Uhuru wa Maoni na Kuabudu: Serikali ya Rais Magufuli itakipata inachokitafuta

Tukwazane Taratibu

Senior Member
Dec 20, 2012
195
537
SERIKALI YA MAGUFULI ITAKIPATA INACHOKITAFUTA.

Na Josephat K. Nyambeya

Kupungua na hatimaye kutoweka kwa uhuru wa kujieleza, kukusanyika, na kupata habari. Kwa mwenendo huu kuna hofu kuwa hata uhuru wa kuabudu uko mashakani.

Tulianza kuona Askofu Kakobe akizongwa zongwa baada ya kutoa maoni yake juu ya serikali ya awamu ya 5 na kumshauri Rais wa serikali ya awamu hiyo atubu ili asamehewe dhambi zake. Neno lile liliwawasha mwili mzima viongozi wa awamu hii na kuanza kuruka ruka kila mmoja kwa staili yake, mara kiduchu tukawaona TRA wakimfuata na kumfanyia uchunguzi wa fedha zake na kanisa baadae wakatoa ripoti yao. Cha kushangaza kwenye ripoti ile wakamadai kwamba Kakobe kamuandikia barua Magufuli akimuomba msamaha juu ya kile alichokihubiri siku ya kristmass. Watu tukajiuliza je ni mamlaka ya TRA kusemea barua za ikulu? Na je ikulu hakuna usiri kiasi cha kwamba barua anazoandikiwa Rais hadi TRA wazipate? Tukiwa tunaendelea na tafakauri hiyo Kakobe akajitokeza na kukanusha habari hizo za kumuomba msamaha huyo aliyemwambia atubu, akatusomea barua ile aliyomuandikia Rais hadharani, haikuwa na sehemu yoyote iliyoonyesha akiuomba msamaha zaidi aliyendelea kumsisitiza kufuata utaratibu wa Kimungu katika uendeshaji wa nchi.

Hatujakaa tukasahau akaitwa na uhamiaji wakimtuhumu kuhusu uraia wake, wakamhoji vya kutosha kisha wakabaki na pasipoti yake (ambayo sina uhakika kama wamekwisha mrudishia), waaendelea kumpleleza hadi kijijini kwao. Kwa mujibu wa taarifa za magazetini ni kwamba kuna kikosi kutoka makao makuu kilitumwa mwezi April huko Kigoma kuchunguza kama Kakobe ni mzaliwa wa Tanzania au Burundi, walichokutana nacho wanajua wenyewe. Nadhani wamerudi Dar es Salaam kwa aibu kubwa.

Kwa nini nimeamua kuanza na stori hii ndefu, kwa sababu nauona muelekeo wa nchi ukituelekeza shimoni, tena shimo refu tusilojua kina chake. Nchi inageuka kwa kasi sana katia mifumo yake ya uendeshaji, awamu hii inataka kutuaminisha ya kwamba sauti ya mtu mmoja ndio inaweza kuamua mstakabali wa watu wote Mil 55 wa nchi hii, totally wrong.

Baraza la maaskofu wa KKKT na wale wa katoliki (TEC) kwa vipindi tofauti katika mwezi wa mfungo wa Kwaresma walipata kutoa maoni yao juu ya mwenendo wa nchi, walizungumzia maeneo mbalimbali ikiwemo uchumi, elimu, siasa, afya, demokrasia na hata muonekano wa nchi kwa ujumla wake.

Maaskofu wote wa KKKT na TEC wametumia wajibu wao wa kikatiba kama unavyooneshwa katika katiba ya nchi kifungu cha 18 cha kutoa maoni yao, pili walitimiza wajibu wao kueleza nchi iendako kwa macho yao ya kiimani, maana sote tunatambua ya kwamba viongozi wa dini ndio wenye uwezo wa kuona kuhusu yajayo kwa macho yao ya imani.

Waliyatenda haya kwa kusimamia misingi ya Biblia waiaminiyo.

"Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
.Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote." Waebrania 13:17

"Nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu." Yeremia 3:15

Vifungu hivyo vichache tu kati ya vingi katika Biblia vinawapa uhuru na uwezo viongozi wa dini kutulisha maarifa na ufahamu sisi waumini wao kwa maana wao ndio wenye mamlaka duniani hapa kuyatenda mambo hayo na pekee wamepewa uwezo mkubwa wa kiroho kuona tusivyoweza kuviona kwa macho.

KWA NINI TUWAANDAME KWA KUSEMA UKWELI?

Leo mchana nimekutana na barua mtandaoni , barua hii inadaiwa kuandikwa na msajili wa vyama nchini kwenda kwa Askofu mkuu wa KKKT akimtaka afike ofisini kwake ajieleze na kwenye barua hiyo kuna mambo kadhaa yamezungumzwa, ikiwemo baraza la maaskofu wa KKKT kutotambuliwa na msajili huyo. Mwisho wa barua msajili akamtaka Askofu mkuu wa KKKT ajieleze kwa nini walitoa tamko la maaskofu mwezi Aprili ? Na akamtaka alifute tamko lile kwa njia ile ile waliyoitumia kulitangaza tamko lao. Nimehuzunika sana. Nadhani siyo Tanzania niijuayo mimi hii, labda tumebadilishiwa nchi yetu.

KKKT wamekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka 100 sasa, wamekuwa wakiendesha shuguli zao za utume kwa miaka mingi bila matatizo yoyote, iweje leo baada ya kutoa tamko la kuiknya serikali juu ya mwenendo wake kwa wananchi ndio waambiwe hawatambuliwi na ofisi ya msajili, ofisi ya msajili ilikuwa wapi kipindi chote cha miaka 54 kufuatilia taasisi hii ya KKKT? Bad enough msajili huyu amekuwa ofisini kwa mda mrefu hata kabla Magufuli hajaingia madarakani.

