Uhuru wa kuzungumza kwa wenzetu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,900
30,235
Filamu, ''JFK'' iliyotengenezwa na kuogozwa na Oliver Stone ilinikuta niko mji mmoja mdogo Uingereza.

Mwaka ni 1991.

Huyu Oliver Stone ni Mmarekani na sifa yake yeye ni kule kutengeneza senema za kushambulika mamlaka.

Oliver Stone akishambulia serikali yake ya Marekani na watendaje wake wakuu.

Hii senema ya JFK Oliver Stone kaitengeneza kutokana na kitabu cha mwanasheria mmoja aliyefuatilia kesi ya kuuliwa John Kennedy akijaribu kudhihirisha kuwa wauaji wa Rais Kennedy ni watendaji wenyewe wa serikali yake waliokula njama kwa kuwa alikuwa nataka kumaliza vita ya Vietnam.

Hili wao hawakulitaka kwa kuwa walikuwa na maslahi makubwa katika vita ile wakijipatia mapesa mengi kutoka makampuni ya kutengeneza silaha.

Wanaita Gala Openning yaani siku ya mwanzo kuonyesha filamu na hii wanafanya kwa wakati mmoja katika miji mikubwa ya ulimwenguni.

JFK ilikuwa imefanyiwa ''publicity'' kubwa sana kwa nia ya kupata faida kubwa katika maonyesho ya filamu hiyo.

Miji mikubwa duniani Los Angeles Hollywood kwenyewe, New York, Boston, Washington, London, Glasgow, Paris, Marseilles, Hong Kong yaani dunia nzima filamu imefika tayari kuonyeshwa.

Televisheni, FM Stations zote Uingereza ukifungua stori ni JFK.

Mimi nasikiliza yote haya kwenye radio na wakati mwingine naona kwenye TV.

FM Station maarufu ya mji wangu katika nyingi zisizo hata na hesabu inaitwa ''Dragon.''

Sikuchoka kusikiliza matangazo ya JFK.
Siku ya siku imewadia.

Ukweli ni kuwa mimi nilikwisha poteza kupenda senama baada ya Tanzania kukumbwa na balaa ikawa kila kitu hakuna kukawa filamu za Hollywood zikawa haziletwi tena nchini.

Zikabakia filam za Kung Fu.

Kwa hiyo nimefika Ungereza sina hamu kabisa ya kuangalia filamu na kwa miaka mingi siwajui hata waigizaji maarufu.

Nilikuja kuwajua Denzel Washington, Julia Roberts, Robert de Niro na wengineo baada ya kufika Uingereza.

Nilikuwa na rafiki yangu kijana wa Kigiriki jina lake Panothiakis George Foundas, mwanafunzi mwenzangu na tunaishi nyumba moja.

Huyu George Foundas alikuwa muigizaji mkubwa na alipata kucheza filamu moja na Anthony Quinn, bingwa katika mabingwa waigizaji Hollywood.

Mwanae ndiye huyo Panos kama tulivyozoea kumwita.

Yeye ndiye aliyenitia mashamsham twende tukaione JFK.

Ilikuwa wakati wa winter, baridi kali lakini nilimkubalia kwenda.

Zaidi kilichonivutia yalikuwa maneno ya Oliver Stone aliyosema katika mazugumzo na waandishi wa habari siku ya uzinduzi wa filamu yake hii JFK.

Oliver Stone kaulizwa, ''Kwa nini wewe senema zako zote unashambulia serikali?''

Oliver Stone akajibu akasema,''Watu wengi sana hawajui kuwa ile White House imejaa majambazi watu wanadanganyika na zile suti mle ndani.''

Kwangu mimi yale yalikuwa maneno mazito ya kushtusha na kwa yakini yake Oliver Stone amemtukana Rais George Bush.

Anasema maneno yale wasikilizaji waliokuwa kwenye hadhira ile wanaangua vicheko.

Yule mtangazaji alikuwa mtu hodari pale pale akapiga simu tukaunganishwa na mama yake Oliver Stone mubashara anaulizwa maswali kuhusu mwanae na yale aliyokuwa amesema.

Mama yake akasema, ''Mwanangu Oliver toka utoto wake ni mtu wa matatizo tu.

Siku moja mwaka wa 1969 vita ya Vietnam imepamba moto, siku zote tunapokea maiti kutoka uwanja wa mapambano Oliver kanipigia simu ananiaga ananiambia kuwa ''Mama nakuaga nimejitolea kwenda Vietnam kupigana.''

Ikawa kama vile yule Bi. Mkubwa anatudhihirishia sisi tuliokuwa tunamsikiliza mwanae akitukana serikali kuwa tumpuuze kwani mwanae ni punguani.''

Ikapita miaka mingi nikajikuta niko New Jersey, Marekani nyumbani kwa familia moja mtu na mkewe wote ni wasomi wa haja.

Kuna jambo moja lilinishagaza hii familia watoto wao wote walikuwa kwa miaka mingi wapo kwenye "cast" ya "The Sound of Music," katika theatre.

Wananiambia, ''Kesho tutakuwa na maandamano makubwa New York, Manhattan uje na wewe tuilani hii serikali ya wahuni inayotuletea vita dunia nzima.''

Nikijibanza Manhattan na si mbali na New Jersey.

Mimi nimeshtuka kusikia maneno yale.

Siku ya pili mimi nimetoka tena kwa miguu kwenda sehemu ambayo ilipangwa maandamano kufanyika.

Sijafika niko mbali nasikia sauti za loud speaker watu wanazungumza, nyimbo zinawekwa ili muradi nimefika nimekuta watu wengi na mabango na polisi wapo wengi vilevile.

Waandamanaji hawatulii sehemu moja wanazungumza kisha wanahamia mtaa mwingine ilimuradi utadhani ni ''carnival'' ya Brazil wanataka Barack Obama na kundi lake watolewe madarakani nk. nk.

Jua lilipoanza kuzama mitambo yote ikazimwa hao watu wanaondoka wanarudi majumbani kwao salama.

Nimetazama pale sikuona magari ya washawasha wala askari waliobeba marungu mazito, ngao za chuma na silaha.

Pembeni ya barabara naona wamachinga wa New York wamefata soko pale wanauza vitu vyao pamoja na ice cream na maduka yako wazi biashara zinaendelea na hakuna dalili ya hofu yoyote.

Nikajiambia kwetu nyumbani ingekuwaje maandamano kama haya?

Pangekosa kupigwa mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji?

Maduka yangesalimika?

Vioo si vingekuwa vimesambaa barabarani kutokana na kuvujwa kwa maduka?

Usiseme majeruhi na waliokamatwa.

Turudi Uingereza.
Shule yetu haikuwa mbali na kati ya mji.

Kwa mwendo wa maandamano dakika 10 tushafika tulipokusudia tunashambulia.

Maandamano yetu tukifanya tukijisikia.
Tunakwenda McDonald's kuwalani kwa ukatili dhidi ya ng'ombe.

Kwa nini wanachinja ng'ombe kutengeneza hamburger?

Tutawakuta askari zamani wameshafika wanatusubiri kwa amani.

Tutasimama pale tutapiga kelele hadi kifu yetu.

Kisha hao tutarudi chuoni salama salimini kuendelea na masomo.
 
Huku hatuna uvumilivu
 
Mzee Mohamed huko ni duniani huwezi kufananisha na huku kwa wakoloni weusi.
 
Back
Top Bottom