Uhuru wa kuabudu nao umeanza kuondoka...(?)

Uhuru wa kuabudu nao umeanza kuondoka...(?)

eti bavicha wanafanya maombi!! eti wamenyimwa uhuru wa kuabudu!!! mi nacheka saaaaana!! na hizi siasa uchwara. hivi ni lini bavicha imegeuka kuwa zehebu!? hadi kufikia kunyimwa uhuru wa kuabudu!!?. hahahahahaa huu ujanjaujanja haujawahi kuicha salama hii bavicha

Mkuu kuomba wakati washida kulikuwepo tangu enzi za ujima

1. Wazee walikusanyika kutoka pande zote kuomba endapo mvua haikunyesha

2. Watu walikusanyika kumuomba Mungu nyakati za majanga bila kujali makabila, itikadi au rangi zao

Tumeona haya yakitendeka.......
 
Kuna watu wanaabudu Ng'ombe lkn hawajakatazwa, kwani hapa tatizo nini hasa. Kumuombea Lisu kunaipa serikali tabu gani?
Mkuu mie naabudu Mungu na naenda kwenye nyumba yangu ya ibada kuabudu sijaona katazo lolote.
 
Spika wa Bunge anaongozwa na kanuni za bunge. hata kwenye mikutano ya kisiasa inaruhusiwa kuanza na sala, lakini hauwi mkutano wa maombi, unakuwa mkutano wa siasa. Je huo wa Bavicha ulikuwa mkutano wa nini?

Chama cha siasa kimesajiliwa kufanya siasa, kesho na kesho kutwa viongozi wa dini wakiandaa mikutano ya kisiasa mtakuja hapa kulalamika.

Tuache kila taasisi ifanye kazi kwa mujibu wa usajili husika.
 
Mipaka ya Uhuru wa kuabudu Tanzania unaisha punde ukimuombea shujaa Lissu.
 
Spika wa Bunge anaongozwa na kanuni za bunge. hata kwenye mikutano ya kisiasa inaruhusiwa kuanza na sala, lakini hauwi mkutano wa maombi, unakuwa mkutano wa siasa. Je huo wa Bavicha ulikuwa mkutano wa nini?

Chama cha siasa kimesajiliwa kufanya siasa, kesho na kesho kutwa viongozi wa dini wakiandaa mikutano ya kisiasa mtakuja hapa kulalamika.

Tuache kila taasisi ifanye kazi kwa mujibu wa usajili husika.

Kwa uelewa wako kunakifungu chochote cha katiba au sheria kinaendana na usemayo.

Hebu kiweke hapa....

Taifa haliendeshwi kwa hisia za mtu tu anavojisikia
 
Mkuu alianza vizuri mwanzoni kutumbua majipu na kuzunguka kukagua miradi kwa kushtukiza.
Mpaka kila mtu akajua kuwa kufukia 2020 hakutakua na haja ya kampeni mana hata mitandaoni mijadala ilikuwa imepotea kabisa.
Kosa kubwa lilianzia pale bunge lilipoanza kuzuiwa. Watu wakaanza kujiuliza kunani mpaka mawaziri hawataki kupigwa maswali magumu na kutupiwa lawama live wakati wameajiriwa kwa kodi ya watanzania?
Watu wakaanza kupata mambo ya kupigania. Hoja ya bunge LIVE ikaanza. Watu wakapata mahali pa kushika. Sababu za mapungufu zikaanza kutajwa kwa kurejea na bunge live. Laite wangeshtuka na kuliweka Live mkuu wa nchi angehamishia udhaifu wa serikali kwa wabunge wanao lala bungeni.

Mambo ya mpasuko wa kisiasa kule Zanzibar nalo pia lilikua ni jambo la kuliundia tume kama alivyofanya Mkapa na JK sio kwa lengo la kumwondo aliyeapishwa la hasha bali kwa lengo la kumfariji aliyekosa kwa shingo upande. Wote ni watanzania na wazanzibar tulipaswa tusiishi kwa namna hiyo bali upendo hata kama mmoja hajaridhika ni watoto wa baba mmoja tulitakiwa tuwaite kwa pamoja na kuwapatanisha.
Biblia natuambia kuwa heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu. Hili nalo likaleta visababu ambavyo wala havikuwa na umuhimu kama taifa moja.

