Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,726
Tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, uhuru na sura zake mbalimbali, umepungua au kwisha kabisa. Ilianza na kuondoa uhuru wa kukutana/kukusanyika - wananchi wakavumilia.
Ikafuata uhuru wa kujieleza. Siku hizi polisi wetu ni rahisi kumkamata mtu aliyetoa maoni yake mtandaoni kuliko kumkamata mwizi au jambazi anayevamia benki. Kila kukicha ni kukimbizana na vijana wanaotoa mawazo yao mitandaoni. Hili nalo likavumilika.
Uhuru wa kupata habari nao ukasombwa na sheria mpya. Waziri wa habari siku hizi anaweza kufungia gazeti, redio, TV mpaka blogu. Waziri asiye na bajeti ya kusomesha waandishi wa habari, ana bajeti ya kununua pingu za kuwafunga wanapotoa mawazo yao. Anafungia gazeti kwa kusema uwongo; baada ya wiki, serikali inamtumbua mtu aliyetajwa katika habari iliyofungia gazeti hilo!
Sasa uhuru wa kuabudu nao umeingiliwa. Spika wa bunge ana mamlaka mpaka misikitini na makanisani. Nguvu ya spika kuamuru kukamatwa kwa mbunge aliyeonekana kanisani akiabudu imetokea katiba gani? Nguvu ya polisi kuzuia wanaotaka kukutana na kufanya sala/dua imetokea katiba gani? Ibada na imani ni mambo binafsi ya watu. Wako wanaoabudu "mungu" wao aitwaye Ndugai lakini wapo wenye shetani wao aitwaye "bashite". Wote hawa wana uhuru usiopaswa kuingiliwa kwa sababu ni imani.
Tutaanza kupata wakimbizi wanaokimbia nchi.