Uhuru: Bajeti yakuna wengi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhuru: Bajeti yakuna wengi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Landala, Jun 16, 2012.

 1. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Habari za leo wanajf,muda si mrefu nilikuwa napitia vichwa vya habari vya magazeti mbali mbali nikakuta kwenye gazeti la Uhuru likisema 'BAJETI YAKUNA WENGI'hivi watanzania wenzangu ni kweli hii bajeti ya 2012-2013 imekuna wengi au hili gazeti la CCM la uhuru linataka kupotosha umma ili kuitetea serikali yao ya magamba..
   
 2. Bornvilla

  Bornvilla JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 925
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Imeakuna wenyewe tu! Hakuna lolote! paye inazidi kupanda, we unategemea nini?
   
 3. BJEVI

  BJEVI JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  HILI NI GAZETI MFU ,HATA HAYA INGAWA NI YA KWELI WAKIAANDIKA WATASEMA KINYUME.

  SOMA HAPA.


  Tangu kuingia kwa mchezo mchafu wa kikundi cha watu tena wachache kujihudumia na kutafuta utajiri kwa kuwauza wenzao, Tanzania si salama ingawa hakuna milio ya bunduki.

  Uliza. Yako wapi mapambano dhidi ya ujambazi, ufisadi (ugamba), biashara ya mihadarati, kurekebisha mikataba ya kijambazi ya uwekezaji ambao ni uchukuaji na uwajibikaji? Si siri.

  Kwa sasa Tanzania iko mikononi mwa maharamia tuseme majambazi hasa kiuchumi. Imefikia mahali majambazi yaitwayo wawekezaji yanakuja na kutuibia mchana kweupe kwa kushirikiana na wenzetu waroho wachache tuliwaamini.

  Uliza uwekezaji kwenye Shirika la Reli uliishia wapi ilipoingia kampuni ya Kihindi iitwayo RITES?

  Mijitu inakuja bila hata senti halafu eti inawekeza kwa kuilazimisha serikali iwape mikopo ili waendeleze mradi! Ni wawekezaji wangapi wanakuja na briefcases zao na makaratasi na kurejea kwao wakiwa na magunia ya dola?

  Uliza. Ni wawekezaji wangapi hasa kwenye madini wanamiliki ndege na viwanja binafsi vya ndege wanavyotumia kutoroshea madini yetu bila kukaguliwa?

  Ni wangapi wanachafua mazingira na hakuna anayewawajibisha?

  Hebu zidi kupiga mbizi kwenye uchafu huu uone mengi. Hakuna ujambazi wa wazi kama unaofanywa na makampuni ya simu kwa sasa.

  Wanakuja na kuweka mitambo chakavu halafu wanawatoza Watanzania viwango vya juu vya kutumia simu.

  Huwa najiuliza. Inakuwaje kupiga simu, kwa mfano, kutoka Canada kwenda Kenya nitozwe senti tano za dola na Tanzania nitozwe senti 27 za dola kwa dakika?

  Wakati viwango vya Kenya ni vidogo, mawasiliano baina ya Kenya, Uganda, Rwanda hata Burundi ni bora na rahisi wakati Tanzania ni utapeli mtupu.

  Mtu unapiga simu unaambiwa ongeza salio, mara namba ya simu haipo, mara simu inatumika mara hili mara lile.

  Kwanini hatusikii upuuzi huu tunapopiga nchi tulizotaja hapo juu kama hakuna namna?

  Ajabu ya maajabu, kila mwaka makampuni ya simu yanabadilisha majina ili kuendelea kufaidi msamaha wa kipuuzi wa kodi.

  Angalia mahoteli yenu yanavyobadili majina na wamilki kila baada ya miaka mitano ili kuendelea kufanya biashara bila kulipa kodi. Angalia watu wanavyouziana makampuni waliyookota Tanzania kwa bei ya kutupwa.

  Anayebishia hili ajikumbushe Richmond ‘ilijiuza’ kwa Dowans kwa bei gani ikilinganishwa na bei ya maandishi tu bila kulipa pesa iliyoianzishia biashara hii hewa.