Mwenye macho haambiwi tazama, tuendako kuna giza tele. Barua ya msajili imekuwa na maneno makali na ya vitisho kwa KKKT ikionesha dhamira ya ofisi hiyo kwa KKKT endapo watashindwa kutekeleza matakwa yaliyomo kwenye barua, vitisho hivi vina mkono wake na mkono huu siyo wa msajili.

Katika nchi za Africa kumekuwa na imani ya kwamba ili uweze kuitawala nchi utakavyo basi kwenye kila kitengo weka watu wanaocheza mdundo wako, barani Africa kumekuwa na viongozi wasiotaka kusikiliza mawazo mbadala. Wao wanaamini kwamba eti "MAWAZO NA FIKRA ZAO NDIO HATIMA YA TAIFA".

Nipende kuwakumbusha serikali kupitia kwa ofisi ya msajili wa vyama ya kwamba "Ngoma ikilia sana hupasuka" na mwanzo wa ngoma ni lele. Wasijitoe ufahamu na kujitia upofu wakashindwa kuliona taifa hili liendako. Vilio vya wengi ni vilio vyenye ishara za kishindo kikuu, msiiikatae na kutosikiliza maneno ya wazee hawa maaskofu wa madhehebu haya mawili makubwa nchini (KKKT, RC) kwa sababu wamekanyaga nyayo zenu bali mkae mtafakari juu ya hayo waliyowaelezeni na kujitathimini.

"Lakini hawakusikiliza, wala hawakutega masikio yao, bali walifanya shingo zao kuwa ngumu, ili wasisikilize wala wasipokee mafundisho." Yeremia 17:23

"Unaona mambo mengi, lakini huyatii moyoni; masikio yake ya wazi, lakini hasikii." Isaya 42:20

Kuendele kuwtafuti njia za kuwakomoa au kuwafuta kabisa katika ramani ya utume katika nchi ya Tanzania ni kuendelea kuwakomaza na kuwatengeneza akina Padri Wenseslaus Munyemshyaka wa Rwanda na wenzake ambao wao kwa ajili tu ya maslahi yao binafsi walikubali kuungana na serikali ya Kihutu kuwaua na kuwaangamiza kabisa Watutsi waliokuwa wakiombea usawa katika taifa hilo. Walithubutu kuwaleta askari wa Intarahamwe makanisani walikokuwa wamejificha waumini na wasio waumini ili wawaue na kuwateketeza kabisa, serikali yetu inatuonyesha njia hiyo na inatoa "signal" kwa maaskofu kuelekea huko, kuacha kunena ukweli na kuwa vipaza sauti wa uovu.

Wabudha wana msemo wao waupendao sana "Three things cannot be long hidden: the sun, the moon, and the truth."

Ukweli, jua na mwezi ndio vitu pekee visivyoweza kufichika duniani. Watanzania siyo wajinga hadi washindwe kuuona ukweli juu ya nchi yao, wanajua waendako, wanajua nchi iendeshwavyo, wanaujua ubabe unaotendwa kwao kutoka ngazi mbalimbali za nchi. Hivi ni nani leo asiyejua mambo ya nchi hii?

Tuwaache maaskofu watende mambo yao ya kitume bila ya kuwabugudhi, wakienda kinyume na sheria za nchi na kutenda kama Mapadri wa Rwanda ya 1994 tuwachukuliie hatua kwa mujibu wa sheria zetu maana watakuwa wamekengeuka kutoka kwenye viapo vyao vya utume.

Niwatie moyo maaskofu wa KKKT, TEC na hata viongozi wote wa dini ikiwemo wachungaji msikatishwe tamaa na mawimbi haya ya mda mfupi, yatapita tu na neno lenu litabaki kusimama daima na hata dahari. Mtakuwa wanafiki sana KKKT kama mtalikana tamko lenu mlilolitoa kwa maono yenu, mtawaangusha wengi kama mtakubali kurudisha mikia nyuma na kuyala matapishi yenu.

Biblia inasema katika 2 Timetheo 4: 2 kwamba "Lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa,karipia,kemea,na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho."

Huu ni wakati usiowafaa, mko katika vita ya ukweli, uongo na unafiki. Mmoja kati ya hizo atashinda.

Naamini hili nalo llitapita na taasisi yenu ya KKKT itasimama na kuimarika zaidi.

Na kila mmoja aseme Amen.

nyambeya@yahoo.com
 
Nchi hii inaelekea kwenye laana kubwa......

Hivi hawa watawala hawajui kuwa hawa watumishi wa Mungu wanatekeleza Yale mambo ambayo wanaelekezwa na Mungu wetu?

Askofu Kakobe alipomwambia Mkulu atubu ni maelekezo toka kwa Mungu kuwa atubu.....

Kitendo cha kukaidi maelekezo hayo, asidhani kuwa amemgomea Kakobe aliyeagiza Bali amekaidi agizo la Mungu mwenyewe!

Kwa hiyo tusubiri nchi yetu ipate kipigo kikuu toka kwa Mungu Mkuu na mwenye utukufu na ambaye ukuu wake huwezi kuufananisha na binadamu yeyote!
 
hiki ni kioja kingine .....Huyu samaki mkubwa Mkuu, hutaweza kummeza atakukwama tu kooni
 
Mungu amejibu maombi yetu.
kwamba sasa ameleta njia mbadala ya kuiondoa CCM madarakani.

kwamba CCM wamejiandikia obituary yao wenyewe kwa kuanzisha vita dhidi ya Mungu.

eeh Yehova Nisi....shusha ule moto ulao shusha!
angamiza kabisa watesi hawa ili Watanzania tupone.

Amen.
 
Back
Top Bottom