Shida inakuja kwenye utekelezaji wa Serikali ktk kutuletea maendeleo Wananchi na vipaumbele vya maendeleo walivyonavyo Wananchi.
Naam!.. mifumo ikiwa mizuri na ya haki Wananchi hawana tatizo kabisa. Ushauri alitoa Mheshumiwa Rais wa kuongeza walipa kodi ni jambo zuri sana kwani litawapunguzia mzigo waliokuwa wamelemewa.
 
Back
Top Bottom