  Leo tunaambiwa kuwa pesa tunayoilipa IPTL, kwa mfano inatosha kununua na kujenga mitambo bora na mikubwa kuliko tunayolipia.


  Je, kwanini tunaona kujikomboa ni dhambi wakati tukiabudia maangamizi kama haya ya IPTL na makampuni mengine mengi ya nishati.

  Je, hapa hakuna rushwa na ufisadi vya wazi? Je, wahusika hawajulikani? Nani anawagusa wala kuwashughulikia? Tunakwenda wapi?

  Imefikia mahali watu wakiuliza ni kwanini uchafu huu unaendelea wakati kuna mamlaka, wanakufa kwenye mazingira ya kutatanisha. Jiulize. Mbunge wetu mmoja alipatwa na nini baada ya kuhoji ni kwanini alikuwa akiona watumiaji wa mihadarati hadharani ambao wangeweza kutuonyesha wanakonunua madawa.

  Tufikie mahali tuambiane ukweli bila kuogopana wala kufichana. Bila kufanya hivyo na kubadilika nchi yetu itaishia pabaya.

  Ni juzi juzi serikali ya Mali imeangushwa kutokana na hasira za jeshi kushuhudia wauza unga wakiwa ndani ya serikali na serikali isifanye kitu kwa vile wakubwa zake walikuwa wakinufaika na uchafu huu.

  Je, sisi tu salama na hawa wauza unga na majambazi wa kiuchumi waliotapakaa nchini mwetu? Je, wananchi wataendelea kugeuzwa mbuzi wa shughuli kila mwaka?

  Huwa siachi kusema kuwa Watanzania ni viumbe wa ajabu hata kama hawana mikia au macho kisogoni.

  Maana ukiangalia kwa mfano, rasilimali zao zinavyoibiwa, wanavyolanguliwa huduma kama vile umeme, simu na mahitaji mengine na wakaendelea kuvumilia unashangaa hawa ni watu wa namna gani.

  Nani kwa mfano anakumbuka na kuhoji ile kashfa ya utoroshaji wanyama iliyotokea Novemba 24, 2010 ambapo ndege ya kijeshi ya Qatar ilifanikiwa kutorosha wanyama mbali mbali 130 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro?

  Je, kama KIA wana uwezo wa kutorosha wanyama hai na wengi kiasi hiki wanashindwa nini kuingiza maelfu ya tani za unga?


  Ukitaka kujua nini namaanisha, watafute wafanyakazi wadogo na wa kawaida viwanja vya ndege uone walivyo matajiri wa kutupwa.

  Unadhani pesa hii wanaipata wapi kama si kuruhusu uchafu na jinai kama ile ya KIA......................

  Nenda TRA, Bandari, Uhamiaji. Mambo ni yale yale. Uchafu, uchafu mtupu. Nani anajali iwapo wanaofaidika wameweka watu wao kufanya kazi hiyo? mfano, vituo vyetu vya mipakani vimegeuzwa maduka ya wezi wachache kupitisha wamtakaye na wakitakacho bila kuulizwa na yeyote?

  Je, namna hii nchi itakuwa salama? Je, namna hii tunaweza kujisifu kuwa yaliyotokea Mali hayawezi kutokea huko tuendako ambapo wahusika wasiporekebisha hali hii wananchi katika hali yoyote wataamua ‘enough is enough’.

  Tumekuwa taifa la hovyo linalowazawadia watenda maovu!

  Uliza waliotimuliwa madarakani kwa kashfa wanalipwa pesa ya umma kwa kazi gani zaidi ya kupaswa kuwa mahakamani hata magerezani? Tumegeuka taifa la watenda maovu na waovu kirahisi hivi?

  Je, baada ya mchezo huu mchafu Tanzania itabaki nini? Tunaviandalia nini vizazi vijavyo iwapo tunafanya mambo kama mataahira kutokana na kufikiri kwa matumbo badala ya vichwa?
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Hawa mafisadi tusiwahanye sana,kwn hakika siku zao zinahesabika!
   