Akaja tena na katazo la mikutano ya kisiasa.
Ikaleta tena sababu za udhaifu wa serikali. Hili likaibua tena mijadala. Watu wakawa hawafuatilii tena masuala ya utendaji bali haya mapungufu ambayo hayakuwa na sababu yoyote mana yapo kikatiba.

Wakaja tena na makatazo ya kutembeleana kati ya wanachama wa chama kikubwa na vile vinavyopingapinga. Watu wa chama kikubwa wakajikuta wanalazimika kujionyesha kuwa wanafuata kauli hizo kwa speed kubwa na kuonyesha misimamo mikali kama gia ya kwenda na speed.

Watanzania wakakatazwa tena kutembeleana kwenye majimbo kwa lengo la kuhamasisha maendeleo kama hawajachaguliwa na watu wa eneo lake.
Yani kama wewe ni mtu kutoka X ubaki huko huko X ukionekana unazungumza na watu wa Y basi inakuwa ni kosa la kukuweka ndani masaa 48 na kupelekwa mahakamani ukatokee huko . Chuki ikaingia miongoni mwa watanzania.Watu wakawa hawatembeleani wala kusalimiana kama tulivyoona wakati mmoja mtu akipewa mkono na kuukataa.
Na wito ukatolewa kuwa alipaswa asisainiwe hata fomu zake za matibabu . Lilikua ni jambo jepesi tu la kufanya kazi ya wana wa Mungu ya kuwaita na kuwapatanisha kwa kumwambia hii hapana kwa nini unakataa kusalimiana na mwenzako. Unajenga taswira gani kwa wananchi. Bila shaka mambo yangeenda vizuri sana.

Ubinadamu ukaanza kutoweka taratibu. Watu wakawa hawaoni tena thamani ya binadamu. Kule kibiti watu wakawa wanaua kwa makusudi kabisa.

Wengine wakawa wanapotea.

Leo hii watu tena hawafuatilii nani kafanya zuri lipi bali nani aliyefanya baya lipi?

Haya yote yamepoteza uelekeo wetu wa kuelekea kwenye nchi ya viwanda na sasa watu wanaishi kwa jazba na kukimbizana na vikundi vya wanamaombi wanaomlilia Mungu kuhusu kesho yao.

Nchi ikimwaga damu zisizo na hatia kinachofuata ni watu wema wasio na nguvu kulesha na kumwomba mana hawajui siku wala saa ya damu yao kumwagwa.

Wachamungu tusimame na kumwomba Mungu aturejeshee amani ya mioyo yetu. Watu wabishane kwa upendo na baada ya kubishana washikane mikono.
Wakati ule wa kuitana mafisadi kuna watu walitukanwa sana tena kwa maagizo lakini walikua wanasamehe na kucheka wanapokutana iwe kwenye shida au raha.

Naamini kwamba tunaweza kupambana na ufisadi na uzembe bila kuuana. Tuwaondoe wale viongozi wanaotuhumiwa wakae pembeni sio kuwaondoa wanasiasa wasio na hatia ili washindwe kufanya kazi zao.

Tuwatishe wanaoiba mali za umma sio kuwatisha watu wanaosoma dua. Ni ajabu kabisa kama tutaona watu waliovaa tisheti za kuhamasisha maombi wakifungwa ili hali walioiba mali za umma wakila bata mitaani.

Kuvaa nguo yenye nembo na maandisho ya kumwomba mwenyezi Mungu sio kosa lakini kuna watu wanaitangazia na kuionya jamii kuwa wajiepusha na nguo hizo na kuachana na kumwomba Mungu aponye wagonjwa na aiepushe nchi yetu dhidi ya wauaji na watu wabaya wasiojulikana

Mwanahabari Huru
 
Nyie ongeeni sana ila ikulu mtaishia kuiona kwenye buku na kupisha msafara wa Magufuli.
 
Back
Top Bottom