 5. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ni kweli imemkuna, Nape, Lusinde, Mukama, JK, Mwigulu and the Like, watanzania wasio magamba ni maumivu
   
 6. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Funguka mkuu, zinahesabika kivipi?
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,771
  Trophy Points: 280
  ccm wanajitekenya wenyewe alafu wanacheka wenyewe.
   
 8. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160


  Nteko Vano! Soma alama ya nyakati! Jamaa zako wako ICU.
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Chadema ikiingia madarakani, wamsweke jela huyu mhariri mkuu wa gazeti la Uhuru na vibaraka wa chini yake.
   
 10. Kibada

  Kibada Senior Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha iwakune magamba ili walale usingizi wa pono wakati upinzani unajipanga kuchukua nchi...:A S 39:
   
 11. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  mkuu, imewakuna wao nyinyiemu kwenye masaburi yao.
   
 12. Mnwele

  Mnwele Senior Member

  #12
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 163
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Bora Uhuru kuliko TBCCM maana wao leo ndo wametenda hovyo kabisa katika uchambuzi wa habari magazetini. Waliperuzi Uhuru, JambaLeo na Mtanzania. Ukweli ni kwamba magazeti makini yote leo yameandika kuhusu kupingwa kwa bajeti ndani ya CCM na kwa WTz from all walks of life.
  Wanaendelea kutumikia kafiri
   
 13. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  zimebaki chache unaweza kuzihesabu kwa urahisi sana
   
 14. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  imewakuna kwa sababu ina *****
   
 15. GEMBESON

  GEMBESON JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 255
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hakuna mtu aliyekunwa na Bajeti, labda mseme imewatekenya wengi....
   
 16. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  neno wengi lina maana ya kuanzia watu wawili na kuendelea..kama ilimkuna mwenyekiti pamoja na katibu mwenezi wake inatosha kuandika ni wengi
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu uliyoandika mengi ni kweli, lakini ni vizuri ukikumbuka kuwa huwa wezi kuwa mwislamu kuliko waislamu wa Mecca, au huwezi kuwa mkatoliki kuliko Papa. Kama boss wako mwizi, ina maana gani wewe kuwa mwadilifu? Unajua kabisa kuwa Kiongozi ni mwizi na anaiba pesa ambazo wewe unakusanya, kwanini na wewe usiibe?

  Ukiangalia thread nyingi hapa JF utaona kuwa yote unayosema yamesemwa sana, na conclusion iliyofikiwa ni kuwa mtaji wa CCM [unyonge wa wananchi kielimu] ni mkubwa. Hadi unyonge huo utakapoondolewa hakuna kitakachokuja badilika hata kelele zipigwe vipi. Mfano wazi ni wezi wa EPA wameibia mabilioni lakini wapo wanatesa mitaani tena na kutukejeli, lakini wanaoiba kuku kwa njaa wanapigwa hadi kufa.

  Ukisema ukweli yatakukuta kama yaliyomkuta Kolimba au kama yaliyomkuta Mwakyembe, ni bora na wewe uwe CCM chukua chako mapema na ukae kimya.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,443
  Likes Received: 81,492
  Trophy Points: 280
  Unategemea nini kiandikwe na gazeti la magamba kama siyo kuifagilia Serikali ya magamba? Eti bajeti imekuna wengi!!! Daaaaah!!!!
   
 19. sam2000

  sam2000 JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Hakuna tofauti kati ya gazeti hili na yale ya mia 300!!!
   
 20. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nafikiri gazeti la Uhuru hawajakosea, bajeti imekuna wengi vichwani. Mtu anapojaribu kutafuta jibu ambalo haliko karibu huwa anajikuna kichwani. Sasa hii bajeti ni kweli lazima watu wajikune vichwani maana haina majibu kabisa kwa watanzania especially walala puh na mimi nikiwemo. Tanzania haina vyanzo vingine vya mapato zaidi ya kupandisha kodi kwenye soda, bia, sigara......watu wakigoma kuvuta sigara na kunywa pombe sijui serikali itapata wapi hela. Na huko ndiko tuendako.
   
Loading...